Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

That’s history. Hatuwezi kuibadilisha!

..tunaweza kubadilisha.

..hata majina ya mitaa mbalimbali ya Dsm yalibadilishwa baada ya uhuru.

..barabara ya uhuru nadhani wakati wa Muingereza ilijulikana kama Accacia street/avenue.
 
Mmenikumbusha ety wachagga walimpeleka Johannes Rebmann kwenda kuwa mtu wa kwanza duniani kuugundua Mlima Kilimanjaro 😂
Ni ujinga tu!! Na kwa mbwembwe mtu akiulizwa mvumbuzi wa kwanza wa mlima Kilimanjaro, anataja huyo mzungu!!! 😂😂😂 Utafikiri hao wachaga hawkuwa watu!!!
 
Sijui kwa nini huelewi! Miji yote mikubwa ilianza kama kijiji ambapo baadae ilibadilika hadhi na kuwa miji kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu! Mji haujengwi ghafla na kuwa mkubwa bila watu!
 
Wewe ndiye huelewi.

Hatusemi Sultani alianzisha kijiji cha Mzizima.

Tunasema Sultani alianzisha mji wa Dar es salaam.

Kama vile ambavyo hatusemi Alexander The Great alianzisha kijiji cha Rhacotis. Tunasema Alexander The Great alianzisha mji wa Alexandria, Misri.

Hivi umesoma na kuelewa kuwa kuna watu wali plan, wakajenga mji?

Sasa hapo huelewi nini?
 
Ni alama zipi au legacy gani muhumu Sultan aliyoacha kutoka mji unaodaiwa aliuanzisha?
 
Ni alama zipi au legacy gani muhumu Sultan aliyoacha kutoka mji unaodaiwa aliuanzisha?
Kwani akianzisha bila alama kubaki anakuwa hajaanzisha?

Nimekuambia hiyo Ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Sultani kama chuo cha Uislamu, hilo jengo limekuwa Ikulu miaka na miaka, hiyo si alama?
 
Kwani akianzisha bila alama kubaki anakuwa hajaanzisha?

Nimekuambia hiyo Ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Sultani kama chuo cha Uislamu, hilo jengo limekuwa Ikulu miaka na miaka, hiyo si alama?
Ikulu ya Dar es Salaam ilijengwa na Wajerumani kama ngome ya gavana.
 
Ikulu ya Dar es Salaam ilijengwa na Wajerumani kama ngome ya gavana.
Hapana mkuu, soma tena historia.

Wajerumani waliichukua tu kwa Sultani.

Ndiyo maana Ikulu ina Arabic architecture.

Na ukiingia ndani Ikulu Dar kuna sehemu mpaka leo kuna maandishi ya Kiarabu ya tangu enzi hizo.

Walioingia ndani Ikulu wanajua.
 
Hii hata mimi imenishangaza, hata hawezi kueleza economic objectives za kufanya hivyo

Hii nguvu ungetumia kuitaka Tanganyika ningemuelewa
 
Daru haimaanishi bandari!

Maana ya Daaru ni nyumba au mahali!

Waarabu walipaita Daaru ssalaam maana yake nyumba ya amani.
 
'Mzizima halikuwa jina la mwanzo hilo lilianzishwa na Waluguru (watembezi kwa kutumia miguu) kutoka Morogoro waliotumwa kuja kuvuna dawa ya mimiea kwenye kina cha bahari.

Waluguru walipofika hapo waliwakuta wandengereko, wamakonde na wakisi kama wataalamu wa mambo ya baharini. Ujio wao uliwafanya wenyeji wajiulize hawa watu wamekuja kweli kutafuta dawa au wana kitu kingine?

Hapo ndipo wakapewa jina la 'waza-ramo' wakalowea; kutokana na uongeaji wao na lafudhi murua wakawa wanawavutia watu wengi kwenda kuwasikiliza na kufanya nao biashara ya ushihiri eneo hilo pakachangamko ndipo likajitokeza jina la 'Mzizima'

Kuanzia maeneo ya Salenda, Upanga, Muhimbili, shuka kuelekea Kinondoni, Magomeni, Sinza, Mwananyamala, Kijitonyama, Mikocheni, Kawe, Mbezi beach, Tegeta (Tega sikio), Boko, Bunju (samaki mwenye sumu na haliki), Mabwepande, Madale, Makabe, Mbezi, Luguruni pote kulikuwa na msitu mnene huku wanyamaa kama simba, chui, nyati walikuwa wakitamba sana.
 
Naomba ujibu swali moja tu,bandari ilikuwa inatumika kusafirisha watumwa ?
 
Naomba ujibu swali moja tu,bandari ilikuwa inatumika kusafirisha watumwa ?
Bandari gani? Kwa nini swali hili ni muhimu katika mazungumzo ya nani kaanzisha mji wa Dar es salaam na si non sequitur logical fallacy tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…