Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Watu wanatetea mambo ya kijinga sana humu. Mama na binti kuzaa pamoja sio maadili haya.
Haya maadili mnayoongelea ni maadili yapi? ya nchi gani hapa Afrika na kabla lipi kwa Tanzania hii, Mambo ya kimagharibi ndo mnaita maadili. Wao kule lazima walie na mafamily planing maana ardhi hawana tena.

Lakini siyo kwa Afrika hii wengi wenu mko brain washed na western beliefs and cultures. La sivyo nipe sababu za kisayansi kwa maana ya sayansi ya jamii na ambazo zinasababisha useme siyo maadili.

Wewe ukishazaliwa wazazi wako wamekupatia elimu pigana kimpango wako usianze kupiga hesabu za urithi na kuhisi kuwa babako na mamako wakiendelea kuzaa urithi utapungua. Roho ya kimaskini kabisa.
 
Was it at all worth it or even at least fair? hasa kwa hao watoto? Imagine wanaenda kuishi maisha yao yote bila baba (japo his legacy will console them) lakini nani asiyejua thamani ya baba katika malezi hasa dunia ya sasa?...
Nimeelewa
 
Wanawake wenzetu wa Uganda na kando ya ziwa Victoria huko wanazaa hadi watoto 16, siyo huku mtu watoto 2 mama kachoka kachakaa.

Ndiyo mnapata sababu za kusema mama kazaa na binti kazaa.

Acheni wamama wazae, binafsi natamani ningezaa hata 6, kila mtoto ana furaha yake kwa mzazi.

Wamama zaeni watoto wengi ,kuna mwaka mtanikumbuka.
 
Nimeelewa
Hiyo hoja ya huyo jamaa hapo juu kwangu bado haina mashiko, kufa mtu yeyote anaweza kufa hata huyo mtoto anaezaliwa leo. Lakini kwa mtu ambaye ana miaka 45 kuna shida kuendelea kuzaa. Babangu akiwa na miaka 45 mimi nilizaliwa nikiwa mtoto wa sita kwa mamangu, na waliendelea kuzaliwa wengine wengine sita.

Bahati nzuri hakuna hata mmoja anayejuta kuzaliwa kwani wote 12 kwa mama yetu ni graduate, lakini pia baba alikuwa na mke mdogo ambaye ana watoto watano. Jumla tulikuwa 17 bahati mbaya wanne wametangulia mbele haki. Binafsi nimekuwa nimekuwa nikijivunia kuzaliwa wengi.

Kwani kwa watoto 14 likitokea tatizo linalomhusu mzee au mamazetu huwa ni rahisi kuhandle, Kwa maana ya kwamba mahali panapohitajika milioni utakuta kila mtu anatoa laki 1 tu. Vipi ungekuwa mmoja mzee anahitaji matibabu pengine akilazwa hospital bora kama aghakani siku mbili tu milions of money.

Kwangu kuzaa mtu azae na asipangiwe na mtu. Nina kakangu mkubwa naye alikuwa na hoja hizi hizi kazaa mtoto mmoja tu bahati mbaya juzi tu kama miezi 2 akiwa mwaka wa pili chuo Mungu kampenda zaidi sasa hivi amebaki hana mtoto. Na mke awezi kuzaa tena make umri umeenda sasa hizo mali kwa sasa zinapigiwa hesabu na kila upande na hata wa upande wa mke.
 
mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa naona kama amekosa akili. zamani watu walikuwa wakizaa mitoto mingi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe na utengeneze future nzuri kwa kuwekeza sio waje kutembea juani wakisaka ajira
Kila mtu angekuwa anawaza hv ingekuwa vzur sana,Kuna mijitu inazaa ili mradi
 
.
Screenshot_20210105-095712_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom