Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said, Jina hili linatokana na kiarabu lugha aliyotumia Sultan
Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."
Dar es salaam ina maana ya Bandari Salama, kwa muda huo Sultan aliitumia bandari kufanya biashara ya kikatili ya kusafirisha babu zetu kwenda kutumikishwa kitumwa. Bandari aliyotumia haikuwa na bugudha, ilikuwa ni salama kwake na ilimtajirisha zaidi kupitia babu zetu.
Ni sawa na mbakaji anaeteka watoto wanaopita kwenye korongo, sehemu hio ikiwa ni salama kwake ataiita korongo salama, itashangaza sana baada ya mtu huyo kudhibitiwa watu waendelee kupaita korongo salama.
Kuita jiji hili kubwa kwa jina la Sultan kunaambatana na kumbukumbu za historia yetu chungu ya utumwa wa masultan waliokuwa vinara wa biashara ya utumwa, Babu zetu walipelekwa kulimishwa kimabavu mashamba ya Zanzibar, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao kama Marekani, utaowakuta ni waliohamia kuanzia miaka ya 70s
View attachment 3250594
Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA