Bado nazidi kuona makosa makubwa kwenye usajili wa Simba. Kwa mwendo huu mashabiki jiandaeni maumivu tena na tena 2023-24

Bado nazidi kuona makosa makubwa kwenye usajili wa Simba. Kwa mwendo huu mashabiki jiandaeni maumivu tena na tena 2023-24

Mimi nalia na no 6 jaman kipind cha Lwanga tuliruhusu magolo machache
Tunahitaj 6 anayelinda mabeki
Ngoma/Mzamiru na Kanoute wote no 8
Msimu uliopita hatukuwa na namba 6 ila tumerusu goli chache tu,tatizo namba 6 pure huwa wanaikaba timu sometimes,mi nasimama na namba nane,coz anafanya kazi zote anaenda na anarudi kama mfano hyo ngoma anaweza sana hata kushambulia na anakaba pia.
 
Simba wanapuyanga ningewaelewa kama wangeshusha kiungo mkabaji wa asili(no 6)mmoja namba 8 mmoja.

Mechi Wyda/Raja Vs Simba kule Moroco viungo wa Simba waliwekwa store.
piga uwa Putin(Kanoute) na Kim Jong Hur(Muzamiru) inatakiwa wawe na mbadala wao.

Mechi zenye presha kubwa Putin huwa anamwaga nyuklia kiasi cha kukaribia red card.
Uko sahihi,ni lazima kiungo aje,ndo mana sawadogo na mkude waliachwa,so kuna wa kigeni mmoja na mzawa mmoja,na nmeskia wa ndani analetwa mvunja watu miguu anaitwa mtenje albano,yaani huyu kadi nje nje asee
 
Simba wana falsafa ya kushambulia kwa sana kuliko kujilinda so ni mara chache sana kuwekeza nguvu kubwa kwa viungo wa kizamani wa ukabaji(pure number 6)..tazama man city unamuona rodrigo yule ni namba 6 ila sio pure.

Sasa simba huwa wanapenda sana kutumia box to box,au namba 8,ambao ndo mpira wa kisasa unataka,kila mtu lazima awe na mchango wa magoli kwenye timu,ndo mana unaona msimu jana,kanoute kafunga,mzamiru kafunga,kapama kafunga..

Tofauti na watu kama kina mtenje albano wa coastal ambaye yeye huwa anaganda eneo lake tuu akisubiri kuvunja wenzie miguu.

Simba wanatarajia kusajili kiungo mkabaji(box to box mmoja kati ya hawa watatu,banfa sylla,efoe novon au fabrice ngoma hao wote ni box to box,tena huyo efoe na ngoma ndo kabisaaa.
Mtenje amesajiliwa Simba tayari ana subiri kutangazwa tu.
 
Asante kwa mchango wako.

USIFANANISHE Manchester city na Simba. TAFADHALI.

NIMEONA Simba IKIWA na Viungo wakabaji pure No 6
1. Mafisango
2. Kotei.
3. Tadeo LWANGA.
4. SAWADOGO.

Uwe na Uhakika na Maoni yako kaka. USIPOTOSHE.
 
Upande wa pili mna wivu sana.
Kati ya mashabiki wa Simba wanaoweza kuongelea mpira ni CAPO. Wewe hatujawahi kukusikia mbali ya kukosoa Kwa vimaneno viwili vitatu. Leta uchambuzi wako tuone.
 
Maumivu yakizidi ndio unaanza kupona.
 
Mpira umejifunza wapi ndugu yangu mbona una tia aibu ?
Chama, Saido na Sakho Sio mawinga ni viungo wa pembeni.
Aina ya majukumu ya kiungo wa pembeni sio sawa na winga.
Bernardo Silva sio winga ila alikuwa ana cheza pembeni kama kiungo wa pembeni.
Onana, Kibu hawa ni shambuliaji wa pembeni na sio mawinga.
Musonda ndani ya klabu ya Yanga ana cheza kama Mshambuliaji wa pembeni na sio winga hivyo sio kila mchezaji anae cheza pembeni ni Winga.
Kramo, Banda hawa ndio mawinga ndani ya kikosi cha Simba.
Sasa basi wachezaji hawa mwalimu (Kocha) ana watumia kulingana na mechi na aina ya mpizani mpangie mchezaji wa pembeni mwenye sifa zipi kulingana na mechi husika.
Suala la wachezaji kuzidi kuna taarifa za kuachwa Banda au Sakho kuuzwa kupisha usajili wa mchezaji mwingine.

Asante kwa Mawazo mazuri.

Nikisema niandikae kwa UFUNDI mwingi Kuna watu nitawapa wakati MGUMU kunielewa.

Natumia UFAFANUZI rafiki Ili iwe rahisi kwa WATU WENGI KUKUELEWA.

Naelewa habari za Sackho na Banda .
NAFASI Moja inachukuliwa na Golikipa.(Santos).

Kuna uwezekano mkubwa nafasi nyingine inachukuliwa na Fabrice NGOMA.

Huwa mnaona makosa ya Onyango., Ila CHANZO Cha makosa ya Onyango au Simba kushambuliwa sana ni kukosa CDM.

YANI lango na KIPA WA Simba wanafikiwa kirahisi mno.
NGOMA sio CDM.
Vita Alikuwa no 10, Raja NK.
ELMERECK 8
 
Mpango wakocha unafahamu au unaleta mipango ya ukocha wako

Ndio Maana nimeomba Uzi Huu ujadiliwe na WATU wanaojua na kuupenda mpira.

Sio Mashabiki Maandazi.
KOCHA Gani Duniani Asiye kosea?

Waswahili wamejisemea Nyota njema huonekana Asubuhi.

KAA PEMBENI

FICHA UJINGA.
 
HAO wawili.

NAFASI ya .....

1. Akpan AKICHUKUA sawadogo Dirisha Dogo.

2. NAFASI ya Okra ilichukuliwa na Saido Dirisha Dogo

Hivyo Simba ikawa na wachezaji 12.

Nimeomba wanaojua mpira ndio wajadili,.

NB. SIO KILA KIONGOZI WA SIMBA ANAJUA MPIRA.
Hili liko Wazi na ilifanya Simba iwe na Wachezaji 14 ikiwa imekopesha wawili.
 
Ndio Maana nimeomba Uzi Huu ujadiliwe na WATU wanaojua na kuupenda mpira.

Sio Mashabiki Maandazi.
KOCHA Gani Duniani Asiye kosea?

Waswahili wamejisemea Nyota njema huonekana Asubuhi.

KAA PEMBENI

FICHA UJINGA.
Amekosea wapi Kwa kuwa hajafanya unachpenda wewe
 
Najua sana usajili Bado.

Eneo Lenye mapungufu makubwa ndio lilipaswa liwe la KWANZA kulitatua.

Kwa wachezaji wa ndani hakuna kiungo mwenye uwezo wa Kucheza pale 6 Michezo Mikubwa na yenye pressure .

Pia kumbuka idadi ya Wachezaji wa kigeni imetimia 12.
Hatuwezi kuweka michango ya maana huku dirisha bado halijafungwa, hatujui nani anaweza kuondoka nani anaweza kuingia, inawezekana ilo eneo unalosema tayari usajir ushafanyika sema hajatangazwa, na inawezekana kuna watu washaondoka sema hawajatangazwa, cha muhimu ni kusubiri usajir umalizike
 
Asante kwa mchango wako.

USIFANANISHE Manchester city na Simba. TAFADHALI.

NIMEONA Simba IKIWA na Viungo wakabaji pure No 6
1. Mafisango
2. Kotei.
3. Tadeo LWANGA.
4. SAWADOGO.

Uwe na Uhakika na Maoni yako kaka. USIPOTOSHE
Upo sahihi hao ni namba sita wa asili kabisa pamoja na Matola"Veron".
 
Asante kwa Mawazo mazuri.

Nikisema niandikae kwa UFUNDI mwingi Kuna watu nitawapa wakati MGUMU kunielewa.

Natumia UFAFANUZI rafiki Ili iwe rahisi kwa WATU WENGI KUKUELEWA.

Naelewa habari za Sackho na Banda .
NAFASI Moja inachukuliwa na Golikipa.(Santos).

Kuna uwezekano mkubwa nafasi nyingine inachukuliwa na Fabrice NGOMA.

Huwa mnaona makosa ya Onyango., Ila CHANZO Cha makosa ya Onyango au Simba kushambuliwa sana ni kukosa CDM.

YANI lango na KIPA WA Simba wanafikiwa kirahisi mno.
NGOMA sio CDM.
Vita Alikuwa no 10, Raja NK.
ELMERECK 8
Sio kweli..makosa ya onyango hususa ni kwenye Champions league ni makosa yake binafsi hayahusu timu, onyango hana speed na marking yake ni mbovu akikutana na striker mtundu lazima achomeshe timu. Simba katikati iko vizuri sana, falsafa yetu ni kushambulia. Na msimu huu tutapeleka moto sana, unapopelekewa moto hiyo akili ya wewe kushambulia utaitoa wapi? Derby ya simba na yanga sikuona yanga ikishambulia maana ilipelekewa moto 90 minutes mamaee
 
Habari ndugu ZANGU.
Mimi ni mdau WA soka.
Na mpenzi na mdau wa Simba.

Nimekuwa nikifuatilia usajili HASA WA wachezaji wa KIGENI ndani ya simba.

NIMEWEZA KUYAONA MAKOSA YAFUATAYO KIUFUNDI.

1. KOSA kubwa la Kwanza ni KUMUACHA Golikipa Beno kakolanya., Hivyo wanalazimika KUSAJILI Golikipa wa kigeni. Baada ya Manura KUUMIA. (Santos)
Hivyo kujinyima WiGo WA wachezaji wa ndani.

2. KOSA la pili Kukosa beki MBADALA WA KIGENI WA Che Malone na Inonga Incase Wana Kadi au WAKIUMIA.

Na hapohapo wamekosea MBADALA WA Mohamed Hussen.
YAHAYA mbegu ameng'ang'ania SINGIDA akiwa na GADIEL Michael ALIYE ondoka.

3 . KOSA KUBWA KABISA KABISA NI KUKOSA BACKBONE YA TIMU/ UTI WA MGONGO WA TIMU KIUNGO MKABAJI CDM 6
Tangu AMEONDOKA LWANGA , mkude, Nyoni na sawadogo hakuna MBADALA wao.

Japo Kunatetesi na Unafuu nasikia NGOMA amesaini Simba hii itakuwa nafuu Ila NGOMA ni 8.

4. KOSA LINGINE ni kujaza idadi kubwa ya Mawinga
I. Saido.
Ii. Onana.
Iii. kibu Denis
Iv. Sakho, Banda
V. Chama.
Vi Aubin Kramo.

5. KOSA LINGINE usajili WA mshambuliaji mmoja tu no 9. Jean Baleke.
Boko AMEISHA.
Ile Simba ya Makombe ilikuwa Kagere, Boko na mugalu saizi ni Baleke pekee

6 . Kidogo wamenifurahisha kwenye no 10.
Phili, Saido, chama.

MAKOSA NI MENGI MNO MUDA NI MCHACHE.
SIMBA NA ROBERTINHO REKEBISHENI HAPA.
USHAURI WA BURE. MSIJE MKAANZA LAWAMA.

NAFASI ,ZA KIGENI NI 12 TU.
NA ZIMEISHA.

Naomba Uzi Huu ujadiliwe na wanaojua mpira tu sio mashabiki Maandazi
Mtoa mada una leseni ya CAF au FIFA? kama huna kaa kimya.. hujui mpira.
 
Mtoa mada una leseni ya CAF au FIFA? kama huna kaa kimya.. hujui mpira.
Mtoa mada ni dish tena continental, anajifanya anaijua simba sana kumzidi robertinho perreila jinga moja tu huyu, alafu anakomaa eti nafasi za wageni zimeisha hajui kuwa thank you bado zinaendelea.
Kuhusu kakolanya alitaka kuondoka alitaka kuanza dhidi ya manula sasa je kakolanya ni bora kuliko manula??
Kuhusu namba 6 kanoute mbona yuko vizuri sana kuliko huyo tadeo lwanga, fabrice ngoma pia ni 6 box to box. Simba hatuitaji namba sita ya kizamani falsafa yetu ni kushambulia sio kujilinda ndiomaana winga zimeshuka kwa wingi yaani hutaki utapigwa usipotaka utapigwa tu.
Simba haina tatizo katikati ila ilikuwa na upungufu tu so tulichofanya ni kuongeza mbadala wa kanoute na mzamiru incase mmojawapo ni majeruhi au amechoka. Simba haijaruhusu magoli mengi kwenye ligi na hata cafcc.
 
Back
Top Bottom