Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Hiyo ya three children a maximum ni kanuni yako uliyojitungia, hata ukisoma maandiko yote ya family planning hawajaweka limit ya idadi ya watoto.

Katika family planning unaelekezwa kuzaa watoto kwa utaratibu wa angalau kila baada ya miaka 2 au 3 ili mama apate muda mzuri wa kumtunza mtoto na yeye mwenyewe Afya yake iwe katika hali nzuri kabla ya kubeba ujauzito mwingine.

Pia inatoa fursa ya kujitathimini kiuchumi Kama unaweza kuongeza mtoto mwingine. Kwa hiyo Kama mtu atafuata utaratibu huo anaweza kuzaa hata watoto Saba.

Tatizo lako inawezekana hali yako ya kiuchumi inakulazimu uishie kuzaa watoto watatu, kwa hiyo unataka kugeneralize, au umekalili tu kuwa ukifuata uzazi wa mpango basi hutakiwi kuzidi watoto watatu.
Maandiko ni hadithi za kale tu, hazina ishu, kuna maandiko mengine yanaandika umuue jirani yako Kama ni mchawi
 
nilikuwa na maana kwamba hautokuwa na uhuru nao sana; maono na unavyotaka wawe inaweza kuwa na mipaka/kikwazo sababu kuna wenye maamuzi nao pia

Uko sahihi chief lakini pia inategemea tangu mwanzo wa muundo wa hiyo familia ama ukoo mipangilio ilikuaje!

Imagine uzaliwe na ukulie katika mazingira ambayo babu na Bibi wako na opinion (sio final say) plus big financial support kwako wewe Mjukuu , huoni kwamba itakua rahisi zaidi kwako just to carry on the same traits?

Bahati mbaya sana familia zetu tunafanya mambo kinyume! Wazazi tunazaa watoto ili waje watusaidie wakati in reality wazazi tunatakiwa tuzae watoto na tuwasaidie ili waendeleze koo zetu, kwa kunyanyuana na sio kubebana!
 
Tatizo liko wapi wakikutana kliniki... mabomu yatalipuka au..?!

Hoja zako za kipuuzi tu!
Yaani kaleta hoja ya kitoto halafu anataka kila mtu akubaliane na fikra zake.

Wa kupuuzwa tu!
Mbona unakimbilia matusi (neno mpuuzi)?

Mwanaume aliyeoa binti yako anakuja kumpa hongera mkeo (mama mkwe wake) kwa kujifungua mtoto mchanga (shemeji yake)?
 
Huku kwetu vijijini tuna uwezo huo, chakula tele mashamba na hata nguvu pendwa uhakika... huko mjini dhiki nyingi chumba kimoja cha kupanga unadhani wote tunaishi hivyo?
Huko kijijini si ndio watoto wa kike wanaolewa wakiwa na miaka 12? Huko pia si ndio mabibi wanauwawa kwa tuhuma za uchawi kwa kuwa wana macho mekundu?

Tabia zisizo za staha nyingi zimejaa huko vijijini mkuu ndio maana hata hili bado unalipigia debe.
 
Wanawake wenzetu wa Uganda na kando ya ziwa Victoria huko wanazaa hadi watoto 16, siyo huku mtu watoto 2 mama kachoka kachakaa.

Ndiyo mnapata sababu za kusema mama kazaa na binti kazaa.

Acheni wamama wazae, binafsi natamani ningezaa hata 6, kila mtoto ana furaha yake kwa mzazi.

Wamama zaeni watoto wengi ,kuna mwaka mtanikumbuka.

Bado tupo wengi tunaotamani kuendelea kuzaa, tena sana!

Tatizo nyakati hazifanani na mazingira pia yanakaba!

Natamani sana nizae hata kumi lakini nataka niwape elimu bora na sio bora elimu, niwape huduma bora za afya na sio bora huduma, niwape lishe bora na sio bora lishe!

Having many children of your own is more like having a personal army! It’s tiresome at the beginning but in the end it pays up!
 
Uko sahihi chief lakini pia inategemea tangu mwanzo wa muundo wa hiyo familia ama ukoo mipangilio ilikuaje!

Imagine uzaliwe na ukulie katika mazingira ambayo babu na Bibi wako na opinion (sio final say) plus big financial support kwako wewe Mjukuu , huoni kwamba itakua rahisi zaidi kwako just to carry on the same traits?

Bahati mbaya sana familia zetu tunafanya mambo kinyume! Wazazi tunazaa watoto ili waje watusaidie wakati in reality wazazi tunatakiwa tuzae watoto na tuwasaidie ili waendeleze koo zetu, kwa kunyanyuana na sio kubebana!
mmm, una hoja lakini bado mi sioni tatizo la kuzidi la kutokuzaa
 
Wanawake wenzetu wa Uganda na kando ya ziwa Victoria huko wanazaa hadi watoto 16, siyo huku mtu watoto 2 mama kachoka kachakaa.

Ndiyo mnapata sababu za kusema mama kazaa na binti kazaa.

Acheni wamama wazae, binafsi natamani ningezaa hata 6, kila mtoto ana furaha yake kwa mzazi.

Wamama zaeni watoto wengi ,kuna mwaka mtanikumbuka.
...👊👊👊..
 
mnapenda kujiropokesha nyinyi, sasa ung'ombe hapo umeingiaje. hayo maadili mmejitungia kichwani, kwasababu sio tatizo la kimaadili kabisa
Mama na binti yake wote wanakutana leba kujifungua wewe hauoni kama sio tabia njema? Kijana ana miaka 25 anamuona mama yake ana mimba wewe hauoni kama sio staha?
 
maoni yako hayakubaliani na watu wengi, hakuna tatizo lolote, wala su ukosefu wa maadili, kwani hiyo mimba kapachikwa tu ama imepatikana kwenye mahusiano rasmi yanayotambulika!!

lini kuzaa kumekuwa jambo la nje ya maadili!!!!?
Inaonekana wewe haujaisoma mada hii kisha ukaielewa. Kuzaa sio kosa bali kosa ni kuzaa bila staha. Mama na binti yake wa miaka 24 wote wajawazito.
 
sasa ujinga gani, hujui familia kubwa ni faraja.
familia ikiwa ndogo sana misiba ikitokea huwa inachoma sana kwa maana mpo wachache, mkiwa wengi kuna amani na faraja fulani hivi

hivyo tatizo sio big family ni uwezo tu wa kulea, kama mtu ana uwezo azae tu, kama kina kardashian, ni wazungu ila familia ni kuubwa hadi inafurahisha ile ni faraja kubwa sana.
Watu wazae kadri ya uwezo wao wa kiuchumi wa kutunza watoto hao
 
Wala sio kosa, kwani hapo maadili gani kavunja, kuzaa ni kukosa maadili, nani kakwambia na mara nyingi ukiona hivyo ujue huyo mama alizaa mapema sana ndio maana mwili wake umemruhusu kubeba kiumbe kengine. Sio kosa sio dhambi sio kukosa maadili
Wewe kama kijana wa miaka 25 unajiskiaje kumuona eti mama yako ni mjamzito?
 
Brother hili swala hutakiwi kugeneralize, siyo kila mtu hana uwezo wa kulea watoto zaidi ya watatu hadi Saba. Kinachotakiwa ni mtu kufanya tathmini ya hali yake kiuchumi kabla hajachukua maamuzi ya kuongeza idadi ya watoto na pia kuzingatia ushauri wa Afya kuhusu child spacing.

Kuzaa watoto ni baraka Kama una wezo wa kuwalea na kuwapatia mahitaji yao jinsi inavyotakiwa. Kwa hiyo hakuna limit kwamba mtu anatakiwa aishie kuzaa watoto watatu ndo aonekane kuwa anafuata uzazi wa mpango.
Zaeni kwa staha na mipango maalum na sio kukurupuka tu
 
Mbona unakimbilia matusi (neno mpuuzi)?

Mwanaume aliyeoa binti yako anakuja kumpa hongera mkeo (mama mkwe wake) kwa kujifungua mtoto mchanga (shemeji yake)?
Huko juu uliandika kuwa mimi NIMEKULIA KWENYE JAMII ISIYO NA MAADILI WALA STAHA!

Unajua maana ya hayo maneno..?!

Yaani kwa kupinga hoja yako tu ukaona jamii niliyokulia mimi yote ni ya 'kishenzi'.

So, ww ndo ulianza matusi.

Hapo sijakutukana.
 
Kwa hiyo mwanaume aliyeoa binti yako anakuja kumpa hongera mkeo (mama mkwe wake) kwa kujifungua mtoto mchanga (shemeji yake)?
Angekuja kumpa hongera kwa kununua ng'ombe, gari au kujenga nyumba ungesemaje...?!

Acheni kukariri nyie watu!
 
Wanawake wenzetu wa Uganda na kando ya ziwa Victoria huko wanazaa hadi watoto 16, siyo huku mtu watoto 2 mama kachoka kachakaa.

Ndiyo mnapata sababu za kusema mama kazaa na binti kazaa.

Acheni wamama wazae, binafsi natamani ningezaa hata 6, kila mtoto ana furaha yake kwa mzazi.

Wamama zaeni watoto wengi ,kuna mwaka mtanikumbuka.
Naamini umeona mengi, kufikia kuandika hivi Basi ni wazi Kuna maana kubwa nyuma ya hii, na Mimi nikijaaliwa uhai na uzazi salama nitaifikisha idadi ya watoto 6 uliotamani kuwa nao
 
Back
Top Bottom