Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mtoto wa kwanza nilimzaa na class mate wangu. Wakati huo wote tukiwa hatuna ajira. Wazazi wote walitusaidia. Ikifika wakati kaka yake alimuita Gabon akamsaidie biashara. Aliniacha na mtoto wa miaka miwili. Tulipoteza mawasiliano.
Mtoto wa pili nilimzaa na aliyekuwa boss wangu. Alikuwa msaada mkubwa kwangu. Alisaidia hata ada ya shule ya mtoto mkubwa. Huyu bwana alipata matatizo kazini na alifungwa.
Mtoto wa tatu nimemzaa na jirani yangu. Huyu kaka ndiyo kwanza alikuwa amehamia mkoa huu. Mimi nikiwa mtu wa karibu nilimsikiliza chakula na kumfahamisha mji. Nilipopata ujauzito aliamua kunifahamisha kwa ndugu zake.
Baba Tatu anataka kunioa na mipango ya mahari imekamilika. Baba Mosi na baba Pili wote wamerudi na kila mtu anataka kuanzisha familia na mimi.