Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Kama dawa zinafanya kazi vzuri bac mungu twakuomba uumpe maisha marefu na usimpe moyo wa kifisadi ili asaidie wengi
 
Serikali iache kufuatilia masuala ya Kiimani. Mtasikia tuu serikali itataka ipime yale maji wanayotumia kubatizia watu kama yanakubalika kiafya au lah
 
Hapa ndio ambapo hutofautiana na wengi. Serikali ina wajibu kwa wananchi yao. Tumekwishaelezwa hali ya mazingira eneo lile ni ya kuhuzunisha kwa hiyo kuna hatari ya milipuko ya magonjwa. Pia hiyo dawa ikileta madhara in the long run, ni nani atakayelaumiwa kama si serikali kwa kutoakuchukua hatua? Hivi kama ni dawa kuna tatizo gani utafiti ukifanyika kwenye dawa hiyo? Kuna mengine tunalaumu bure. Kwangu mie hatua hii imechelewa.
 
Kwa kweli watu tunazidi kufarijika na habari za Loliondo. Kitu ambacho bado sijaelewa, hivi watu wote mnatumia kikombe hicho hicho kimoja au unakwenda na kikombe chako unamiminiwa? Babu mungu akupe maisha marefu.
 
jamani leteni mbegu za uo mti huku dar tuoteshe labda utatusaidia mbeleni kujitibu wenyewe! serikali ishakuwa kuku aliyekatwa kichwa anakimbia hovyo tu bila kujua pa kukimbilia.

wizara badala ya kupeleka dawa na magodoro amana na mwananyamala watu wanalala chini na hakuna dawa wanaangaika na babu???
 
Yule babu wa Loliondo aliyepata umaarufu kwa muda mfupi kutokana na dawa yake kutibu magongwa sugu amefungiwa kuendelea ma kutoa dawa kwa wagonjwa na wizara ya afya,wizara imesema inataka kuifanyia utafiti dawa hiyo pia wamemsauli mchungaji huyo mstaafu kuisajili dawa yake mamlaka ya chakula na dawa(TFDA). Source.Channel ten habari ya saa 7 mchana.

Wasi wasi ni
How long huo utafiti utachukua?

  • Kujua chemical contect na compostion ya kitu ni kitu ambacho kinaweza kufanyika within 24 hours sabbau maabara zipo

  • Kujua faida au madhara na inaleta mabadiliko gani kwenye mwili wa ni kitu kinaweza kuchukua muda lakini wapo wagonjwa wameshatumia dawa na wapo watu tayari kujitolea kuendelea kutumia dawa so sababu test sample ya watu ipo na watumiaji wapo majibu ya utafifi wa awali hayatakiwi kuzidi siku 7.
Lets wait and see see huyu mama blandina nyoni. Napenda style yake ya ufanyaji kazi ya mambo kufanyika chap chap. This case may prove my percecption to her wrong

Na zaidi ya kusajili hiyo dawa TFDA serikali inatakiwa imsaidie kusajili hakimiliki ili hata makampuni makubwa yakitaka kutengenza dawa zinazoendana na hiyo babu alipwe.
 
Huku idadi ya watu wakizidi kumiminika katika kijiji cha samunge tarafa ya sale wilayani loliondo kupata kile kinachoitwa dawa ya mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT Ambilikile Mwasapila serikali imetoa amri kupitia kwa waziri wa afya kuwa babu huyo anapaswa kusitisha huduma yake hiyo mpaka utafiti ufanyike. Akiongea na waandishi wa habari hivi punde jijini Dar waziri wa afya Dr Haji Hussein Mponda amesema kuwa ni lazima babu huyo asitishe huduma zake mpaka utafiti ukamilike pia amemtaka babu huyo kufata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kuisajili huduma yake hiyo.

dr_haji-mponda.jpg

source http://novadream.blog.com/
 
Leo hii watu wanahangaika kutafuta tiba za kisukari, BP n.k ambapo magonjwa haya ni matokea ya vyakula tunavyokula ambavyo havijafanyiwa tafiti za kutosha kwa matumizi ya mwanadamu. Wahusika wangeweka kipaumbele katika utafiti wa vyakula na madawa yanayoingia nchini ambayo yamepelekea leo hii watu kuhaha kutafuta tiba.
 
Babu ana haki ya kuwazuia hao wataalamu wa wizarani kwani uchunguzi wao umelalia katika mambo mengi ambayo yatapunguza utendaji wa babu wa kuwahudumia wengi. Pili hawa watakuwa wameambatana na wale watu wa tiba mbadala pale muhimbili ambao kimaingi utafiti wao haujawahi kuisaidia jamii ya kitanzania. Kuna njia nyingi za kupima kama walivyodekeza baazi ya wachangiaji, ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi wale waliyokunywa dawa na matokeo yake. Na pili ni kuchukua majani ya mti ambao babu ashautaja na kuufanyia uchunguzi wa kina. Kama ndivyo ilivyo kwamba babu kaoteshwa hiyo dawa na Mungu kuna masharti ambayo atakuwa amepewa na yatakuwa yanahitaji umakini na utiifu wa hali ya juu. God is simplicity, mambo yake anafanya kirahisi sana na hahitaji kusaidiwa na akili za binadamu. Ninachomaanisha ni kwamba agizo lake halihitaji kufanyiwa ukarabati wa wazo mbadala isipokuwa tu amelirejelea mwenyewe na kuelekeza vinginevyo. Hivyo watz tuache malalamishi na tujaribu kumuunga mkono babu kwa kile kipaji Mungu alichomtunukia. Watakaofaidika na huo uponyaji kama sio wewe basi ni baba,mama,shangazi,mjomba ama ndugu kwa namna yoyote. Walalamishi najua kwa vyovyote vile watakuwepo ila cha kujua ni kwamba watu wa namna hiyo wamekuwepo hata enzi za Musa nabii wa Mungu.
.
 
Hivi hii serikali iliyoshindwa majukumu yake inahusikaje na shughuli za babu wa Loliondo? Jamani ama kweli tunashida sana nchi hii serikali ya marufuku imetoka wapi? yaana baada ya kusaidia kuboresha mazingira watu wapate huduma wao wanapiga marufuku? hivi wananchi ni mabwege kiasi hicho mbona hawapigi marufuku hospitali yao ya ocean road inayoendelea kuua watu wasio na hatia kila siku hebu tuamkeni watanzania wenzangu hawa majuha kalulu tukiwaachia tutaigia nao msikitini

sasa mkuu hapo mambo ya msikitini yameingiaje?
 
napenda watu wawe na afya njema na natamani watu wasiwe na hofu kwa magonjwa ila naomba nitarudi baada ya wiki moja kuwapa taarifa kamili maana kuna wagonjwa wawili KCMC walienda loliondo wakapata tiba wakaacha dawa baada ya siku tatu ugonjwa ukachachamaa wapo hoi!
wagonjwa wa OPD wamepungua sana hasa wale wa kisukari na HIV hivyo baada ya wiki nitawapa matokeo ya uchunguzi wangu.ila nawatakia kila la kheri
 
Hiyo ni sawa na kupoteza tumaini La uhai wa watu,kuna binadamu ndio ilikua nafasi yao ya kupona hii,vipi kama watapoteza uhai, kuna wakati mwingine busara itumike zaidi kulingana na mazingira halisi kuliko kufuata kanuni, watu wanaumwa na washaangaika muda mrefu miaka kwa miaka unamwambia mtu asubiri utafiti kwa vile uhai wake nao unasubiri huo utafiti..waache habari zao bana...
 
hapo hawapimi hiyo dawa ila wanapima nguvu za mungu...Mungu anaweza kuniotesha mimi hapa na akasema edson mwanangu unauona huo mchongoma hapo mbele yako...juma majan yake, chemsha, kisha wape watu watapona.......

michongoma ipo mahali pengi na imetapakaa..lakini mungu ameuchagua mchongoma wangu mbele hapo.....

sasa hawa wanakuja kupima mchongoma au nguvu ya mungu iliyomo ndani ya mchongoma.....???

wapuuzi sana hawa
 
Bi mkora glasi ni nyini na pia ana wahudumu,ye anaweka then wahudumu huwapa wagonjwa na walio hoi wna pona on the spot.nimeshuhudia with my naked-eyes.
Pia ni kweli ametoa angalizo kwamba kwa yeyote atakae pandisha bei ya v2 hatafaidika kwakukomoa wagonjwa.i left kwa babu kama sa2 na nusu am na bado nipo loliondo.nanauli zinafanyiwa ufumbuzi iwe ile ile 37000 kwenda nakurudi ila msosi bei bado inatisha
 
hapo hawapimi hiyo dawa ila wanapima nguvu za mungu...Mungu anaweza kuniotesha mimi hapa na akasema edson mwanangu unauona huo mchongoma hapo mbele yako...juma majan yake, chemsha, kisha wape watu watapona.......

michongoma ipo mahali pengi na imetapakaa..lakini mungu ameuchagua mchongoma wangu mbele hapo.....

sasa hawa wanakuja kupima mchongoma au nguvu ya mungu iliyomo ndani ya mchongoma.....???

wapuuzi sana hawa
 
[/COLOR]
sasa mkuu hapo mambo ya msikitini yameingiaje?

nadhani alichojaribu kueleza kaka ni msisittizo tu hana uhusiano wa moja kw moja na mskitini anajaribu kueleza hisia zake ni jins gani amekwazwa na jambo hli,tumuelewe wana JF.
 
Kwa kweli watu tunazidi kufarijika na habari za Loliondo. Kitu ambacho bado sijaelewa, hivi watu wote mnatumia kikombe hicho hicho kimoja au unakwenda na kikombe chako unamiminiwa? Babu mungu akupe maisha marefu.

Vikombe vipo vingi. Ni sawa na kushiriki chakula cha bwana au au utatu mtakatifu, kwamba unakunya ule mvinyo kwa imani ya kukusafisha mwili wako na kuondoka magonjwa na laana zote, kisha babu anaomba, mwenye imani anapona papo hapo.

Babu ubarikiwe, kutoa ni moyo.
 
Back
Top Bottom