Babati: Viongozi BAVICHA Taifa wakamatwa na Jeshi la Polisi kwa kufanya mkusanyiko usio na kibali

Babati: Viongozi BAVICHA Taifa wakamatwa na Jeshi la Polisi kwa kufanya mkusanyiko usio na kibali

Chadema ini
Leo, viongozi wa BAVICHA, John Pambalu na ujumbe wake wamekamatwa na jeshi la Polisi Babati wakiwa kijiweni, wakijadili na vijana wenzao masuala ya nchi yao.

Polisi Babati wanasema hili ni kusanyiko lisilokuwa na kibali, hivyo John Pambalu (mwenyekiti wa BAVICHA) na wenzake 7 wamekamatwa kwa kosa hilo.

PICHA: Viongozi wa BAVICHA Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti John Pambalu wakiwa kwenye kijiwe cha Kahawa wakitoa elimu ya Uraia kuhusu KATIBA MPYA.


CHADEMA ijitoe kwenye mazungumzo na Hawa mafisadi. Shauri yao wanawaziabaisha waje wawafunge mdomo. Mbowe ashtuke mapema maana kesi ya kina mdee ipo na huku akina Pambalu wanakamatwa.
 
Pambalu kwao ni babati? Mbona jezi za chama kazipigilia na wenzie? Hapo ni familia au chama?

Mbona Shaka hakukamatwa wakati yupo kijiweni. Nchi Ina laana ndio maana imeshuka kwenye Uchumi wa Kati.
 
Sikia acheni Kuwahamasisha watu kugomea SENSA. Afu acheni kuwafata watu kwenye kazi zaoo na badala yake fanyeni mikutano ya Hadhara ili watu waje na wasiopenda wasijee. Sio kufata watu kwenye kazi zao

Hapo ni kazini au kwenye kahawa kijiweni wanaongea. CHADEMA itawasumbua Sana.
 
Wapuuzi kweli nyie badilisheni kwanza Katiba ya Chadema Mbowe aache kutawala maisha.

Na nyie badilisheni katiba ya CCM Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti washindanishwe sio kupita kwa kura za ndio. Halafu tofautisha katiba ya Chama siasa na Katiba ya nchi. Watanzania wachache na wanachama wa vyama vya siasa.
 
Taarifa: Jeshi la Polisi limewakamata na kuwashikilia viongozi na wafuasi wa CHADEMA waliopanga kufanya fujo huko manyara wakidai ni kongamano la Katiba Mpya.

Viongozi hao wa BAVICHA Twaha Mwaipaya , John Pambalu na wenzao wako kizuizini kwa kuvunja Sheria za nchi.

Please kupanga fujo ndio Nini?. Mmeona bungeni mnafanya utumbo mmeona hasira mmalizie kwa CHADEMA.
 
pamoja na mazungumzo yanaendelea lakini serikali inawaonyesha inaweza kuwafanya chochote,wakati wowote.

Serikali ya kijinga. Inatumia nguvu nyingi kwa CHADEMA kuliko uchumi. Ndio maana walishuka kwenye uchumi wa Kati. Bungeni mmejaa wenyewe lakini roho mbaya bado inawatafuna muiharibie CHADEMA.

Wananchi Hali ngumu lakini mmekalia kupambana na chadema.
 
Chama kina hali mbaya kifedha, inabidi mbinu za kimkakati zitumike kujifanya mko na wananchi, kumbe ndio mnamakiza na ratiba ya chai
Leo, viongozi wa BAVICHA, John Pambalu na ujumbe wake wamekamatwa na jeshi la Polisi Babati wakiwa kijiweni, wakijadili na vijana wenzao masuala ya nchi yao...
 
Back
Top Bottom