Bado ni CHADEMA tuu.. CCM inazidi kufutika kwenye siasa za Tanganyika

Ila kwenye Dunia hii hakuna chama kitakaa kitokee chenye wahuni wazee kama chama dola walah tena!!.Yaani mazee maongo kuliko hata shetani.
 
Sasa nimeelewa kuwa unaweza kuwa unampangia adui yako mabaya yampate halafu wewe mwenyewe ukasahau kufunga mlango ndiyo yatakayoipata chama kikubwa mwaka huu. Watawala wametulia na wala hawahisi joto. Jambo la ajabu litatokea hawawezi kukiamini. Samahani hivi kule Misri siku chache kabla ya pigo la mwisho halijatokea, angekuja mtu kumwambia Farao kuwa baada ya siku chache wana wa Israel wataondoka angeamini? Wala asingeamini hata kidogo, lkn ndicho kilichotokea. Muda ni rafiki mzuri tuvute subira
 
Ila kwenye Dunia hii hakuna chama kitakaa kitokee chenye wahuni wazee kama chama dola walah tena!!.Yaani mazee maongo kuliko hata shetani.
tena!!.Yaani mazee maongo kuliko hata shetani.😂
 
 
CHADEMA, tusiingie kwenye mtego KUIPAISHA CHAUMA. TAARIFA za Kiintelijensia zinaonesha kwakushirikiana na MACCM na Intelligence zao, CHAUMA wamepandikiza watu watakao Fanya kazi ya kuhakikisha platforms zetu zinaongelea wao.

ADMINS, wachomoe wote wanaojadili hawa MACCM.

TUJIKITE kwenye maandalizi ya KWENDA Kwenye kesi ya Mwenyekiti wetu mh. Tundu A. M. Lissu 02/06/2025, MIKUTANO ya #NoReformsNoElection KANDA YA KASKAZINI na #ToneTone.
 
Baadhi ya watu waliotoka mikoani kuja Dar es salaam kuhudhuria Mkutano wa CHAUMMA wamelaumu kunyimwa posho walizoahidiwa baada ya kufika Dar es Salaam.

Mmojawapo anasema Wenje aliwatumia hela ya Kula kutoka Mwanza kuja kwenye Mkutano wa CHAUMMA lakini hawajapewa posho yao baada ya kufika Dar na ndiye aliratibu safari yao kufika huku.

Wamedai Wenje amekuwa anahudhuria vikao vyao vya kuwapanga huko Mwanza na tayari ameshajiondoa CHADEMA muda mrefu.

Wanadai pia Mbowe na Wenje wamekuwa wanafanya vikao kadhaa vya siri, na pesa iliyotengwa kwa ajili ya kufanikisha safari za wajumbe ni Tsh. Milioni 250.
 
Mimi nina hakika CCM hatuwezi kuhalalisha uchaguzi Mkuu kwa kutumia CHAUMA na ACT Wazalendo.

Jumuiya za ndani ya nchi na za kimataifa zinakitambua CHADEMA kuwa ndiyo Chama kikuu Cha upinzani.

Jumuiya hizo pia zinatambua kuwa taratibu za uchaguzi haziko sawa.

Ikumbukwe kuwa Magufuli,pamoja na ubabe wake,lakini alihakikisha Chadema kinashiriki uchaguzi Mkuu.Hii ni kwa sababu katika nchi yoyote jambo linaloangaliwa kwa unzito mkubwa na wananchi na Jumuiya za kimataifa ni uchaguzi Mkuu.

Tujiulize kama nchi tunaweza kumudu uchaguzi utakaogharimu fedha yote halafu ustambuliwe na Watanzania walio wengi na Jumuiya ya kimataifa.Ni sawa na kupanda shamba kubwa na usivune chochote.

Madhara yake ni kutengwa na Jumuiya ya kimataifa,kukosa uwekezaji,kukosa misaada na mikopo.Hatuwezi kumudu kujiendesha bila misaada au mikopo.
Mapato yetu bado yako chini mno.
 
CHADEMA WANAJITEKENYA WENYEWE ILI WAJICHEKESHE WENYEWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…