Wasaalam wote.
Huenda visa viko vingi ila, vinafichwa na kimoja kati ya hivyo ni kama hiki ambacho, kimefikishwa kwangu kwa ufupi:
...."Nimefanyiwa ukatili na mtoto wa boss kwa kupigwa sana kisa nimekataa kutoka naye kimapenzi. Alinitishia kuniua kwa sababu nimekataa kufanya naye mapenzi. Tayari tumeripoti ingawa, anaendelea kutuma vitisho na alishaapa kuwa, msichana wa kazi yoyote yule lazima alale nae uwe kwa hiari au kwa lazima. Mama tunaomba msaada".....
LENGO LA KUKUSHIRIKISHA MWANAJAMII; ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila, yanafichwa kwa uoga au kumlinda mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA [FAECH].
WITO; wasaidizi wa kazi waheshimiwe na tukipata taarifa mtoto wa boss atajua hajui. Wengine vunjeni ukimya tafadhali.
KINACHOENDELEA; ufuatiliaji wa karibu unaendelea kwenye hatma ya tukio hili.
Ahsanteni kwa ushirikiano, tunafikika na watu wote hadi vijijini hata wenye simu za vitochi hivyo, tuongeze ushirikiano ukatili utaisha siku moja.
✍️🇹🇿
Ikumbukwe, wasaidizi wa kazi wanaweza kuwa wa kike au kiume.
Naye @peace_maker_pm kasema kumbe, hata baadhi ya maboss wako kama watoto wao..... 🤔🤔🤔PIA TOENI TAARIFA HARAKA.
Wengine nao wanasema, kuna wasaidizi wa kazi wananyanyasa watoto wa maboss... ko, nao tupate taarifa pia.
Nawatakia ushirikiano mwema✍️