Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

Bandari gani? Kwa nini swali hili ni muhimu katika mazungumzo ya nani kaanzisha mji wa Dar es salaam na si non sequitur logical fallacy tu?
Dar es salaam (Bandari salama), Bandari aliyotumia Sultan Majid kufanya biashara zake,

bandari ilikuwa inatumika kusafirisha watumwa ?
 
Dar es salaam (Bandari salama), Bandari aliyotumia Sultan Majid kufanya biashara zake,

bandari ilikuwa inatumika kusafirisha watumwa ?
Kwanza kabisa jina Dar es Salaam halitokani na "Bandari Salama".

Mpaka hapo tu ushajionesha hujui historia.

Pili, hakuna mtu aliyesema Sultani Majjid hajafanya biashara zake.

Point yako nini hapa?
 
Kwanza kabisa jina Dar es Salaam halitokani na "Bandari Salama".

Mpaka hapo tu ushajionesha hujui historia.

Piki, hakuna mtu aliyesema Sultani Majjid hajafanya biashara zake.

Point yako nini hapa?
Sawa sawa, itakuwa Dar es salaam ina maana ya jiji la tende

nitaanzisha uzi husika
 
Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said, Jina hili linatokana na kiarabu lugha aliyotumia Sultan

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Dar es salaam ina maana ya Bandari Salama, kwa muda huo Sultan aliitumia bandari kufanya biashara ya kikatili ya kusafirisha babu zetu kwenda kutumikishwa kitumwa. Bandari aliyotumia haikuwa na bugudha, ilikuwa ni salama kwake na ilimtajirisha zaidi kupitia babu zetu.

Ni sawa na mbakaji anaeteka watoto wanaopita kwenye korongo, sehemu hio ikiwa ni salama kwake ataiita korongo salama, itashangaza sana baada ya mtu huyo kudhibitiwa watu waendelee kupaita korongo salama.

Kuita jiji hili kubwa kwa jina la Sultan kunaambatana na kumbukumbu za historia yetu chungu ya utumwa wa masultan waliokuwa vinara wa biashara ya utumwa, Babu zetu walipelekwa kulimishwa kimabavu mashamba ya Zanzibar, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao kama Marekani, utaowakuta ni waliohamia kuanzia miaka ya 70s

View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Utumwa utakuwa kichwani kwako vile unajiona mtumwa na utatenda sawa na watumwa mbele ya waarabu hadi leo.

Jina linabaki kama utambulisho wa mtu au mahali ili watu wapatofautishe na mahali pengine. Nani aliipa jina hiyo sehemu inabaki kuwa historia. Tulikuwa na stendi ya mkoani inaitwa Mbezi Luis sasa hivi ni Magufuli na watu wamekubali jina hilo kuwa ni kituo cha kukutania kwa safari au mambo mengine.

Ukiwa na akili ya kitumwa utawaza kila kitu kwa mtizamo wa kitumwa. Au maskini kwa mtizamo wa kimaskini. Badili mtizamo.

Mfano.

Bwagamoyo........ Bagamoyo.
Watumwa walibwaga mioyo yao wakiingia kwenye boti kwenda utumwani.

Saa Dani...... Saa ndani.
Mwarabu akiishi eneo ilipo hifadhi ya Saadani kwa sasa alikuwa akiwajibu watu wanaomuuliza ni muda gani sasa, yeye anajibu saa dani yaani saa ipo ndani.

Msasani .......... Musa Hasani
Eneo hili akiishi ndugu mmoja akiitwa Musa Hasani. Ndipo pakawa maarufu Msasani.

Mnyamani....... Mwinyi Amani
Soko la Buguruni Mnyamani likipewa jina la mtu maarufu hapo Mwinyi Amani.

Nhobora .......... Tabora
Hinyanga.......... Shinyanga
Ng'wanza ........ Mwanza
Geta ............ Geita
Gahama ....... Kahama
Idodomya...... Dodoma

Ukiangalia yote hayo majina ya upande wa kushoto ya asili yana maana, lakini yalikuja kubadilishwa na wageni kwasababu ya kushindwa kutamka kwa Lugha za wenyeji. Lakini vile wao ndio walikuwa watawala enzi hizo ilibidi vitabu viandikwe kwa kufuata maelekezo yao. Ni sawa na leo flyover ya Ubungo tunaiita Kijazi kwa kuwa watawala waliamua iwe hivo.

Futa utumwa kichwani ufurahie maisha.
 
Sultani alichukua eneo kimabavu hana hadhi yoyote ya kusifiwa kuanzisha mji, kwao alikotoka ni uarabuni.

Hao masultan wamechukua babu zako kuwauza sehemu nyingi duniani, Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa babu zetu waliopelekwa uarabuni walikatwa viungo vya uzazi ndio maana leo hii ni ngumu kukuta vizazi vya watumwa uarabuni
Tuwekee ushahidi wa haya uliyo yaandika.
 
Kwani akianzisha bila alama kubaki anakuwa hajaanzisha?

Nimekuambia hiyo Ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Sultani kama chuo cha Uislamu, hilo jengo limekuwa Ikulu miaka na miaka, hiyo si alama?
Screenshot_20250226-203928_Google.jpg
 
Tuwekee ushahidi wa haya uliyo yaandika.
watumwa waliopelekwa nchi za masultani walikatwa viungo vya uzazi, hawakuruhusiwa kuzaliana na kulikuwa na hofu wanaweza kuchanganya damu na mabinti wa huko.

jiulize kwanini ni nadra kukuta wajukuu wa watumwa waliotumikishwa uarabuni lakini nchi kama Marekani wapo.

1740591909705.png
 
Ukianzia historia ya Dar 1891 kuna miaka karibu 30 ushairuka hapo.

Sultan Majjid alinunua kipande hicho cja kutoka Magogoni mpaka Aga Khan kutoka kwa famikia ya Tambaza tangu alivyoingia huko 1860s.

Sasa Mjerumani kajenga vipi Ikulu hapo wakati hilo jengo la Ikulu lilikuwapo kabla Mjerumani hajafika hapo?
 
Ukianzia historia ya Dar 1891 kuna miaka karibu 30 ushairuka hapo.

Sultan Majjid alinunua kipande hicho cja kutoka Magogoni mpaka Aga Khan kutoka kwa famikia ya Tambaza tangu alivyoingia huko 1860s.

Sasa Mjerumani kajenga vipi Ikulu hapo wakati hilo jengo la Ikulu lilikuwapo kabla Mjerumani hajafika hapo?
Hili jengo la sasa la Ikulu inasemwa lilijengwa na British architect John Sinclair baada ya ngome ya Mjerumani kuharibiwa.
 
Back
Top Bottom