Babu ana haki ya kuwazuia hao wataalamu wa wizarani kwani uchunguzi wao umelalia katika mambo mengi ambayo yatapunguza utendaji wa babu wa kuwahudumia wengi. Pili hawa watakuwa wameambatana na wale watu wa tiba mbadala pale muhimbili ambao kimaingi utafiti wao haujawahi kuisaidia jamii ya kitanzania. Kuna njia nyingi za kupima kama walivyodekeza baazi ya wachangiaji, ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi wale waliyokunywa dawa na matokeo yake. Na pili ni kuchukua majani ya mti ambao babu ashautaja na kuufanyia uchunguzi wa kina. Kama ndivyo ilivyo kwamba babu kaoteshwa hiyo dawa na Mungu kuna masharti ambayo atakuwa amepewa na yatakuwa yanahitaji umakini na utiifu wa hali ya juu. God is simplicity, mambo yake anafanya kirahisi sana na hahitaji kusaidiwa na akili za binadamu. Ninachomaanisha ni kwamba agizo lake halihitaji kufanyiwa ukarabati wa wazo mbadala isipokuwa tu amelirejelea mwenyewe na kuelekeza vinginevyo. Hivyo watz tuache malalamishi na tujaribu kumuunga mkono babu kwa kile kipaji Mungu alichomtunukia. Watakaofaidika na huo uponyaji kama sio wewe basi ni baba,mama,shangazi,mjomba ama ndugu kwa namna yoyote. Walalamishi najua kwa vyovyote vile watakuwepo ila cha kujua ni kwamba watu wa namna hiyo wamekuwepo hata enzi za Musa nabii wa Mungu.
.