Baba wa Joshua aomba serikali ya Tanzania iongee na nchi rafiki za HAMAS ili waachie mwili wa mwanae

Mwili tena ndani ya miezi miwili
na nimesikia bullet proof ya nn tena si wanafunzi jamani!?

Kila nyumba ktk kibbutz ina safe room ikitokea kushambuliwa watu wanaingia na kukupata usalama huko kuna bullet proof vest, chakula cha dharura, maji n.k hadi polisi au IDF ifike kuwaokoa au kutoa tamko tishio limepita salama.

Vyumba hivyo vya safe room pamoja na vifaa vya dharura pia vipo ktk vituo vya mabasi, shopping mall n.k
 
Politics nyingi sana nchi hii, huyo mzee alienda kufanya nini huko?
 
Wanajeshi walikuwa wanafanya nini tena kwenye Camp ya Kilimo?? Daah maswali ni mengi kuliko majibu
Mkuu,mkiwepo kule sio mnakaa camp kama timu ya Mpira .
Ndio maana kwenye Hilo shamba lao kulikua na watanzania kama wanne tu kama sijakosea kati ya 260 walienda kule.

Na makazi ni nyumba za kupanga tu uraiani huko.Kwa hiyo lazima mchanganyike.
 
Maelezo ya bababyake Joshua Molel yamenibubujisha machozi.

Tuendelee kusimamia amani popote pale duniani maana vita ni mlango wa maangamizi dhidi ya ustawi na uwepo wa utu
 
Politics nyingi sana nchi hii, huyo mzee alienda kufanya nini huko?
Mkuu
Serikali ya Israel inayojali ilimualika kumueleza ukweli kuhusu kilichojiri hadi kupelekea umauti wa mwanae.

Wenzetu hawana cheap politics kama za CCM na sisi Watanzania.

Tupunguze upuuzi maana ushabiki wa vita umetufikisha hapa kuanza kugawanyika kama Taifa na tumeanza kupoteza watu wetu
 
Mmmmmmm
 
Wanaopigana Gaza sio Hamas pekee yao kuna Wanamgambo wa PIJ Palestinian Islamic Jihad.
 
Maelezo ya bababyake Joshua Molel yamenibubujisha machozi.

Tuendelee kusimamia amani popote pale duniani maana vita ni mlango wa maangamizi dhidi ya ustawi na uwepo wa utu
Unabubujika machozi ya mtu mmoja? Nenda Israel na Gaza kuna maelfu wameuawa.
 
Daah kwa hiyo Israel wanamshauri mzazi ndio aiombe Serikali yetu nilidhani Israel walitakiwa wao ndio wawe Bega kwa Bega na Serikali ila naona kinachofanyika ni tofauti kabisaa...
 
Wanapiga halafu wanakimbila ardhini qanaenda kutokea upande mwingine.

Kama Vietcong kwenye kwenye vita ya Vietnam na USA.
Kama wewe uliopo Bongo unajua kwamba wanapiga na kukimbilia kwenye tunnels si ingekuwa rahisi kudhibitiwa kwa kulipua hizo tunnels.Wacha kutoa majibu rahisi kwa maswali magumu.
Vietnam vita ilikuwa inapiganwa porini na Marekani alitandikwa haswa licha ya kuua raia kwa fujo.Mwisho akasarenda na kukimbia Vietnam na kuwezesha Vietnam Kaskazini kuungana na Vietnam Kusini na kuwa Nchi moja Vietnam.
 
Anayeweza kumwambia Huyo Balozi kuwa Huwezi ukashinda Dunia nzima, Hakuna Nchi hata moja iko tayari kuwasaidia Hao Wapalestina kwa vitendo zaidi ya Kuwatumia.

Miaka 50 ijayo Judea and Sumeria yote itakuwa na Wayahudi kila sehemu
 
Wakati wa Carpet Bombing ya Misitu ya Vietnam sio kwamba raia hawakufa walikufa Vijiji viliangukiwa na Mabomu

Hamas wao wamechimba network ya Tunnels chini ya makazi ya watu kitu ambacho kinasababisha raia wafe kwa wi.ngi
 
Daah kwa hiyo Israel wanamshauri mzazi ndio aiombe Serikali yetu nilidhani Israel walitakiwa wao ndio wawe Bega kwa Bega na Serikali ila naona kinachofanyika ni tofauti kabisaa...
It means Seriakali yetu imelala kwenye kujali usalama wa Raia wake, Israel walitarajia kuona Serikali ya Tanzania kama taifa mojawapo ambalo Raia wake wameathirika na tukio hilo wakiwa wanafanya Juhudi za Kimataifa.

Putin, Thailand, France and Mataifa yote wamekuwa wakizungumza na Hamas kupitia Channels tofauti tofaut kama Qatar na Egpty kwa ajili kujua Usalama wa Raia wao wanaoshikiliwa Mateka.

Hili linaonesha Kuwa Either tunauongozi dhaifu sana au tuna kikundi cha watu wenye mamlaka wasiojua malengo ya taifa au kuthamini Raia wake
 
Wakati wa Carpet Bombing ya Misitu ya Vietnam sio kwamba raia hawakufa walikufa Vijiji viliangukiwa na Mabomu

Hamas wao wamechimba network ya Tunnels chini ya makazi ya watu kitu ambacho kinasababisha raia wafe kwa wi.ngi
Huo uongo usiokuwa na aibu.Hakuna tunnels zozote zilizokutwa kwenye makazi ya watu.Na hata jaribio la kutengeneza ushahidi kwamba kulikuwa na tunnel chini ya Al Shifa Hospital lilikwisha kwa aibu kubwa kwa kukosa ushahidi.Tunnels maarufu za Hamas ni kwenye mpaka na Egypt ku smuggle silaha,petroleum na chakula kutoka Egypt.
 
Kuna Video chungu nzima zinaonyesha Al Qasam Brigade wakichimba Tunnels na Yahya Sinwar hadi anaendesha Gari ndani ya tunnel unataka kubisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…