Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Kumbe humu pasi kutaja majina yako halisi na kadiri siku zinavyokwenda ipo siku unafunguka tuu, ahahahaaa...
johnthebaptist

Iringa hapo sokoni hawajambo ahahaaaa, namkumbuka konda flani niliwahi safiri naye miaka hiyo na Scand alikuwa mwenyeji wa Iringa, miaka ya majuzi nilikutana naye iringa anauza duka.
 
Inawezekana ushamba na uadimu wa huduma ndiyo unaokufanya mpaka Leo ukumbuke. Sasa hv huduma Bora zinapatikana popote ndiyo maana huoni Cha ziaida..if unataka scania tupu zipo sauli, Kilimanjaro na Arusha express. Mm sijaona utofauti wa kupanda scania na youtong labda uniambie utofauti wake nipate kung'amua.
 
Magari ya Sumaye hayo!! alipotoka nayo yakaishia kabisaaaaa!
 
Sababu ya kifo cha Scandinavian ni baada ya mmiliki kujiingiza kwenye siasa za kijinga huku akijua analo deni beki ya ADB, ADB walikuwa wanamdai yeye akachukua mabasi kuwapeleka bure wanaccm Rufiji kuzindua daraja la Mkapa, mabasi yaliporudi ADB ikakamata mabasi yote ya Scandinavian na kuyafungia kwenye yadi ya serikali Temeke kusubiri mnada, huo ndio ulikuwa mwisho wake.
Kilichomponza ni kudhani kuwa CCM itaiambia benki mwacheni huyu ni mwenzetu, lakini ADB haiko Tanzania hivyo haiwezi kujua kama ni mwenzao.
 
Sababu ya kifo cha Scandinavian ni baada ya mmiliki kujiingiza kwenye siasa za kijinga huku akijua analo deni beki ya ADB, ADB walikuwa wanamdai yeye akachukua mabasi kuwapeleka bure wanaccm Rufiji kuzindua daraja la Mkapa, mabasi yaliporudi ADB ikakamata mabasi yote ya Scandinavian na kuyafungia kwenye yadi ya serikali Temeke kusubiri mnada, huo ndio ulikuwa mwisho wake.
Kilichomponza ni kudhani kuwa CCM itaiambia benki mwacheni huyu ni mwenzetu, lakini ADB haiko Tanzania hivyo haiwezi kujua kama ni mwenzao.
Acha urongo wewe Mnyasa
 
Hoja Yao kubwa ni kuwa Scandinavian ni gari ya mzungu.
Huwezi mlinganisha ratco na scandinavia kwakuwa ratco ana route chache sidhani kama zinazidi mbili, ninayoifahamu ni Dar-TA tu
 
Kwa lipi? Je zilikuwa zinapaa? Au mwisho wa safari alikuwa anarudisha nauli? Kipi kilikuwa ni special ambacho mabus mengine hayakifanyi?
Scandinavia ulikuwa huwezi kuta abiria wamesimama au pale mbele kwa dereva ukute watu wamekaa, hakuna hiyo, kwasasa ratco na nacharo wanajitahidi tatizo wana route chache
 
Jamani Scandinavia iliuwa kampuni ya kipekee sana,mie sijawahi kwa ushamba wangu ila nilitamani sana kuyapanda japo siku moja,nakumbuka kipindi icho nipo Tanga,kuna mdada mmoja alipanda ilo basi kufika homu mtaa mzima ulijua na kumshangaa,yaani mtu amefika homu majirani kama wote kumuuliza safari ilikuwaje yaani alionekana kama mtu aliyetoka kupanda ndege,Alikuwa anasema Dar tumetoka saa 1 na kuingia Tanga saa 5 na nusu hapo tanga yenyewe ofisi zao zilikuwa mbali na stand kuu ya mabasi lakini walikuwa wanapata wateja,kuna sikumoja shuleni kuna jamaa mmoja nae alipanda ilo kesho yake jumatatu akaja hadi na tiketi yake basi shule nzima ilijua na kumshangaa kama mtu aliyepanda ndege,basi kila mtu alikuwa anataka ahadithiwe kuhusu Scandinavia ndani kulivyo hadi nje,wale jamaa walijua care ya usafiri kwa mteja sidhani kuna kampuni itaja kuweza huduma zao uko mbeleni,wale jamaa walikuwa na mabasi nchi nzima yanaondoka on time bila ya ubabaishaji,wewe umeona wapi mtu unaenda stand zao unakata tiketi unaambiwa safari ni saa mbili halafu inafika iyo saa 2 inakuwa kweli,ulikuwa ukiwa na mzigo wako kuna unawekwa label ya jina lako na sehemu unayoenda halafu mzigo wako wakishaupokea wewe huuoni tena ila wao wanaupakiwa kwa muda wao na ukifika mwisho wa safari mnakaa sehemu na kusubiria mzigo wako na unaukuta vilevile kama ulivyouweka
 
Zile ulizozitaja zoote nimezipanda shabiby ni loyal customer wao wa basi la mwisho kutoka Dar to Dom hivyo najua alipopungukiwa kumfikia scand, Darlux kabla ya hizi zilizomshinda akamuuzia klm alikuwa na zile polo original mbili(2) nazo nilizipanda japo kwa ule upungufu wao wa kuvuja kipindi cha mvua miaka hiyo akiwa na route ya Dar Mwanza. Hao abc ni uchafu usiomfikia hata shabiby
Hivyo ninapokubali ubora wa scand dhidi ya hao uliowataja na wengine ambao umewaruka, sio kwa sababu za kisiasa aka mihemuko ni kwa sababu ya kile alichokuwa anatupatia bila yeye kutuchoka hata tukiwa on board kwa masaa ishirini na zaidi
Sio jambo rahisi kwa hawa wasafirishaji wa leo mteja afanye booking ya mwezi mmoja mbele akubaliwe na siku ya safari akute nafasi ile aliyoomba bila kuletewa sarakasi ila kwa scand ilikuwa inawezekana
Asipoelewa hapa haelewi Tena,kulikua na coordination inayoeleweka sana unafanya booking kama ndege Tena miaka hiyo.
 
Niko darasa la 5 miaka hiyo,tulisafiri kifamilia kwenda Arusha,nakumbuka tulipandia kipata kariakoo. Scandinavia alikua ahead of his time. Hata akirudi now Kwa huduma zile zile Bado angekimbiza. Ila naskia alikua anapata hasara sana,anaweza akatoa gari hata ikiwa na abiria 10
 
Point kubwa niliyoielewa ulipenda hizo gari sababu ni Scania it's seems haupo interested na Brand nyinginezo lakini kuhusu huduma tuseme ukweli kampuni nyingi zinajitahidi kuwa royal Kwa customer wao ukizingatia time hii Kuna competition kubwa kwenye game la usafirishaji.
Swala si tu kuwa royal kwa customers. Scandinavia walijali hata emotions za watu wengine. Basi lilopata ajali au ubovu wowote likivutwa na breakdown,hufunikwa lote kwa turubai. Mabaki ya ajali huwa na mitazamo hasi.
 
Akikujibu pls tag me, na atoe facts sio blah blah, Scandinavian Express walikua na top class systems ya tickets, top class boarding lounge, ALWAYS ON TIME,they never ever cancel a trip, well serviced buses, well trained staff,no RUSH njiani,mkisimama sehemu ya mapumziko it's more than 30mins,ndani y bus ni smile tupu, binafsi nilipenda bcs always no 1
Kuna vibinti viwili nilivipitia miaka ya mwanzo ya 2000, vilikuwa pale KAMATA.
Pia DELUXE Coach kwa sisi wa Dom - Dar ilikuwa classic sana pia, japo hawakuwa na gari nyingi.
 
1. Scandinavia
2. Fresh ya Shamba
3. Dar Express
4. Zainab

Hawa ndio wakali wa hizi kazi wa muda wote...
Scandinavia na Zainab walikuwepo zamani, wakapotea then wakaja kwa nguvu kubwa na mwisho wakapotea mazima...
Mohamed Trans je!?
 
Back
Top Bottom