Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

Baba wa Manabii na Mitume wote Ibrahimu au Abrahamu alikuwa Dini gani?

hili swali nalikalibisha tu,kwa watu wenye uelewe wa mambo ya Dini.

Huyu ni nabii na mtume wa Mwenyezi Mungu,ambaye anakubaliki na Dini zote,kuanzia Uyahudi,Ukristo mpaka Uisilamu,na hawa wote ibada zao zimetofautiana.

Je niwapi wanaomfata?
Badala ya kukomaa na historia ya mababu zenu mnakomaa na historia ya mababu wa huko mbali ambapo hata hawawapendi, yaani nasikitika sana kutokujua jina la Babu wa Babu yangu back to almost year 1800 wakati likija suala la Israel n the neighbors mtu unamsoma aliyeishi miaka 2000 iliyopita, naumia sana basi tu
 
Hatukuja hapa kutukanana, rekebisha lugha yako.

Hii ni mijadala yenye faida kwa wengi, huna sababu ya kuwa na lugha za kuudhi.
Mungu akupe uvumilivu na ustarabu na kesho Akhera uwepo daraja la juu kwa ustarabu wa jibu lako, Waisilamu siku zote ni wavumilivu na wastarabu sababu wana hofu ya muumba wao
 
Kuna kitu huwa tunashindwa kuelewa kuhusu dini, maranyingi Wakristo wamekuwa wakiwakebehi Waislam wasemapo kwamba manabii ama mitume fulani waliokuwepo miaka mingi nyuma kabla ya Uislam ni Waislam. Hamtakiwi kukebehi kuhusu hili maana ndio imani yao na vitabu vyao vimeandika hivi.

Kinachofurahisha Wakristo wao hujiona wako sahihi kusema Manabii hao wlikuwa upande wao wakati Ukristo umekuja baadae sana.

Iko hivi: Wayahudi wanaamini maandiko yao matakatifu (Torah). Wakristo wameandika katika biblia yao takatifu kuhusu Moses na maandiko yake lakini hii haiwezi kuwashawishi Wayahudi waamini kwamba Ukristo ulikuwepo tangu kipindi cha Musa. Vivyo hivyo kwa Waislam, Quran imeandika kuhusu Musa na hata Yesu lakini hiyo haitawafanya Wakristo waamini kwamba Uislam ulikuwepo kabla ya Yesu.

Mkijua hili wala hakuna haja ya kumsema mwenzako wakati hata wewe umefata mfumo huo huo. Wakristo wanaamini Wayahudi walimkataa Yesu na walijutia kwa hilo baada ya kumuua lakini ukweli hadi leo hii Wayahudi hawamuamini Yesu kama messiah. Waislam wanaamini Muhammad ni muendelezo wa mpango wa Mungu kuwaleta wasaidizi wake kueleza utukufu wake lakini Wakristo hawaamini katika hilo.

Anayewaita wenzake wafia dini yeye keshaoza katika dini yake[emoji23]
Umemaliza mkuuu

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK
 
Nyakati za Ibrahimu hakukuwa na dini tulizo nazo sasa...

Watu walikuwa na imani juu ya ama Yehovah au miungu...
 
Endelea kujifurahisha.
Hiyo aya kwanini imesema ibrahimu hakuwa myahudi wala mkristo bali muislamu,? iluandikwa na nani? Kipindi gani?

Maana hiyo aya imeelezea kuhusu ukristo, na ukristo ulikuja karne baada ya Yesu wala haukuwepo wakati wa Ibrahimu, sasa wapi ibrahimu mwenyewe aliutaja kuwa yeye alikua Muislam?

Nb: hakua pia mkristo
 
WEWE NDIO YALE MAJITU MWALIM ANAFUNDISHA DARASANI POINT MUHIMU HAYAZINGATII...

NIMEKWAMBIA...DINI NI ITIKADI...ITIKADI YA DINI YA KIKRISTO NI NINI? JE ITIKADI HIYO ALIKUWA NAYO IBRAAHIIM...? KAMA ALIKUWA NA ITIKADI KAMA WAKRISTO HIVI LEO...BASI IBRAAHIIM ALIKUWA MKRISTO...
Dini ni itikadi kwa mtazamo wako wewe/nyie, wengine wanamitazamo tofauti kuhusu dini kuanzia wahindu , wabudha nk, siyo ohms law kusema always V=iR
 
Historia ya biblia inarudi nyuma maximum 6000yrs, yaani kwenye uumbaji.

Lakini kulikuwa na jamii nyingine zinaishi, older than 6000yrs, na maandiko mengine ya zamani zaidi kuliko ya Wayahudi kutoka kwenye jamii za Mashariki (mostly India).

At the moment naelewa zaidi mafundisho/understanding yao, their description of God and life kuliku hizi Abrahamic religions.
 
3_67.gif

Qur'an 3:67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina. 67
Maana ya neno la kiarabu ISLAM ni mnyenyekevu kwa kiswahili......, Hii aya inamzungumzia Ibrahimu kama muongofu na mnyenyekevu mbele za Mungu ila sio Muislam kwa maana ya Dini
 
Tuanze na yeye mwenye kitabu chake biblia...wapi IBRAAHIM ALIAMINI KATIKA UTATU MTAKATIFU, WAPI IBRAAHIIM ALIAMINI KATIKA YESU KUWA MWANA WA MUNGU NA NI MUNGU...BASI KAMA HAITOSHI LETA ANDIKO KWENYE BIBLIA LINALOSEMA IBRAAHIIM ALIKUWA MKRISTO...

Tutawapa andiko kwenye Quran linalosema IBRAAHIM ALIKUWA MUISLAAM NA ALITAMKA MWENYEWE...NA ALIMUOMBA MUNGU WAKE AWE MUISLAAM...
Kwanza hakuna kitabu cha Mungu kinachoitwa Biblia.
Hili linabaki hivyo kwanza.


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
We ni moja ya yale majitu tunaita makubwa jinga. Sasa anakuaje muislamu wakati uislamu haukuwepo?
Ulikuwepo:

۞ شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ ۚ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ

(ASH-SHUURA - 13)
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom