Mimi kwa mtazamo wangu haijatajwa Nabii Ibrahimu (as) ana dini gani, kilichotajwa ndani ya Qur'an ni kwamba Nabii Ibrahimu alikuwa mnyenyekevu/aliyejitupa kwa Allah na hii unaweza kupata katika Qur'an 2:127-128, ambapo amemuomba Allah amfanye awe mnyenyekevu, neno unyenyekevu ndio "Islam" na mtu mnyenyekevu anaitwa "muslim" kwa kiarabu, hivyo popote nabii Ibrahimu anapotajwa ndani ya Qur'an kwa jina la la "Muslim" maana yake ni hiyo kwamba yeye ni mnyenyekevu na hata manabii wote wanabeba sifa hiyo ya kuitwa "Muslimina" yaani wanyenyekevu mbele ya Allah.
Kitu kinacho wachanganya watu ni kuona manabii wameitwa Muslimina na hivyo kusema kwamba wao ni Waisilamu waliofuata dini ya Kiisilamu dini hii iliyoanzishwa na mtukufu mtume Muhammad (saw)-- kitu ambacho sio sahihi kwani Dini hii ya kiisilamu imejengwa katika nguzo 5 na nguzo ya kwanza (shahadatein) ambayo ili uwe muisilamu lazima uitamke katika kila swala (katika kikao cha attahiyyatu) nk, je kama nabii Ibrahimu alikuwa mfuasi wa dini hii (hata kabla haijaanzishwa) alikuwa akitoa hii shahada hii?? je alifunga swaumu hii ya Ramafhani??, kuna maswali mengi kwa wale wanaoshindwa kujua Nabii Ibrahimu anapoitwa Muslim ina maana gani!!.
Hivyo nabi Ibrahimu (as) ni Muslim kwa maana ya unyenyekevu na sio Muslim kwa maana kwamba yeye ni mfuasi wa dini hii ya Kiisilamu dini iliyoanzishwa na mtukufu mtume Muhammad (saw) ambayo imejengwa katika nguzo tano, na manabii wote wameitwa Muslim kwa maana hiyo ya kuwa wao ni wanyenyekevu mbele ya Allah.