And fatherlessInategemea na mazingira na familia yako ikoje.
Ndugu Marehemu Mengi alipoona hana wajukuu akaaamua kutafuta wajukuu yeye mwenyewe. They are now 6/ 7 years old.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
And fatherlessInategemea na mazingira na familia yako ikoje.
Ndugu Marehemu Mengi alipoona hana wajukuu akaaamua kutafuta wajukuu yeye mwenyewe. They are now 6/ 7 years old.
Kunywa maji ya kutosha mkuuHabari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums.
Ndugu zangu Watanzania;
Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.
View attachment 1667340
Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikuwatana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.
Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.
Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.
Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.
View attachment 1667350
Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.
Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"
Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.
View attachment 1667352
Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.
Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.
Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amelufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.
View attachment 1667341
Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.
Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.
Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?
"HAPPY NEW YEAR 2021"
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Maoni ya wadau
=====
Hiyo sio asili ya binadamuKama suala ni nature mbona kaka na dada wa tumbo moja hawaoani kama wafanyavyo wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi?
Ndo vile ndugu yangu,goodmorningSawa mkuu, nimekuelewa ulikuwa unam-quote mtu ila kwa bahati mbaya ukakosea...
That is the last stupid thing you do before you die.Sio lazima mtumie kondomu,unaweza kufunga uzazi kwa operasheni.
Hiyo ya three children a maximum ni kanuni yako uliyojitungia, hata ukisoma maandiko yote ya family planning hawajaweka limit ya idadi ya watoto.Imani za kizamani eti kuzaa watoto ni baraka
Halafu unaposema uwezo ni kitu relative mwingine uwezo kwake ni kuwapeleka watoto international school ndio anajiona ana uwezo, mwingine akiweza kuwalisha ugali maharage usiku naye anajiona Ana uwezo
Whatever the case 3 children should be a maximum for everybody
Huu ndio ukweli. Katika uhalisia, wadada huolewa beteeen 14------18 years, 15 years later, mwanaye anaanza kuzaa huku mama akiwa 30 years na bado ana mayai ya kutosha. Nimeshuhudia mama aliyezaa watoto 14, hapa lazima watoto walingane na wazazi wao[emoji3][emoji3]
Hii mada Kuna muda inachekesha Sana.
Yaani tunawafundisha maadili waliotufundisha maadili kwamba hawana maadili
Mbaya zaidi wengine wamezaliwa kwa njia hii hii au wazazi wao walizaliwa kwa njia hii hii then Sasa hivi inaonekana hawana maadili[emoji2960]
Ubaya wake nini..?!Hii mbaya sana mkuu
Mleta mada yamemkuta haya mambo, sasa anajisikia vibaya inakuwaje yeye ana miaka 25 halafu mjombaake ndo kwanza kazaliwa mkesha wa mwaka mpya, na kwa mila za kwao ni lazima AMUAMKIE kwa kupiga goti! [emoji23][emoji23][emoji3][emoji3]
Hii mada Kuna muda inachekesha Sana.
Yaani tunawafundisha maadili waliotufundisha maadili kwamba hawana maadili
Mbaya zaidi wengine wamezaliwa kwa njia hii hii au wazazi wao walizaliwa kwa njia hii hii then Sasa hivi inaonekana hawana maadili[emoji2960]
ndiyo lkn sio muda wote kila utaratibu utaenda km ulivyopanga!Mtoto ana raha yake sawa mkuu lakini ndio wazaliwe kwa utaratibu maalum
hata sijazungumzia kuzaa watoto wengi km sungura, kinachozungumzwa hapa ni sawa au si sawa kuzaa pamoja na mtoto wako. kwangu mimi nimesema sioni tatizo lolote km mazingira, hususani ya uhitaji na usalama, yanaruhusu. ndicho nilichosema mkuu!!Kwa hiyo kwa sababu wewe ni muafrika ndio uzae kama sungura? Akili za wapi hizi!
Kama Kigezo ni kipato cha kuwapa elimu watoto na future nzuri, basi hapo moja kwa moja jidharau wewe na umasikini wako, au panua wigo wa kipato, kama we ni mwajiriwa na kipato chako kiko fixed huna budi kufanya hayo mafamily planning yako.mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa naona kama amekosa akili. zamani watu walikuwa wakizaa mitoto mingi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe na utengeneze future nzuri kwa kuwekeza sio waje kutembea juani wakisaka ajira
Mtoa mada mtizamo wako sio sahihi kwa upande fulani..Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums...
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Mleta mada yamemkuta haya mambo, sasa anajisikia vibaya inakuwaje yeye ana miaka 25 halafu mjombaake ndo kwanza kazaliwa mkesha wa mwaka mpya, na kwa mila za kwao ni lazima AMUAMKIE kwa kupiga goti! [emoji23][emoji23]
Kwa mtu kama wewe na hii mentality yako basi nadhani ulistahiki kuandika hivi,lakini kwa mtu ambae anamentity ya kumkuza mtoto wake kwa kujitegemea na kuwa mpiganaji basi hawezi kuona shida kuzaa.mimi mtu anayezaa zaidi ya watoto 3 katika dunia ya sasa naona kama amekosa akili. zamani watu walikuwa wakizaa mitoto mingi kwa sababu elimu na njia za uzazi wa mpango kulikuwa hakuna, sasa hivi zipo tele, mtoto pia alikuwa akitumika kama rasilimali ya kulima shamba na kuchunga mifugo, saa hivi mtoto anatakiwa alishwe, avalishwe na asomeshwe na utengeneze future nzuri kwa kuwekeza sio waje kutembea juani wakisaka ajira
sawa, lkn bado hilo naona si salama sana kwako kwani sio wako hao....furaha ya kweli na ya kudumu ipo katika chako; isitoshe km uwezo upo bado unaweza tu kulea na hao wajukuu.Hapana sio maneno ya mwenye kushiba, hata kidogo!
Nimefikiria tu binti yangu awe na umri wa miaka 18 which means soon ataleta wajukuu kwanini nisiendelee kuwajengea wao misingi imara badala ya kuhangaika na vitanda vya leba?...