Kwanza rejea maoni yangu hapo juu kwamba Baba yako akijenga nyumba kwenye kiwanja cha familia ulipokulia unapofikia kuwa mtu mzima ikawa na muonekano wa design ya kizamani hutakiwi kuibomoa bila ridhaa yake na hata ukimuomba akuhurusu atakuambia jenga ya kwako kwanza kabla hajafikiria kukuruhusu uibomoe. Hilo nataka uelewe kwanza. Halafu kumbuka Nyerere alipochukua uongozi wa nchi hapakuwa na hata kimoja, kulikuwa kweupee! Akaanza na mashule, vyuo, mashirika, viwanda nk. Sasa nikuulize ni nani aliyekutana na changamoto zaidi, aliyevikuta vipo ila havikuwa vinazalisha kama ilivyotegemewa au ni aliyekuta mapori akafyeka akavijenga?