Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

Jina la Dar es salaam tulishalikubali, tulikichukua na kulifanya letu, si la Sultani tena.

Ukishikilia kuwa ni la Sultani, wewe ndiye unampa Sultani umuhimu asiokuwa nao.

Pia, kihistoria Dar es salaam kama mji ni mji ulioanzishwa na Sultani. Hiyo ni historia ambayo haifutiki hata ukibadili jina.
Sultani alianzisha kivipi mji wa Dar es Salaam kwani hapo hapakuwa na wenyeji? Au ndiyo yale ya ziwa Victoria kuvumbuliwa na mzungu?
 
Mimi ni muumini wa historia na napenda sana majina ya sehemu yabaki kama yalivyokuwa ili tuweze kujua historia yetu. Hata mitaa ya Dar sidhani kama ilikuwa busara kubadilisha majina ya enzi zile. Nyumba pia walibomoa kwa makosa.
Mimi nitapenda Kijazi Interchange ibadilishwe kuwa Ubongo Interchange, Mfugale Flyover ibadilishwe kuwa Tazara flyover.
 
Sultani alianzisha kivipi mji wa Dar es Salaam kwani hapo hapakuwa na wenyeji? Au ndiyo yale ya ziwa Victoria kuvumbuliwa na mzungu?
Kulikuwa na kijiji cha wavuvi ndiyo hicho cha Mzizima.

Sultan Majjid ndiyo akaweka administration ya kwanza ya kujenga mji, akajenga majengo.

Kasome "Dar Es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis"

Kitabu naki attach hapa tukisome tuchambue mambo kisomi kwa taarifa sahihi.
 
Attachments

..tunaweza kubadilisha jina.

..Harare kabla ya uhuru wa Zimbabwe iliitwa Salisbury.

..Maputo kabla ya uhuru wa Msumbiji iliitwa Lourenco Marques.

..Na sisi tuna dhima ya kuondokana na Dar Es Salaam jina la kikoloni.
 
sehemu gani official inapaita hivyo
Ukiliacha kuna kosa gani? Ukitaka kubadilisha Jina kisa lilitokana na neno la kiarabu basi utabadilisha vitu vingi kuanzia mavazi ( tulikuwa tukitembea uchi kabla ya wakaloni), makazi ( tulikuwa tunaishi kwenye mapango na nyumba za tembe), chakula, lugha zote za kigeni, njia za mawasiliano kama gari, simu n.k.
Hao wakoloni ni wazuri kuliko wewe na mimi tunaochochea kupindisha sheria na taratibu ili mwenzio adhurike au akose haki zake.
 
Kulikuwa na kijiji cha wavuvi ndiyo hicho cha Mzizima.

Sultan Majjid ndiyo akaweka administration ya kwanza ya kujenga mji, akajenga majengo.

Kasome "Dar Es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis"

Kitabu naki attach hapa tukisome tuchambue mambo kisomi kwa taarifa sahihi.
Ndugu yangu, pamoja na maelezo yako na historia kuandikwa hivyo, Sultani alichofanya ni kuendeleza mji ambao tayari ulikuwepo (Mzizima) wala hakuanzisha mji mpya! Kwa sababu hakukuta pori pale!
 
Sultani alianzisha kivipi mji wa Dar es Salaam kwani hapo hapakuwa na wenyeji? Au ndiyo yale ya ziwa Victoria kuvumbuliwa na mzungu?
Kulikuwa na kijiji cha wavuvi ndiyo hicho cha Mzizima.

Sultan Majjid ndiyo akaweka administration ya kwanza ya kujenga mji, akajenga majengo.

Kasome "Dar Es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis"

Kitabu naki attach hapa tukisome tuchambue mambo kisomi kwa taarifa sahihi.
Mmenikumbusha ety wachagga walimpeleka Johannes Rebmann kwenda kuwa mtu wa kwanza duniani kuugundua Mlima Kilimanjaro 😂
 
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said, Jina hili linatokana na kiarabu lugha aliyotumia Sultan

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Dar es salaam ina maana ya Bandari Salama, kwa muda huo Sultan aliitumia bandari kufanya biashara ya kikatili ya kusafirisha babu zetu kwenda kutumikishwa kitumwa. Bandari aliyotumia haikuwa na bugudha, ilikuwa ni salama kwake na ilimtajirisha zaidi kupitia babu zetu.

Ni sawa na mbakaji anaeteka watoto wanaopita kwenye korongo, sehemu hio ikiwa ni salama kwake ataiita korongo salama, itashangaza sana baada ya mtu huyo kudhibitiwa watu waendelee kupaita korongo salama.

Kuita jiji hili kubwa kwa jina la Sultan kunaambatana na kumbukumbu za historia yetu chungu ya utumwa wa masultan waliokuwa vinara wa biashara ya utumwa, Babu zetu walipelekwa kulimishwa kimabavu mashamba ya Zanzibar, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao kama Marekani, utaowakuta ni waliohamia kuanzia miaka ya 70s

View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Mkuu, ila Jina Dar Es Salaam Mimi Huwa linanivutia kuliko Mzizima
 
..tunaweza kubadilisha jina.

..Harare kabla ya uhuru wa Zimbabwe iliitwa Salisbury.

..Maputo kabla ya uhuru wa Msumbiji iliitwa Lourenco Marques.

..Na sisi tuna dhima ya kuondokana na Dar Es Salaam jina la kikoloni.
Tumechelewa sana
 
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said, Jina hili linatokana na kiarabu lugha aliyotumia Sultan

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Dar es salaam ina maana ya Bandari Salama, kwa muda huo Sultan aliitumia bandari kufanya biashara ya kikatili ya kusafirisha babu zetu kwenda kutumikishwa kitumwa. Bandari aliyotumia haikuwa na bugudha, ilikuwa ni salama kwake na ilimtajirisha zaidi kupitia babu zetu.

Ni sawa na mbakaji anaeteka watoto wanaopita kwenye korongo, sehemu hio ikiwa ni salama kwake ataiita korongo salama, itashangaza sana baada ya mtu huyo kudhibitiwa watu waendelee kupaita korongo salama.

Kuita jiji hili kubwa kwa jina la Sultan kunaambatana na kumbukumbu za historia yetu chungu ya utumwa wa masultan waliokuwa vinara wa biashara ya utumwa, Babu zetu walipelekwa kulimishwa kimabavu mashamba ya Zanzibar, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao kama Marekani, utaowakuta ni waliohamia kuanzia miaka ya 70s

View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
That’s history. Hatuwezi kuibadilisha!
 
Kulikuwa na kijiji cha wavuvi ndiyo hicho cha Mzizima.

Sultan Majjid ndiyo akaweka administration ya kwanza ya kujenga mji, akajenga majengo.

Kasome "Dar Es Salaam. Histories from an Emerging African Metropolis"

Kitabu naki attach hapa tukisome tuchambue mambo kisomi kwa taarifa sahihi.
Majjid alikuwa mraibu wa dawa za kulevya na mfanyabiashara ya watumwa.
 
Ndugu yangu, pamoja na maelezo yako na historia kuandikwa hivyo, Sultani alichofanya ni kuendeleza mji ambao tayari ulikuwepo (Mzizima) wala hakuanzisha mji mpya! Kwa sababu hakukuta pori pale!
Hapana mkuu. Kuna tofauti kati ya mji na kijiji.

Tuangalie mfano wa mji wa Alexandria, Misri, mji ambao tunasema umeanzishwa na Alexander The Great.

Hapa nimeiuliza Meta AI (Llama)swali hili.

"Me:
What did Alexander the Great find in present day Alexandria before he built the city?

Meta AI:
When Alexander the Great arrived at the site of present-day Alexandria in 331 BCE, he found a small Egyptian fishing village called Rhacotis. The village was situated on a narrow strip of land between the Mediterranean Sea and Lake Mareotis.

According to historical accounts, including those by the ancient Greek historian Arrian, Alexander was impressed by the site's natural harbor, strategic location, and defensive potential. He envisioned a grand city that would serve as a center of Greek culture, trade, and power in the region.

Alexander's architects, including Dinocrates of Rhodes, designed the city, which was built on a grid plan. The city's construction began in 331 BCE, and it quickly grew into a thriving metropolis, becoming a major center of culture, learning, and commerce in the ancient world."
 
Back
Top Bottom