Baba yangu mzazi amepangisha chumba changu

Miaka 48 unajiita kijana?
Habari zenu ndugu zangu, naandika nikiwa na hasira kali sana juu ya uyu baba yangu mzazi, mimi ni kijana wa umri wa miaka 48, sijaoa bado ila nina mtoto mmoja, ambaye yupo kwa bibi yake upande wa mama yake. mwaka huu mwezi wa tano niliondoka nyumba lasmi baada ya kuona baba angu ameanza manyanyaso mpaka kufikia atua ya kuwa nanyimwa chakula, kwa kumuamuru mfanyakazi wa ndani asiwe anapika chochote kile asubuhi na mchana, baada ya kuona iyo hali inazidi kuwa mbaya kwangu nikaondoka kabisa nyumba mwaka huu mwezi wa tano.

Nikaenda kupanga chumba maeno ya Mabibo Relini, nimekaa uko kwa muda wa miezi 5 nikiwa nabangaiza hapa na pale, ndugu zangu nikili kabisa kuwa maisha yamekuwa magumu sana kwangu, nimeamua week hii kurudi nyumbani, cha kushangaza nafika nyumbani na kukuta chumba changu nilichokuwa nakaa amepangishwa mtu, nilipata hasira sana na kumuambia mzee mimi kama sio mtoto wake aseme.

Ndugu zangu iliniuma sana mzee kusema kuwa ndio sio mtoto wangu na naomba uondoke hapa kwangu haraka sana, anadai sijui amepoteza pesa zake nyingi kunisomesha mpaka level ya degree ila sina msaada wowote, nikamuambia kuwa kunisomesha sio tatizo kama ningekuwa sina juhudi za kusoma kwa bidii ningepata ata iyo degree au kwa kuwa yeye kutoa pesa ndio imekuwa ni sehemu ya kuninyanyasa.

Niliamua kwenda moja kwa moja kwa mjumbe wanyumba kumi wa hapo mtaani kwetu ila nilicho gundua mjumbe na mzee wangu lao ni moja maana nae anadai sina haki yoyote kwa sasa.

Ndugu zangu naadika uku machozi yananitoka naombeni ushauri wangu nataka kusogea ngazi za juu zaidi, ili kupata haki zangu za msingi, maana mzee wangu imefikia atua amewaambia mpaka askari wa mtaani kwa jina la sungusungu kuwa nikija kwake awape taarifa waje wanitoe kwa nguvu.

Muda huu nimekuja kwa rafiki yangu hapa kujiegesha kidogo uku natafakari hatua za mbele zaidia za kuchukua. Karibu kwa ushauri wenu ndugu zangu.
 
Hamna kijana wa miak 48 wewe kunguni 😅😅😅😅

Asa mpaka sasa hivi unakaa nlikuwa baba Yako 😅😅

Anyway jipe moyo utayashinda 😅😅,afu nyie ndo wazazi wetu kabisa em tufundisheni kulambana bana acheni zenu

Ila hii story ni scripted unatuongopea 😅😅😅
 
Mzee kumbe una degree? Kama ni hivyo dah nenda mahakaman kaistaki serikal kwa
 
Umri ni namba tu mzee kakosea haya maisha tu mi mwenyewe nipo home vyumba vya wapangaji kibao nikajinyakulia changu kimoja nakaa nilipoona mzee kaanza miyeyusho maswala ya misosi nikajinunulia vyombo vya kupikia nikaoa naenjoy mwaka wa tatu huu niende wapi nikaangaike manyumba yote haya,

Muombe msamaha mzee au utafute mzee mwenzake muelewa umuelezee aongee nae akuombee msamaha haya maisha tu na yeye awe muelewa sasa maana mazee mengine miyeyusho naamini mambo yatakaa sawa.
🤣🤣🤣🤣 Umetishaa
Halafu Kuna watu wanafikiri ni chai, hawajui haya mambo yapo
 
Habari zenu ndugu zangu, naandika nikiwa na hasira kali sana juu ya baba yangu mzazi, mimi ni kijana wa umri wa miaka 48, sijaoa bado ila nina mtoto mmoja, ambaye yupo kwa bibi yake upande wa mama yake.

Mwaka huu mwezi wa tano niliondoka nyumba rasmi baada ya kuona baba yangu ameanza manyanyaso mpaka kufikia hatua ya kuwa nanyimwa chakula, kwa kumuamuru mfanyakazi wa ndani asiwe anapika chochote kile asubuhi na mchana. Baada ya kuona hiyo hali inazidi kuwa mbaya kwangu nikaondoka kabisa nyumba mwaka huu mwezi wa tano.

Nikaenda kupanga chumba maeno ya Mabibo Relini, nimekaa huko kwa muda wa miezi 5 nikiwa nabangaiza hapa na pale, ndugu zangu nikiri kabisa kuwa maisha yamekuwa magumu sana kwangu, nimeamua week hii kurudi nyumbani. Cha kushangaza nafika nyumbani na kukuta chumba changu nilichokuwa nakaa amepangishwa mtu, nilipata hasira sana na kumuambia mzee mimi kama sio mtoto wake aseme.

Ndugu zangu iliniuma sana mzee kusema kuwa ndio sio mtoto wangu na naomba uondoke hapa kwangu haraka sana, anadai sijui amepoteza pesa zake nyingi kunisomesha mpaka level ya degree ila sina msaada wowote.

Nikamuambia kuwa kunisomesha sio tatizo kama ningekuwa sina juhudi za kusoma kwa bidii ningepata hata hiyo degree au kwa kuwa yeye kutoa pesa ndio imekuwa ni sehemu ya kuninyanyasa?

Niliamua kwenda moja kwa moja kwa mjumbe wa nyumba kumi wa hapo mtaani kwetu ila nilichogundua mjumbe na mzee wangu lao ni moja maana nae anadai sina haki yoyote kwa sasa.

Ndugu zangu naadika huku machozi yananitoka naombeni ushauri wangu nataka kusogea ngazi za juu zaidi, ili kupata haki zangu za msingi, maana mzee wangu imefikia hatua amewaambia mpaka askari wa mtaani kwa jina la sungusungu kuwa nikija kwake awape taarifa waje wanitoe kwa nguvu.

Muda huu nimekuja kwa rafiki yangu hapa kujiegesha kidogo huku natafakari hatua za mbele zaidia za kuchukua. Karibu kwa ushauri wenu ndugu zangu.
Kuna mama huko uzunguni amewapeleka watoto wake mahakamani ili wahame kwake wakajitegemeee,

Jiuli wataki baba yako ana miaka 40 alikuwa anaishi kwa baba yake?(babu yako ) kama jibu ni hapana nawe hama hapo nyumbani
 
Habari zenu ndugu zangu, naandika nikiwa na hasira kali sana juu ya baba yangu mzazi, mimi ni kijana wa umri wa miaka 48, sijaoa bado ila nina mtoto mmoja, ambaye yupo kwa bibi yake upande wa mama yake.

Mwaka huu mwezi wa tano niliondoka nyumba rasmi baada ya kuona baba yangu ameanza manyanyaso mpaka kufikia hatua ya kuwa nanyimwa chakula, kwa kumuamuru mfanyakazi wa ndani asiwe anapika chochote kile asubuhi na mchana. Baada ya kuona hiyo hali inazidi kuwa mbaya kwangu nikaondoka kabisa nyumba mwaka huu mwezi wa tano.

Nikaenda kupanga chumba maeno ya Mabibo Relini, nimekaa huko kwa muda wa miezi 5 nikiwa nabangaiza hapa na pale, ndugu zangu nikiri kabisa kuwa maisha yamekuwa magumu sana kwangu, nimeamua week hii kurudi nyumbani. Cha kushangaza nafika nyumbani na kukuta chumba changu nilichokuwa nakaa amepangishwa mtu, nilipata hasira sana na kumuambia mzee mimi kama sio mtoto wake aseme.

Ndugu zangu iliniuma sana mzee kusema kuwa ndio sio mtoto wangu na naomba uondoke hapa kwangu haraka sana, anadai sijui amepoteza pesa zake nyingi kunisomesha mpaka level ya degree ila sina msaada wowote.

Nikamuambia kuwa kunisomesha sio tatizo kama ningekuwa sina juhudi za kusoma kwa bidii ningepata hata hiyo degree au kwa kuwa yeye kutoa pesa ndio imekuwa ni sehemu ya kuninyanyasa?

Niliamua kwenda moja kwa moja kwa mjumbe wa nyumba kumi wa hapo mtaani kwetu ila nilichogundua mjumbe na mzee wangu lao ni moja maana nae anadai sina haki yoyote kwa sasa.

Ndugu zangu naadika huku machozi yananitoka naombeni ushauri wangu nataka kusogea ngazi za juu zaidi, ili kupata haki zangu za msingi, maana mzee wangu imefikia hatua amewaambia mpaka askari wa mtaani kwa jina la sungusungu kuwa nikija kwake awape taarifa waje wanitoe kwa nguvu.

Muda huu nimekuja kwa rafiki yangu hapa kujiegesha kidogo huku natafakari hatua za mbele zaidia za kuchukua. Karibu kwa ushauri wenu ndugu zangu.

mimi ni kijana wa umri wa miaka 48,....... 🥴🥴🥴, Baba yangu amepangisha chumba changu.... 😐😐
 
Cha kwanza wewe sio kijana,wewe ni mzee acha kulalamika kama mtoto mdogo.
 
Hiki kisa kishawahi kuletwa humu.

Sema nini mwanangu mpeleke mahakani, iambiw mahakama mzee alikupata kwenye starehe zake, we hukuwa na mpango wa kuja duniani, hivyo anapaswa kusimamia show nzima, hataki akurudishe kwenye kende😂🤣
😂😂🤣
 
Huna haki yoyote kwa Sasa

Umeshapita miaka 18 hivyo sio jukumi lake kisheria.

Haki utaipata akifa
Na akifa alisema hataki asogelee mwili wala kaburi lake,na akivunja utaratibu mzee atafufuka amtie adabu kijana wa hovyo
 
Umesema una miaka 48 halafu baadae ukasema "baba amepangisha chumba changu".....

Kwa huo umri ulivyosema "chumba changu'', moja kwa moja nikajua chumba ulichojenga ww
 
una utindio wa ubongo nduguu...sema baba ako kama anajitambua ilibdi akuripoti polisi umekuja kumfanyia fujo nyumbani kwake.
Fujo gani? Si mwanae na hapo si kwao kwani ni sheria gani kifungu kipi kinaeleza ukomo wa umri wa mtu kutoka kwao
Nyumbani ni nyumbani.
 
Nigekua baba yake huyu boya na mpa sumu hiyo ni hasara, umri huo ni wakulea wazazi sio wewe kulelewa tena na wazazi.
Mkuu sio hivyo kumbuka haya maisha tu we kama unao uwezo jenga nyumba za kutosha maana kwenye watoto wako sio wote watatoka home so wapate pa kukaa hapo nyumbani
 
Back
Top Bottom