Kwani iyo ndoa ikifungwa cheti kinatolewa na Nan? Jibu hapo nikueleweshe
Ndoa sio cheti, NDOA NI NINI?
1. KISERIKALI
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.
2. KIKRISTO (BIBLIA)
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.
3. KIISLAM
Ndoa ya Kiislamu (Nikah) ni mkataba (Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu.
Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakuna ndoa isipokuwa tu kwa (idhini ya) Walii». (Abuudaud, Hadithi Na. 2085. Tirmidhiy, Hadithi Na. 1102) .
Cheti ni ushahidi tu kwamba ndoa imefungwa ila sio hitaji la msingi la ndoa. Ndoa ni maagano ya watu wawili.