Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Unajua kuna mambo yapo hidden.

Pale Temeke kuna mzee mmoja alikuwa Anaitwa Mzee Mdowe (RIP)

Alikuwa amepata watoto wakubwa age 30+ ,40+

Hao watoto wake wakubwa walikuwa wamemtupa baba yao nikisema kumtupa walikuwa hawana habari nae .

Ila mzee alikuwa pia na watoto wadogo age 12+ 9+

Sasa hawa watoto wadogo wa uzeeni ndo walisimama na Baba yao mpaka anafariki mwaka 2021.

Mzee alichofanya ile Nyumba potential na ndo hiyo alikuwa nayo pekee aliwapa wale watoto na akasema MTU asisogelee na aliweka hizo document kisheria kabisa sasa wale watoto ndugu zao wakubwa na wajinga walimtupa baba yao wapo wanapambana kutaka kuipata hiyo Nyumba .


So na huyo mzee kuna uwezekano Ana watoto Ila ndo wale watoto wajinga wasiojitambua
Ni kweli kabisa kabisaa ndugu tujifunzee
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Ieleweke kuwa mzee huyu kwa mujibu wa maelezo ana maeneo mengi, na maeneo hayo ameshawapa watoto wake, hilo hapo ameamua kulitoa sadaka, shida iko wapi? Ingekuwa kosa kama watoto wasingeachiwa urithi wao.

Kafanya jambo zuri sana
 
👉Kwa upande wake yupo sahihi

👉Ila Mimi monetary doctor siwezi fanya hivyo kwa wanangu, nitajitahidi niweke mazingira wezeshi kama nilifika 3/10 basi wao ule uwezeshi wafanye 5/10 na kizazi kijacho hivyo hivyo

👉 Kariakoo ni sehemu ya kibiashara kuweka kitega uchumi Cha jengo ni fursa tosha, mapato yatokanayo na jengo Hilo itawawezesha kutafuta eneo jingine potential na kuwekeza ten,


👉waki generate cash flow 20 yrs next wanajikuta wapo mbali

👉 Ndugu zangu katika imani tumepata pa kuswalia Takbir secretarybird
Umenena vyema, sahihi 100%,,
 
je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?

video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua

kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake

Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.

Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo


imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake

View attachment 3379922
Kama mitoto yenyewe haijishughulishi toa sadaka ipambane na Hali zake
 
Back
Top Bottom