je ni sawa baba yenu aliyezeeka kutoa nyumba yake ya pekee kwenye prime area kariakoo kuwa mali ya msikiti huku watoto wake hamna maisha ya kueleweka, mnateseka kutafuta mtaji wa kujikomboa ?
video inaonesha mzee akiitoa nyumba yake yenye ardhi yenye thamani kubwa kariakoo kuwa mali ya msikiti, watoto walipinga ila mzee ndio kashaamua
kwa nini watu weusi wengi hatutambui Generational wealth ? kama kina Donald Trump walivyofaidika nayo kutoka kwenye ardhi za prime areas alizorithi kutoka kwa baba yake na babu zake
Hata tajiri kama Bakhressa na GSM huwezi kukuta wanatoa sadaka ardhi yao ya Kariakoo ama prime area kama masaki na oysterbay.
Ardhi ya kariakooo ni kama mgodi wa dhahabu isiyoisha... hakuna tajiri aliewahi kutoa sadaka ardhi ya kariakoo.. hao kina bakhressa sadaka wanazitoa ardhi za huko chamazi ama kisemvule, ila sio kariakoo
imagine hilo eneo lao kariakoo wangeingia mkataba na tajiri angejenga ghorofa la ma fremu hapo,,, watoto wake wangekula hadi kizazi cha nne kingekula matunda yake
View attachment 3379922