Baba mzazi hataki binti yake aolewe

Baba mzazi hataki binti yake aolewe

Labda mzee nwnazifahamu matatizo ya bint ake au Kama vip apigwe mimb
 
Ndio labda Dada anaeolewa alikuwa mkeo na hujampa taraka au kaka anae funga ndoa ana ndoa nyingine na hajatoa talaka
[/QUOTE

MKUU MIMI SWALI LANGU BADO NI LILE LILE BINTI ANAWEZA KUOZWA PINDI BABA MZAZI AJAKUBALI NA YUPO HAI.
Hawezi mzazi teyali amekuwa kipingamizi kwaiyo labda uyo baba alishakura mahali ya mtu mwingine ndio Sababu labda inamfanya akatae
 
MKUU MIMI BADO NAULIZA BINTI ANAWEZA KUOLEWA BILA KUOZESHWA NA BABA YAKE MZAZI ALIYEMZAA NA YUPO HAI BABA YAKE HUYO?.
Endapo baba Hana pingamizi na kipindi Cha tangazo la ndoa huyo baba hakupeleka pingamizi lakini Kama amepeleka basi ndoa haita fungwa na Kama haja peleka ndoa itafungwa
 
Katika kanisa ninalosali kuna Baba mzazi mmoja Ana binti yake wa kwanza, japo mama wa binti huyo alifaliki baada ya kumzaa binti huyo. Baba akaoa mwanamke mwingine.

Hila huyo binti anamiaka 36 hivi Sasa. Na Ni mwalimu wa chekechekea. Shida Ni kwamba Baba mzazi hataki binti yake aolewe kabisa. Binti akipanda mtu akienda kumwambia Baba yake , Baba anajibu "sitaki kujua kuhusu hayo Mambo na usiniambie Tena hebu toka hapa" kamfanyia hivi Mara kadhaa tuu Hadi binti analia inafika kipindi analia.

Miaka Kama 4 Nyuma alitengeneza mahusiano, na kijana mmoja kanisa huyo kijana Kaka Yale tunasalinae hapa hapa kanisani na Kaka Yale ameoa.

Binti na kijana walipenda sana ikafika mpaka kipindi kanisa Zima wakajua mapaka baba yake, japo Baba yake hakusema chochote, binti alikuwa anaenda mapaka kwenye geto la jamaa kufanya usafi na kumsaidia Baadhi ya kazi nyumbani kwake, na ikafika hatua wakakubaliana wafunge ndoa. Shida ikafika namna ya kwenda kwa mzee wake.

Wakaamua kwenda kwa uongozi wa kanisa kuomba waandae utaratibu wa kwenda kwa Baba yake KUPITIA Mwamvuli wa kanisa. Kanisa likaamua kuchugua wazee wakanisa Kama 3 wanaoeshimika kanisani waende kwa mzee. Kijana akandaa barua ya posa na wazee wakaenda.

Walipo fika nyumbani kwa wakakalibishwa vizuri sana na vinywaji juu. Wakaongea na kueleza kilicho wapeleka, mzee akawajibu kuwa "Nani aliyewahambia kuwa Mimi ninaoza binti na sijatangaza binti yangu alitewe posa, sitaki kusikia kuhusu haya Mambo hebu tokeni hapa sitaki kuwaona tokeni tokeni" wazee wabusara wakandoka na kurudisha taarifa.

Binti yule alivyorudi home mzee wake hakusema chochote alinyamaza tuu mapaka leo , na binti mara nyingi akimwambia Baba nimepata mchumba mzee hapana sitaki kusika.

Washiriki wa kanisa walisema Sana juu ya iyo ishu , mpaka shemeji Yale "mke wa Kaka yake" alilalamika Sana na akasema Wenda akawa anamtaka au anatembea na binti yake.

Kijana alipata mchuba mwingine na akafunga ndoa kanisani na ukumbi nje ya kanisa na ilikuwa Ni mzuri Sana watu walikula na walifurahi , yule binti hakuja kwenye ndoa.

Hivi sababu gani inaweza kupelekea Baba mzazi kukataa binti Yale asiolewe shida Ni Nini wakuu.
Karibuni......
Mkuu kama hiki kisa ni cha kweli njoo inbox nikupe uahauri wa kumpa binti.
 
Kwani iyo ndoa ikifungwa cheti kinatolewa na Nan? Jibu hapo nikueleweshe
Ndoa sio cheti, NDOA NI NINI?

1. KISERIKALI
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

2. KIKRISTO (BIBLIA)
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

3. KIISLAM

Ndoa ya Kiislamu (Nikah) ni mkataba (Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu.

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakuna ndoa isipokuwa tu kwa (idhini ya) Walii». (Abuudaud, Hadithi Na. 2085. Tirmidhiy, Hadithi Na. 1102) .

Cheti ni ushahidi tu kwamba ndoa imefungwa ila sio hitaji la msingi la ndoa. Ndoa ni maagano ya watu wawili.
 
MKUU MIMI BADO NAULIZA BINTI ANAWEZA KUOLEWA BILA KUOZESHWA NA BABA YAKE MZAZI ALIYEMZAA NA YUPO HAI BABA YAKE HUYO?.
Ndio inawezekana kabisa kwa upande wa waislam ndoa ili ifungwe basi lazima baba, kaka au ndugu mwanaume mwenye ukaribu na binti aridhie hiyo ndoa, asiporidhia haitafungwa ila pia awe na sababu zenye mashiko bila ya hivyo ndoa inafungwa bila hata idhini yake.
 
Hawezi mzazi teyali amekuwa kipingamizi kwaiyo labda uyo baba alishakura mahali ya mtu mwingine ndio Sababu labda inamfanya akatae
Acha ujinga wewe hujui kitu, inaitwa Mahari sio Mahali. Kwa mujibu wa dini ya kiislam mahari anataja binti anayeolewa na pia atakula yeye sio mzazi. Acha kudanganya
 
Ndoa sio cheti, NDOA NI NINI?

1. KISERIKALI
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

2. KIKRISTO (BIBLIA)
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

3. KIISLAM

Ndoa ya Kiislamu (Nikah) ni mkataba (Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu.

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakuna ndoa isipokuwa tu kwa (idhini ya) Walii». (Abuudaud, Hadithi Na. 2085. Tirmidhiy, Hadithi Na. 1102) .

Cheti ni ushahidi tu kwamba ndoa imefungwa ila sio hitaji la msingi la ndoa. Ndoa ni maagano ya watu wawili.
Unaweza kuthibitisha vip kuwa ndoa imefungwa au ni halali Kama haina cheti?
 
Acha ujinga wewe hujui kitu, inaitwa Mahari sio Mahali. Kwa mujibu wa dini ya kiislam mahari anataja binti anayeolewa na pia atakula yeye sio mzazi. Acha kudanganya
Ww umeongelea kwa upande wa dini yako
 
Sheria ya ndoa imebainisha kuwa vitu vitakavyo fanya ndoa isifungwe ni pamoja na wazazi au mzazi Kama hajalizia ndoa iyo kufungwa kwaio ili ndoa ifungwe ni lazima wazazi warizie kufungwa kwaio ndoa

Sheria ipi Ndugu?

Kama ni sheria za nchi hakuna kitu Kama hicho.

Serikali inapinga Force Marriage kumaanisha Suala la Ndoa ni ishu personal ya watu wawili wenye jinsia tofauti waliokubaliana.
 
Unaweza kuthibitisha vip kuwa ndoa imefungwa au ni halali Kama haina cheti?
Kwa kutumia mashahidi, kwenye kufunga ndoa kunakuwa na mashahidi. Cheti ni muhimu ila sio lazima. Ili ndoa iwe halali inahitaji mambo yafuatayo :-

1. Iwe kati ya mwanaume na mwanamke. (Hapa mashoga na wasagaji imekula kwao)

2. Wawe wameridhia bila kulazimishwa.

3. Awepo walii na (baba, kaka, bamdogo, bamkubwa wa binti n.k) na aridhie kufungwa kwa ndoa.

4. Kuwe na mashahidi wa pande zote mbili.

Cheti kimekuja kwa ajili ya kuweka kumbukumbu kwamba fulani na fulani wamefunga ndoa mbele ya mashahidi fulani na fulani ila sio hitaji la lazima.
 
Back
Top Bottom