Badala ya kubinafsisha mashirika yanayotushinda kwa kampuni za nje kwanini tusitafute ma CEO kutoka nje, wenye uzoefu na kazi hizo?

Badala ya kubinafsisha mashirika yanayotushinda kwa kampuni za nje kwanini tusitafute ma CEO kutoka nje, wenye uzoefu na kazi hizo?

Yanafanya vizuri lakini hao wawekezaji wanachukua sehemu kubwa ya faida wanayopata na kupeleka kwao. Na si kwamba wanachukua Tsh, wanachukua dola. Yaani humu wanafanya biashara kwa Tsh lakini wanapopeleka faida kwao wanaondoka na dola. Akiba yetu ya dola inapungua huku thamani ya pesa yetu ikizidi kuporomoka.
Mbona kama mlemavu wa akili wewe? Yaani ulitaka TBL au TCC wakuachie ngapi? Labda umezaliwa after 1990 wewe.

Nikupe mfano mmoja hapa wa TBL wakati ikiwa chini ya Serikali na wakati ikiwa chini ya inBev/ SABMILLER. Wakati ikiwa chini ya Serikali haijawahi kutoa gawio, ilikuwa inalipa kodi kidogo kwa kuwa uzalishaji ulikuwa mdogo n vilevile bidhaa zilikuwa chache kwenye soko hivyo kuleta ajira kidogo.

Ikiwa chini YA SABMILLER/ inBev kila mwaka Serikali inapata gawio kubwa, kodi kubwa na imesabisha ajira kwenye mnyororo wa thamani
 
Yani pale ch muhimu bor apewe muhindi tu apewe n target kama private sector tu. Akiishibdwa kufikiksha anapigiwa chini muone watu watakavyohanya
Akipewa muhindi mishahara itaporomoka toka laki 8 hadi laki 3 😂😂😂 na vile wizi utakuwa hamna wengi wataikimbia ile kazi. Naunga mkono hoja
 
Ceo anayefahamu kazi anayopewa na amewekewa viwango vya kufikia cha kwanza atakuonyesha njia itakayomuwezesha kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuondoa red tape na bureaucracy zisizo za lazima..utakuwa mjinga wewe unayempa kazi km utakataa kufanya anayokushauri mtendaji! Hizo bureaucracy sio misahafu zinabadilishwa au hata kuondolewa kabisa kwa mwenye kutaka matokeo..!
Unaondoaje red tape kwenye Shirika lililo mali ya Serikali kwa kuwa wewe ni CEO tu mwenye uwezo?

Kwa mfano uko TANESCO unaambiwa mashine ya kupooza umeme wa kutoka JNHEP imeungua na inahitaji replacement. Je unaweza kufanya nini kama CEO na kununu mashine nyingine ndani ya masaa 38 kwa mfano, assuming hiyo mashine inapatikana Dar es Salaam with existing Public Procurement Act of 2015?
 
Shida sio CEO, shida ni mtazamo wa wafanyakazi. Nimewahi kufanya kazi nje ya Tanzania na baadae Tanzania. Niliyoyaona ni watanzania wanapenda kupata mishahara na marupurupu bila ya kuitolea jasho. Tanzania tuna kizazi kisichoamini kutimiza wajibu bali ujanja ujanja.
CEO anaweza kuwa na tija ikiwa atalinda integrity na kuwa tayari kuachia ngazi ikiwa watamletea mauza uza ila tumeona ma CEO wengi walioletwaga na Jakaya kutoka nje wengi waliishia kuwa mafisadi japo walianza vizuri. System yetu ya nchi hairuhusu watu wenye vision kubwa ku prosper hasa katika nafasi kubwa za uongozi sababu integrity ni kitu ambacho kina miss kwenye mfumo. Ukiwa mwadilifu unaonekana kituko na ili uendane na mfumo lazma watakubadili uwe jambazi kama wao.
 
CAG awe anatoa mchanganuo wa maeneo yaliyosababisha hasara au faida ya shirika,
-CAG awe anatoa ufafanuzi unaonyesha kama mapato na matumizi ya shirika yameshuka au kuongezeka mwaka wa ukaguzi .
-CAG aonyeshe kama kuna ubadhirifu wa fedha za shirika au uwezo mdogo wa uendeshaji na menejimenti ya biashara ya shirika.
-CAG aonyeshe kama hasara inasababishwa na maamuzi ya kisiasa,
-kwa mfano ATCL,zile ndege zinanunuliwa na Serikali na kukabidhiwa TGFA.
-TGFA inakodisha ndege ATCL,na ATCL hutakiwa kulipa fixed rental charges TGFA regardless ndege iwe imefanya kazi au Iko grounded au imepelekwa matengenezo (check 3) nk.
-TGFA wanatuma Ankara ya rental charges ATCL.
-Mlolongo huu husababisha ongezeko la gharama za uendeshaji wa ATCL na ongezeko la mapato ya TGFA, lakini Muamala huo,ni kama window dressing.
-
Ushauri
-Serikali ikabidhi ndege ATCL moja kwa moja badala ya kukabidhiwa TGFA ambao wanakodisha ATCL
-Mama kuna sababu mahususi,inayofanya Serikali kukabidhi ndege TGFA,basi watendaji wa TGFA na ATCL wakae pamoja kufanya mapitio ya mikataba yao na kuja na reasonable rental charges.
-Mizania/Mahesabu ya taasisi hizi mbili yafanyiwe marekebisho ipasavyo
 
Mbona kama mlemavu wa akili wewe? Yaani ulitaka TBL au TCC wakuachie ngapi? Labda umezaliwa after 1990 wewe.

Nikupe mfano mmoja hapa wa TBL wakati ikiwa chini ya Serikali na wakati ikiwa chini ya inBev/ SABMILLER. Wakati ikiwa chini ya Serikali haijawahi kutoa gawio, ilikuwa inalipa kodi kidogo kwa kuwa uzalishaji ulikuwa mdogo n vilevile bidhaa zilikuwa chache kwenye soko hivyo kuleta ajira kidogo.

Ikiwa chini YA SABMILLER/ inBev kila mwaka Serikali inapata gawio kubwa, kodi kubwa na imesabisha ajira kwenye mnyororo wa thamani
Si kosa lako mkuu. Uelewa ndiyo mdogo. Ni hivi, hao TBL na TCC hata kama wanazalisha faida kiasi na ajira na kodi kiasi gani kwa nchi lakini wanachukua faida na kupeleka kwao. Faida hiyo wanaichukuwa ikiwa katika dola na si madafu. Wanavyoingiza faida kubwa zaidi ndivyo wanavyoondoka na dola nyingi zaidi. Wanavyoondoka na dola nyingi zaidi ndivyo Tsh inavyozidi kushuka thamani. Ndivyo tunavyozidi kupata uhaba wa dola. Ndivyo tutakavyohangaika kuagiza mafuta na dawa na ngano nk nk. Hao ni tofauti na watu kama Barrick au Mwadui. Wao wanachimba madini ambayo wanayauza nje kwa dola na hivyo kuingiza dola nchini. Unapokaribisha uwekezaji nchini jambo la muhimu sana kuangalia kama utakuletea fedha za kigeni au utaziondoa.
 
Ndiyo. Inatakiwa mkataba wa kazi umpe yeye na timu yake madaraka ambayo kazi yake haitaingiliwa lakini anaweza kuwajibishwa.
Sasa hapo ndio unamfunga mikono 😂
Eg, haya makampuni hayawez punguza mishahara, yatalazimishwa tumia sheria za serikali, yatalazimika kuwa na audited financials nying ambazo at the end zinaenda kuua creativity
 
Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.

Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.

Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.

Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.

Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.
Mkuu ni kama ulikuwa kichwani mwangu.
 
CEO ni decision maker. Na exposure yake na connection itasaidia kuwavusha pale ambapo usually hua kuna foleni.

Maamuzi yote atayafanya kulingana na data atazogewa na wa chini yake. And mostly CEO hua anakuja na camp yake anayoiamini kuanzia wingman mpaka secretary.

Ukiniuliza mimi nitasema mashirika yetu hayafi kwaajili ya CEOs yanakufa kutokana na wakuu wa idara kushindwa kuendana na kasi ya ulimwengu.
 
Ilitakiwa zote nafasi kubwa za umma kuanzia wakuu wa wilaya,mikoa,wakurugenzi wa Idara na taasisi ,wakuu wa mashirika na vitengo yao nk Zingekuwa za ushindani wa kuomba nchi ingepata viongozi wazuri sana.Wanaomba wengi wanafanyiwa interview na Panel independent. Raisi anapelekewa majina machache achague mojawapo .Hapo tutapata wakuu wa wilaya ,mikoa ,maafisa wakuu ea serikali wazuri sana.Ikitangazwa ruksa kuomba aliye ndani na aliye nje washindanishwe.Na akipata inatakiwa kuwa ya mkataba mfano wa miaka mitatu mitatu anayoweza ongezewa muda kutegemea na performance
Hizi zimekuwa ni nafasi za makada tupu
 
Inaonekana wazi serikali haiwezi kuendesha shirika lolote. Mwendokasi na hasara za ATC ni mfano wa karibuni juu ya kushindwa huko. Mwendokasi unaenda kutafutiwa muwekezaji kutoka nje!! Huku ni kujirudisha nyuma maana muwekezaji huyo hata kama atatoa huduma nzuri namna gani lakini atachota uchumi wetu na kupeleka kwao.

Kwa nini mashirika haya yasitafutiwe ma CEO, ma CFO nk nk kutoka nje wenye uzoefu. Wapewe madaraka na malengo. Wakifeli wanatimuiwa na kuletwa wapya.

Kama vile kwa makocha wa timu za mpira? Kwanini tusitafute mameneja wa ATC kutoka Ethiopia na nchi nyingine zilizofanikiwa kwenye upande huo.

Kwanini tusisake duniani mameneja na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mwendokasi.

Kiuchumi gharama za kuwalipa wakuu hao ni ndogo sana ukilinganisha na hasara za kiuchumi zitokanazo na kuleta kampuni za kigeni.
Swala siyo ma CEO swala ni sera na malengo ya serikali ndo ya ovyo kabisa ,binafsi naona kubinafsisha ni sawa lakin tatizo la Tanzania wapo matajir apa wenye uwezo lakin hawajitokezi kuwania izo nafas na wakijitokeza masharti ya serikali yanakuwa ya ovyo wanapotezea ,nakumbuka kuna kipindi mengi alitakaga kuwekeza kwenye gas wakasema hawawez kumpa mtu mwenye fedha za kununua machungwa so ni kama serikal inazarau watu wake na nikama serikal iko tayar kuingia hata mikataba ya kuwaumiza ilimrad watu wa njee wapate
 
Ivi mtu kama mo ameshindwa kuendesha kitu kama iko ila anajua serikal ilivo, kwanin mtu atoke njee aje apewe mali za nchi apate faida wakati tunaeza kubifshia mataji wa hapahapa, ni Bora kumpa mtanzania kwa mashart dhaif kuliko mtu wa njee kwa mikataba dhaif
 
Back
Top Bottom