Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Baadhi ya watoto wa maboss huwanyanyasa kingono wasaidizi wa kazi za nyumbani

Halafu pia kuna watu wanapenda kusubiria kupanda vyombo vya usafiri vilivyojaa yaani watu wamesimama ili wawakumbatie wengine na hili mliangalie mana dunga dunga wanazidi kuongezeka kwa kasi hao wanaojiita kataa ndoa.
 
Tusiwe na ushabiki kwenye hili...je tumejiuliza root cause ni nini? Mzizi wa tatizo ni nini?
Mtoto anyefanya hivyo amelelewa ama analelewa katika.malezi ya namna Gani? Mahusiano kati ya baba na mama yapo vipi? Vipi kuhusu mahusiano Kati ya wazazi na watoto ama baba na mtoto, ama mama na mtoto ..muwe mnatafuta root causes na sio ushabiki kua "watoto wa mabosi" hata watoto wa mafukara wanaweza kumtaka mfanyakazi as long as anasimamisha na adabu mbovu kutoka kwa wazazi wenye malezi mabovu na wao wakifanya hizo tabia kwa wengine....aaah nimechoka kuandika ....moral decay is an issue, poor or bad parenting is the issue, awe mtoto wa bosi ama fukara wote kama Wana root cause mbovu wote Wana weza kufanya huo uozo..
 
Wasaalam wote.

Huenda visa viko vingi ila, vinafichwa na kimoja kati ya hivyo ni kama hiki ambacho, kimefikishwa kwangu kwa ufupi:

...."Nimefanyiwa ukatili na mtoto wa boss kwa kupigwa sana kisa nimekataa kutoka naye kimapenzi. Alinitishia kuniua kwa sababu nimekataa kufanya naye mapenzi. Tayari tumeripoti ingawa, anaendelea kutuma vitisho na alishaapa kuwa, msichana wa kazi yoyote yule lazima alale nae uwe kwa hiari au kwa lazima. Mama tunaomba msaada".....

LENGO LA KUKUSHIRIKISHA MWANAJAMII; ni ufahamu kuwa haya nayo yapo na huenda huko kwako pia yapo ila, yanafichwa kwa uoga au kumlinda mtoto wa boss. Hivyo, chunguza chukua hatua a.k.a FAHAMU, ELIMIKA, CHUKUA HATUA [FAECH].

WITO; wasaidizi wa kazi waheshimiwe na tukipata taarifa mtoto wa boss atajua hajui. Wengine vunjeni ukimya tafadhali.

KINACHOENDELEA; ufuatiliaji wa karibu unaendelea kwenye hatma ya tukio hili.

Ahsanteni kwa ushirikiano, tunafikika na watu wote hadi vijijini hata wenye simu za vitochi hivyo, tuongeze ushirikiano ukatili utaisha siku moja.
✍️🇹🇿

Ikumbukwe, wasaidizi wa kazi wanaweza kuwa wa kike au kiume.

Naye @peace_maker_pm kasema kumbe, hata baadhi ya maboss wako kama watoto wao..... 🤔🤔🤔PIA TOENI TAARIFA HARAKA.

Wengine nao wanasema, kuna wasaidizi wa kazi wananyanyasa watoto wa maboss... ko, nao tupate taarifa pia.

Nawatakia ushirikiano mwema✍️

Ni kweli, na hali hii inaakisi tabia ya baadhi ya viongozi wetu wa ngazi za juu, ambao hujiona kana kwamba wana haki ya kipekee juu ya uhai na uhuru wa wananchi wa kawaida kwa sababu tu ya madaraka waliyonayo na mali walizozipata kupitia jasho la watu wa hali ya chini. Ukweli ni kwamba mwenendo huu huanzia ngazi ya familia.
 
Mheshimiwa, hao watoto wa kazi hawanyanyaswi na vijana wa mabosi tu, bali hata hao baba wenye nyumba huwa wanawalazimisha kufanya nao ngono.

Iliwahi kutokea, mdada wa kazi aliwaambukiza baba na kijana wake maradhi.
 
Yulle Joyce kiria hana nia ya kuwasaidia wafanyakazi za ndani ndio maana serikali inabidi iwe inazikagua hizi NGO.

Kwenye Kodi naamanisha ni Paye
Imagine binti wa kazi unakaa naye unamhudumia kama mtoto tu wa nyumbani kwa kila kitu tofauti ni mshahara kama shukrani maana kuna familia zingine watu wakiwepo nyumbani wanamsaidia kila jambo. Karibia mtasema apate benefits, zote kama anavokuwa government au NGO ama company
 
Mheshimiwa, hao watoto wa kazi hawanyanyaswi na vijana wa mabosi tu, bali hata hao baba wenye nyumba huwa wanawalazimisha kufanya nao ngono.

Iliwahi kutokea, mdada wa kazi aliwaambukiza baba na kijana wake maradhi.
Wakomeee😀😀
 
Ukatili wa aina hiyo unapaswa kuchukuliwa hatua za haraka, kongole kwa wizara kwa kujitahidi kufuatilia na kuchukua hatua stahiki inapobidi
 
Nashukuru sana Mama yangu Mhe. Gwajima D.

Lakini unafikiri, hisia za mapenzi zinaweza kutibiwa kwa USHAURI NASAHA?

Leo tuzungumze kama mama na mwana!

Kweli labda inawezekana mtu akaacha kufanya mapenzi ya jinsia moja kutokana na kushauriwa au kukaripiwa au kutishwa, lakini unafikiri hizo hisia za ushoga zinaweza kutoweka na kuisha kabisa kwa kushauriwa tu?

Unaweza ukamshauri simba aache kula nyama?

Unaweza ukamshauri ng'ombe ale mifupa?
Hakuna hisia isiyokufa kama umeshalichukia jambo ndiyo maana wapo wengi walitoka huko. Ni akili tu ikijitambua.
 
Nyumba zenye Watoto wa kiume(baru baru) zisitafute House Girls.Na umesahau na Wajomba na Baba Wadogo.
 
Hongera kwa kazi nzuri.
Ili ni tatizo kubwa sana kwa hawa wasaidizi wa kazi za nyumbani,ila naomba nikuulize kaswali kidogo Mh. Sitangoja uniruhusu na swali lenyewe ni hili;
Leo ndio umeambiwa na ndio umegundua uwepo wa ukatili wa namna hii au ulikuwa una tafiti ili upate kujiridhisha juu ya uwepo wake?

Zaidi nakuomba uwakazanie akina mama,hao ndio maadui nguli wa wasaidizi wao,muda woote nikuwafokea tu kwa kuhisi kuwa huenda wakapinduliwa,sasa waume zao,vijana wao nao wanatumia huo mwanya kuwanyanyasa hawa mabinti kwani wanakosa mtetezi ndani ya nyumba.
Ukatili uko aina nyingi tu na elimu tunatoa na tunakumbusha kwa kurudia rudia. Kwani kwenye ibada wakikemea dhambi mbalimbali huwa ndiyo wameanza siku hiyo au ni mwendelezo ba marudio? Hoja yako sijaelewa tafadhali
 
Hilo lipo sana, tatizo lipo unapotoa taarifa sehemu husika, hakuna hatua yeyote inayochukuliwa, ndo mana watu wanaona kma ni kujisumpua tu.

Mh. Jimbo gani unagombea?, nje ya mada
Hiyo taarifa ambayo ilitolewa hatua hazikuchukuliwa niletee kwa sms kuja 0765345777 ili tuchukue hatua kisha tumchukulie hatua ambaye hakuchukua hatua.
 
Asante
Kundi lingine linalonyanyasika ni wanafunzi wanapokwenda shule asubuhi na wakati wa kurudi,
swala la usafiri upande wao ni changamoto haswaa
 
Kwa mara ya kwanza Madam kaanzisha madam ngumu na tete. Hili jambo hata kwake lipo, labda kama hana watoto wanao barehe au walio barehe. This includes baba yeyoo. Hivi vitu hufanyika 24/7, hasa wewe madam ambaye unafanya kazi kuliko kazi yenyewe. Mara Bunge marathon sitting huko Dodoma mara uko kwenye msafara wa Rais mkoani au nje ya nchi (Kama una bahati hiyo to be included). Piga picha ya teenagers wetu na housegirls na houseboys. Yapo yapo na yapo saana. Wazazi ni ngumu kujua, tusi danganywe na A za mitihani watoto wetu si Malaika.
Kazi ya elimu kwa umma wote ni muhimu, na kazi ya wasomaji wote na wasikilizaji wote ni kuelimika na kuchukua hatua wakiwemo hao unaowasema, maana naona mwenzetu wewe ni xray ya familia za watu. Sasa endelea kupiga xray na mimi niendelee na kazi yangu ya elimu kwa umma, na ukipiga xray yako ukabaini wagonjwa wa familia mbalimbali utawaleta tuwatibu. Sawa? Kila mmoja afanye kazi inayomhusu ili twende kasi zaidi. Hatuna muda
 
Mama afadhali ulivyoongea..
Nakumbuka baada ya kumaliza form four nilikua sina la kufanya na sikuweza kusoma pree form five kwa sababu hata matokeo yalikua bado...

Sasa hapa nikapata kazi kwa nyumba ya mwalimu fulani hv ambaye huyu mwalimu alikua na watoto wake wakike ambao walikua chuo....

Sasa hao wadada walikua wana mambo ya ajabu sana aitosema ila kwa kipindi kile nilikua sijui haki yangu..

Wale niliwachukulia kama dada zangu ila wao hawakujali hilo
 
Imagine binti wa kazi unakaa naye unamhudumia kama mtoto tu wa nyumbani kwa kila kitu tofauti ni mshahara kama shukrani maana kuna familia zingine watu wakiwepo nyumbani wanamsaidia kila jambo. Karibia mtasema apate benefits, zote kama anavokuwa government au NGO ama company
Tatizo mnatoa ajila Kwa watoto, Tukiacha kuwaona kama wasaidizi na wao wanahitaji kukuwa sio tu kubaki kuwa msaidizi ndio maana nchi zilizoendelea zimefanya kazi hizo kuwa rasmi
 
Mh. Waziri angalia na hawa ambao ni wateja wa baa wakiona wahudumu wa kike wa baa wao ni kuwashikashika bila lidhaa zao kwa nadharia kuwa kutokana na kazi zao pia watakuwa wanajiuza.
Ahsante sana, mambo ni meeengi, huenda kwa wakati wangu yasiishe yote, tutaweza tuliyoweza na mengine tutatoa elimu na watu wajue kuwa, kila usilolipenda chukua hatua tunazotangaza upate msaada wa kisheria na mengine husika.

Yako tuliyoweza kuyasukuma na takwimu tumetoa na mengine ni endelevu na yanahitaji ushirikiano endelevu wa jamii. Ahsante sana
 
Asante mheshimiwa. Yani serikali ndio itoe muongozo kwa waajiri wanaotaka kuajiri msaidizi wa ndani, ili hata siku ikitokea shida basi. huyo mfanyakazi awe anasheria za serikali zinazomlinda kuhusu mshahara na malimbikizo, na wawe na chama cha wafanyakazi wa ndani kiwepo wizara yako ili kisimamie haki zao na iwe rahisi kufikisha kero zao serikalini direct kupitia wizara yako.
Hili la miongozo liko wizara ya ajira na kazi. Mimi natoa elimu tu kama changamoto za kijamii ninazopokea na zinazogusa kundi kubwa la wanawake na watoto wakiingizwa humo. Kuna taarifa ya mwongozo wa wizara ya ajira na kazi kuhusu mikataba eneo hili, nitaileta. Ahsante kwa maoni
 
Back
Top Bottom