Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Akili ya haraka mkuu ni kuwa hao watoto walikuwa wanazingua,na ukute sumtime walikuwa wanaomba Mzee adedi warithi mali,naona Mzee kaona achukuwe maamuzi kabla hajafa.
Inaitwa timing game nafikiria wazazi wengi wangefanya hivi wangekuwa wanapatia Sana .
 
Kuwndesha ni ngumu, failure ina comprise of many factorsoja wapo ni maandalizi.
Kama kizaz kilichopita hikuandaa kikamilifu na ku teansfer uzoefu lazima itafeli tu, si suala la bahati
Ukisoma Corporate raiding iliyofanyika miaka ya 70 mpaka 90 ni kwamba watu walijua kabisa ukipunguza wafanyakazi shares zinapanda na kampuni nyingi ambazo ni family owned zilikuwa zina assets za kutosha hivyo wadau walikuwa wanaangalia kampuni zenye assets nyingi; wanatumia mikopo / funds (Hususan za Pension Funds) wananuna Shares za wanaozunguka familia wanakuwa na Majority Shares wanaamua kuuza kufukuza wafanyakazi (down sizing) wanauza shares na kuacha kampuni inajifia wao wanaondoka kwenda kutafuta kampuni nyingine (most family owned companies in USA na UK zilikumbwa na hii dhahama ) kumbuka hapo kale kampuni karibia zote zilikuwa family owned au made from scratch by founders...; Sasa hivi ni Stock Market inasemaje with a lot of Cooking the Books....
Yes once company ikishaenda publick ni ngumu but moja ya trick kubwa wanafanya ni kushikilia majority ya shares, na mwenye share kubwa ndie anakuwa na sauti
So tunarudi pale pale
utashikilia majority ya shares kama umepata shida na unahitaji mtaji zaidi hivyo kuuza hizo shares ? na wote waliokuzunguka hata kama wana 51 % na wewe 49% unadhani watu wakiamua kuwahonga hao ili wakutupe kando inashindikana ? Muulize Musk yaliyomkuta ya kuwa Fired kwenye Kampuni aliyoshiriki katika uanzishaji wake..
 
Mzee anajiandalia pepo yake, watoto wakatafute za kwao. Mzee wangu alinipa fundisho kubwa, nakumbuka siku naondoka nyumbani nilikuwa na suruali moja , mashati mawili,kobaz na bukta (mchana ndio Pichu, usiku bukta ya kulalia)
Mali za mzazi ni za kwake akiamua kukupatia alhamdulillah, akikutosa basi nenda kapambane na dunia.
 
Hilo eneo anauza anaenda jenga pembeni na anajenga msikiti hiko pembeni na anabakiwa na pesa za mtaji na maisha yanaendelea. Ogopa sana Mtu akigia dini hawabadiliki.
 
Mzee yupo sahihi Ila angekuwa Ana one kana hayupo sahihi Kama Ange-dumb familia yake .

Ila ikiwa amewalea watoto mpaka utu uzima basi yupo sahihi kugawa Mali zake popote anapotaka.
Safi Sana kaka tuwawezeshe watoto wetu kwenye ELIMU na kujitegemea na tusiwalee kutegenea urithi unakuta familia nyingi Sana za mikoa ya pwani unakuta kijana anasubir mzee afariki waanze kuuza na kugawana mali za mzee wao kwa FUJO NA KUFUJA MALI ZA MZEE WAO.
 
Slaver mind hiyo --- Ogopa sana kichaa Cha dini kikikupanda dini imefilisi watu wengi na kuwanufaisha wajanja


Na wajanja wamefanikiwa zaidi katika Hilo Kwa sababu Huwa Wana wabrain wash waumini wao kwamba Ukiwa mtoaji sadaka basi ukifika waenda peponi na unapata thwawabu Kwa mungu
 
Mzee miyeyusho hana akili wanaoto wakfu ni wasio na watoto ,ye alipaswa aiuze billion za kutosha awajengee wanawe nyumba then ingine ajenge msikiti naiko kituo uyo mzee ni mbinafsi
Mzee kapiga kwenye mshono 😅😅🤣 vilio kila konaa mzee yupo sahihi kwenye hii scenerio.

Kama matoto yako yame kengeuka malevi na mavuta bange na Malaya ulitegemea mzee kutoa mali kwa watoto wa aina hiyo.

Mimi binafsi mpaka Sasa licha ya mzee kuwa na mali ZAKE nashukuru kaniwezesha na sitolei macho chochote mzee akitaka kufanya lolote yeye afanye TU
 
Akili ya haraka mkuu ni kuwa hao watoto walikuwa wanazingua,na ukute sumtime walikuwa wanaomba Mzee adedi warithi mali,naona Mzee kaona achukuwe maamuzi kabla hajafa.
Hakika unakuta watoto hawaishi vyema na MZAZI WAO.

WAZEE WA UMRI WAKE NI WENYE UPENDO SANA ILA ITAKUA WATOTO WAMEZINGUA MZEE AKA AMUA MALI ZAKE AZITOE KWA UMMA
 
Yupo sahihi hizo ni mali zake anafanya anachotaka hao watoto nao watafute vyakwao wasitegemee mambo ya kurithi .
 
Huku niliko jamaa alitoa frem Tatu za sokoni kabisaa kuwa za msikiti,wamemsubiri afe kilichotokea sidhani kama Kuna mtu wa msikitini anayeweza kusogea pale.Watoto wameshaiva hawataki kusikia chochote.
 
Shida hapo mambo yameingiliana wewe na wenzako mnajali maisha, Mzee amemaliza maisha anaangalia anakoelekea ambako ni akhera, na wengi hatuna mambo hayo kifupi Mali ni yake na anaitumia anavyoona, na inafaa, japo lengo lake lingetimia chini awape mkataba matajiri, ghorofa ya pili unakuwa msikiti na juu nyumba za kuishi, lkn inaonekana pia hakuna maelewano mazur kata ya baba na mtoto na huenda watoto mpaka bado hawajielewi, jingine unaskia miskiti mingi ikiitwa jina la mtu huo ni Waqfu Wala si Jambo geni, watoto katafteni Mali zenu
 
Ipo hivi mkuu

Kwa kuwa mzee Babu hakuacha wosia na pia watoto wake hawakuwahi kufungua mirathi na wote wamekufa ilhali mirathi ya Mzee Babu haijafunguliwa, basi mtu yeyote (hasa wajukuu) anaweza kufungua mirathi ya Mzee Babu na akiteuliwa kusimamia basi yeye ndiye atakayeamua kugawa nini na kwa nani.

Sheria haielezi kuwa ni lazima msimamizi apate maoni ya warithi ila anashauriwa kusikia maoni ya warithi kuwa wanataka mgawanyo uwaje, wakikubaliana basi atafuata maoni yao, ila akiona wanabishana - ataamua anavyoona inafaa yeye.

Mahakama ya Rufani hapa majuzi tu kwenye kesi ya Peter Augustino Mrema vs Doris Agness Augustine Mkandala (Civil Appeal No. 102 of 2024) [2025] TZCA 362 (16 April 2025) iliamua kuwa Msimamizi wa Mirathi ndiye muamuzi wa mwisho wa agawe nini na kwa nani, yaani anaweza kumkataa hata mrithi akiona ana mashaka nae.

Kujibu swali lako kwa kifupi ni kuwa, Mahakama haigawi mali bali msimamizi. Hata hivyo uzoefu unaonesha inapofika kwa wajukuu, mgawo huangalia vichwa vya watoto na sio idadi ya wajukuu.
 
Yupo sahihi hizo ni mali zake anafanya anachotaka hao watoto nao watafute vyakwao wasitegemee mambo ya kurithi .
Unakuta mzee amedukua kijana wake kapeleka mwanamke hapo kariakoo na kwenye kutongoza kamwambia anangojea mzee afariki then wauze mali wapate pesa ya kula Bata na harusi.

Hata ungekua wewe ndio mzee unagundua mtoto wako anakuombea Dua mbaya Sanaa 😊
 
Jacqueline mengi ataka ml 90 kwa mwezi kuhudumia Jayden na Ryann

Wakishinda wapewe buku,

nanto mbe
 
🤣🤣🤣
 
Asante sana mkuu. Na msimamizi wa mirathi anapatikanaje? Je, wajukuu wasipofikia muafaka na kukubaliana ni nani awe msimamizi itakuwaje? Na yule mjane ana nafasi yoyote kwenye kutoa maamuzi ya msimamizi wa mirathi awe nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…