Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Kazi ya elimu kwa umma wote ni muhimu, na kazi ya wasomaji wote na wasikilizaji wote ni kuelimika na kuchukua hatua wakiwemo hao unaowasema, maana naona mwenzetu wewe ni xray ya familia za watu. Sasa endelea kupiga xray na mimi niendelee na kazi yangu ya elimu kwa umma, na ukipiga xray yako ukabaini wagonjwa wa familia mbalimbali utawaleta tuwatibu. Sawa? Kila mmoja afanye kazi inayomhusu ili twende kasi zaidi. Hatuna muda
Ahaa haaaah Madam Eti Xray. That was beyond that, its MRI. Though no ill intentions Dr.
 
Mh kati ya wanaoongoza kwa Ushenzi na Ufilauni ni nyinyi viongozi wa chama na serikali ,wateuliwa,wafanyabiashara wakubwa,mkiwa kwenye V8 mnawalamba sana watoto wa 2000.
 
Wasaalam wote.

Huenda visa viko vingi ila, vinafichwa na kimoja kati ya hivyo ni kama hiki ambacho, kimefikishwa kwangu kwa ufupi:

...."Nimefanyiwa ukatili na mtoto wa boss kwa kupigwa sana kisa nimekataa kutoka naye kimapenzi. Alinitishia kuniua kwa sababu nimekataa kufanya naye mapenzi. Tayari tumeripoti ingawa, anaendelea kutuma vitisho na alishaapa kuwa, msichana wa kazi yoyote yule lazima alale nae uwe kwa hiari au kwa lazima. Mama tunaomba msaada".....

LENGO LA KUKUSHIRIKISHA MWANAJAMII; ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila, yanafichwa kwa uoga au kumlinda mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA [FAECH].

WITO; wasaidizi wa kazi waheshimiwe na tukipata taarifa mtoto wa boss atajua hajui. Wengine vunjeni ukimya tafadhali.

KINACHOENDELEA; ufuatiliaji wa karibu unaendelea kwenye hatma ya tukio hili.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tunafikika na watu wote hadi vijijini hata wenye simu za vitochi hivyo, tuongeze ushirikiano ukatili utaisha siku moja.
✍️🇹🇿

Ikumbukwe, wasaidizi wa kazi wanaweza kuwa wa kike au kiume.

Naye @peace_maker_pm kasema kumbe, hata baadhi ya maboss wako kama watoto wao..... 🤔🤔🤔PIA TOENI TAARIFA HARAKA.

Wengine nao wanasema, kuna wasaidizi wa kazi wananyanyasa watoto wa maboss... ko, nao tupate taarifa pia.

Nawatakia ushirikiano mwema✍️

Dah! Mungu akutunze ili tuendelee kukutumia.
 
Ukatili uko aina nyingi tu na elimu tunatoa na tunakumbusha kwa kurudia rudia. Kwani kwenye ibada wakikemea dhambi mbalimbali huwa ndiyo wameanza siku hiyo au ni mwendelezo ba marudio? Hoja yako sijaelewa tafadhali
Asante mh!
Kwa ujio wako na uvumilivu ulionao.
Nilimaanisha kwamba,ukiachilia mbali ukatili mwingine ambao pia haukubaliki,mimi nilimaanisha huu ambao umeuzungumzia kwenye hoja yako hii.

Nilivyokusoma km sikuelewa vizuri nimeona ni kama leo ndio umebaini uwepo wa ukatili wa namna hii.
Sasa ndio nikawa ninauliza,je ni kweli kwamba leo ndio umegundua ama ulikuwa unaujua ila ulikuwa ukifanya utafiti tu ili ujiridhishe na sasa umebaini kuwa ni kweli?

Nimezungumzia pia kuhusu ukatili waufanyao baadhi ya akina mama kwa hawa wasaidizi wao na kwamba hawa akina mama waelimishwe ijapo ni kweli kwamba elimu hutolewa kila mara.

Nikiwa kijana wa miaka 25 niliwahi chaniwa flana yangu niliyokuwa nikiivaa mara chache sana na dada mmoja ambaye alikuwa ni jirani yetu.
Sababu ikiwa ni mimi kumkingia kifua binti yake mdogo kama miaka minne au 3.5 ili asimpige.

Kosa alilokua ametenda halikuwa lake,lilikua ni la mama yake huyo ila tu kwa upuuzi wake akataka kumuadhibu mtoto nikagoma ijapo ili nigharibu kwa kupigwa makofi kadhaa na kuchaniwa nguo.

Basi kwa heshima ya kwamba ni mke wa mtu,na kuogopa kubambikiwa kumtongoza kwa vile wengi hili ndilo chaka lao na sheria zetu zinawalinda sana hawa viumbe basi nikawa mpole.

Lkn kwa ukatili anafanyiwa mtoto wa kike kwa asilimia kubwa nyuma ya huo ukatili kuna mwanamke,wanyooshewe vidole.

Ref binti wa Yombo na yule afande wa Dodoma na akina Nyundo.
 
Tafadhali sana tumia plural yako vema

Sawa Mh nimekuelewa ila katika kampeni za kufichua wanyanyasaji tusisahau kutupia jicho kwa baadhi ya viongozi wa chama na serikali ,wateuliwa ,wafanyabiashara na watu wanaofanana na hao kwa maana wanatumia pesa zao kurubuni visichana vya 2000 etc kesi ya Mkuu wa mkoa mmoja huko kanda ya ziwa ya kumuingilia kinyume na maumbele msichana mdogo.
 
Shida kubwa ni wakina mama.
Narudia tena shida kubwa ni wakina mama wenyewe.
Binti hana pakusemea kwa sababu, mama mwenye nyumba (mlezi wake) ndio utakuta anafuga huo ukatili. Binti atalazimishwa kimapenzi na mwanaume yoyote wa ndani ya nyumba (mume, mtoto, wajumba, wageni nk) lakini akiripoti tu kwa mama, moto utamuakia.

Ukatili kwa mabinti wa kazi kwenye jamii zetu utaendelezwa daima mpaka siku wanawake wenyewe watakapoamua uishe.
Kweli niliwahi shuhudia hg akifukuzwa na mama mwenye nyumba baada ya kulalamikiwa kwamba "baba ananishikashika"!.
 
-Ifanyike namna ikitokea hiyo shida mfanyakaz areport
-Kwenye Makanisa na Misikiti ikemee hilo swala na kuwapa watu elimu
Ujumbe unawafikia kiurahisi
-Sheria kali ziwepo
 
Mengi yanafanyika humo na mtu anawekewa vitisho kama atasema siri
Mh kati ya wanaoongoza kwa Ushenzi na Ufilauni ni nyinyi viongozi wa chama na serikali ,wateuliwa,wafanyabiashara wakubwa,mkiwa kwenye V8 mnawalamba sana watoto wa 2000.
 
Pamoja na mapungufu ya wanaume,wadada wa kazi baadhi Yao wanajitengenezea wao wenyewe mazingira mabaya,Binti unaamka kufanya kazi zako umejifunga kitenge au kanga Moja unadeki ,unafua,unapika halafu unategemea Nini hapo na wanaume marijali wapo,anaangalia tv anajua kabisa nyumba Ina wanaume amekaa na kinguo Cha ajabu utafikiri kakaa na mtoto mchanga,mkitoka kidogo ukarudi gafla kama huna kifua unaweza kudondoka.Binti zetu pia waelimishwe waache uzungu mwingi tusihukumu tu upande Mmoja.
 
Hakika hii vita ni kali sana

Ukienda kwenye angle chanya

Nawakubali sana wazazi ambao huishi na mdada wa kazi kama ni moja ya familia yake

Wapo wengine huwapatia mpaka fursa kama ufundi kushona pasi na na gharama yoyote.
 
Pamoja na mapungufu ya wanaume,wadada wa kazi baadhi Yao wanajitengenezea wao wenyewe mazingira mabaya,Binti unaamka kufanya kazi zako umejifunga kitenge au kanga Moja unadeki ,unafua,unapika halafu unategemea Nini hapo na wanaume marijali wapo,anaangalia tv anajua kabisa nyumba Ina wanaume amekaa na kinguo Cha ajabu utafikiri kakaa na mtoto mchanga,mkitoka kidogo ukarudi gafla kama huna kifua unaweza kudondoka.Binti zetu pia waelimishwe waache uzungu mwingi tusihukumu tu upande Mmoja.
Alipokuja mlimpa semina? Maana ukitangaza mwaliko wa kazi si na miongozo unatoa? Au mnaishi ishi tu
 
Alipokuja mlimpa semina? Maana ukitangaza mwaliko wa kazi si na miongozo unatoa? Au mnaishi ishi tu
Seminar wanapewa,ila walio baadhi ni wakaidi ukiwepo atajifanya anazifuata kwa muda ukisafiri ukirudi kwa kushitukiza ndio utajua ni mtu wa aina gani unaishi naye,sio wote ila baadhi usipokuwa makini ni vishawishi kwa vijana wetu
 
Wasaalam wote.

Huenda visa viko vingi ila, vinafichwa na kimoja kati ya hivyo ni kama hiki ambacho, kimefikishwa kwangu kwa ufupi:

...."Nimefanyiwa ukatili na mtoto wa boss kwa kupigwa sana kisa nimekataa kutoka naye kimapenzi. Alinitishia kuniua kwa sababu nimekataa kufanya naye mapenzi. Tayari tumeripoti ingawa, anaendelea kutuma vitisho na alishaapa kuwa, msichana wa kazi yoyote yule lazima alale nae uwe kwa hiari au kwa lazima. Mama tunaomba msaada".....

LENGO LA KUKUSHIRIKISHA MWANAJAMII; ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila, yanafichwa kwa uoga au kumlinda mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA [FAECH].

WITO; wasaidizi wa kazi waheshimiwe na tukipata taarifa mtoto wa boss atajua hajui. Wengine vunjeni ukimya tafadhali.

KINACHOENDELEA; ufuatiliaji wa karibu unaendelea kwenye hatma ya tukio hili.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tunafikika na watu wote hadi vijijini hata wenye simu za vitochi hivyo, tuongeze ushirikiano ukatili utaisha siku moja.
✍️🇹🇿

Ikumbukwe, wasaidizi wa kazi wanaweza kuwa wa kike au kiume.

Naye @peace_maker_pm kasema kumbe, hata baadhi ya maboss wako kama watoto wao..... 🤔🤔🤔PIA TOENI TAARIFA HARAKA.

Wengine nao wanasema, kuna wasaidizi wa kazi wananyanyasa watoto wa maboss... ko, nao tupate taarifa pia.

Nawatakia ushirikiano mwema✍️

Madam Mungu akutunze huko ulipo.
Najua una wasaidizi wa kazi!
Kuna msemo unasema hakuna msaidizi wa kazi wa kike mgumba...Je, ni kweli au wanatushawishi kujaribu? Nimeutafakari huu msemo kiasi kwamba naona kama unachochea kama sio kuchangia kabisa katika suala la ukatili wa kingono kwa wasaidizi wa kike?

Lakin jambo lingine, je wafanyakazi hawa wanapata elimu ya kutosha ili kutoa taarifa juu ya masuala ya ukatili wanayofanyiwa ilhali wanafungiwa ndani na hawapewi nafasi ya kutoka nje au kutishwa wakitoa taarifa kwa wazazi au mama wa familia kutegemea aliefanya kitendo hiko?
Jambo lingine, haki za hawa wasaidizi wa kazi zinalindwaje wanapopitia changamoto hizi ilhali jamii kwa ujumla bado inaelimu duni kuhusu ukatili wa kingono?
Nawasilisha.
 
Seminar wanapewa,ila walio baadhi ni wakaidi ukiwepo atajifanya anazifuata kwa muda ukisafiri ukirudi kwa kushitukiza ndio utajua ni mtu wa aina gani unaishi naye,sio wote ila baadhi usipokuwa makini ni vishawishi kwa vijana wetu
Mrejeshe kwako fasta
 
Madam Mungu akutunze huko ulipo.
Najua una wasaidizi wa kazi!
Kuna msemo unasema hakuna msaidizi wa kazi wa kike mgumba...Je, ni kweli au wanatushawishi kujaribu? Nimeutafakari huu msemo kiasi kwamba naona kama unachochea kama sio kuchangia kabisa katika suala la ukatili wa kingono kwa wasaidizi wa kike?

Lakin jambo lingine, je wafanyakazi hawa wanapata elimu ya kutosha ili kutoa taarifa juu ya masuala ya ukatili wanayofanyiwa ilhali wanafungiwa ndani na hawapewi nafasi ya kutoka nje au kutishwa wakitoa taarifa kwa wazazi au mama wa familia kutegemea aliefanya kitendo hiko?
Jambo lingine, haki za hawa wasaidizi wa kazi zinalindwaje wanapopitia changamoto hizi ilhali jamii kwa ujumla bado inaelimu duni kuhusu ukatili wa kingono?
Nawasilisha.
Maswali yako mazuri sana. Ila ndiyo tunaelimisha kwa njia mbalimbali hata shule za Msingi na Sekondari kuna mabaraza ya watoto na semina mbalimbali...... redioni nk na nyie online elimisheni mkienda majumbani kwenu na kwenye majukwaa yenu mengine na kwenye jumuiya, ibada nk
 
Back
Top Bottom