Bado tupo utumwani? kwanini tunasita kubadili jina la jiji kubwa zaidi Afrika mashariki

Unaweza ukarudia kuiweka hapa👇

Offside

Unasema tumpuuze mleta mada sio Mtanzania? Unasema na mm Nkaburu wa Zabanga, sio Mtanzania?

sasa haya aliyoleta mleta mada yametoka wapi kama sio kwa Watanzania/Mtanzania?

...

Kama confusion ya Gulf Of Mexico?

Muulize aliyeleta mada anajibu ase.

Hata hivyo kuna kitu hakipo sawa mpaka hapa Uzi ulipofika.

Usiku mwema mkulu, nimepata majibu niliyokuwa natafuta. ASANTE🙏
Mkuu,

Nimekuuliza swali hujalijibu umelibrush off tu bila kulijibu. Sijui hata kama umwlielewa na umeelewa umuhimu wake kimantiki.

Kwani tukisema huyu rais kachaguliwa na Watanzania, huyo rais inakuwa lazima awe kachaguliwa na Watanzania wote?

Kwani haiwezekani Watanzania wengi wakamchagua rais, akawa kakubalika na Watanzania wengi na hivyo kiujumla akakubalika ndiye rais halali wa Tanzania, wakati hajachaguliwa na Watanzania wote?

Kukiwa na Watanzania 100 JF wanataka kubadili jina la Dar es salaam, halafu hao wengine wote zaidi ya milioni 65 hawajali hilo jambo, hapo mtu akisema Watanzania hawajali hili jambo utakataa kwa sababu kuna 100 wanajali?

Kwani kusema Watanzania hawajali ni lazima wasijali wote?

Tukisema Watanzania wamemchagua mtu kuwa rais ni lazima awe amechaguliwa na Watanzania wote?
 
..hata kuondoa kumbukumbu za utumwa na ukoloni inaweza kuwa moja ya sababu za msingi za kubadilisha jina la Dsm.

..kama ilikuwa sahihi kwa Sultani kubadilisha jina la asili na kuita eneo hilo Dsm basi haitakuwa makosa na sisi kama taifa huru kubadilisha jina hilo.
Hutakiwi kuondoa kumbukumbu za utumwa na ukoloni.

Unatakiwa kujenga makumbusho, kuandika vitabu, kumbukumbu zisipotee.
 
Itabidi tuanze kubadili vitu vyote vyenye majina ya kikoloni na alama za kikoloni,pamoja na na yale majina yalikosewa kutamka halafu yabaki kutamkwa kwa lugha ya kikoloni
 
Hakuna kitu kibaya kama kushindwa kumove on. Vinginevyo utakuwa kama yule Mzee wa story za Wazee Wa Kariakoo walimpokea Nyerere.

Wazee hivi, Wazee that.
 
Acha pumba.

Dar es Salaama ni jina la kawaida ambalo halina link na jina la mtu au sehemu nyingine. Majina yaliyobaidlishwa majina kama Salisbury na Leopordville ni kwa vile yalikuwa ni majina ya miji ya ulaya au ya watawala wa ulaya.
 
Tukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?

Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam, sehemu ambazo babu zetu walifikia wamechapwa sana mijeredi, wamelimishwa sana mashambani, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao, utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s
View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Wewe unashangaa hilo jina la zamani mbona poa tu? Historia na tafsiri yake bado ni nzuri sana, shangaa bakita walikaa miaka ya karibu katika kutafuta kiswahili cha neno live wakachukua moja kwa moja kwenye kiarabu eti mubashara, puuzi kabisa. Yaani hawakufikiria hata kidogo
 
Hutakiwi kuondoa kumbukumbu za utumwa na ukoloni.

Unatakiwa kujenga makumbusho, kuandika vitabu, kumbukumbu zisipotee.

..nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.

..hata kama tutabadili jina la jiji la Dsm bado jina hilo litabakia ktk vitabu vya historia na kumbukumbu nyingine.
 
Wala hakuna sababu ya maana ya kubadili jina la Dar es salaam.

It's just an overly woke Quixotic pursuit for unattainable purity using misguided identity politics.
 
..hata kuondoa kumbukumbu za utumwa na ukoloni inaweza kuwa moja ya sababu za msingi za kubadilisha jina la Dsm.

..kama ilikuwa sahihi kwa Sultani kubadilisha jina la asili na kuita eneo hilo Dsm basi haitakuwa makosa na sisi kama taifa huru kubadilisha jina hilo.
Ni zoezi lisilokuwa na tija yoyote na kuna unafiki ndani yake! Vinginevyo, hata watu basi acheni kutumia majina ya wakoloni, slave masters! Majina kama vile Joseph, John, Peter, Mohamed, Omar, Hassan, etc hayana tofauti na jina “Dar es Salaam”. Yote ni legacy ya colonial and slave masters! Hata kitendo cha kuadhimisha siku ya uhuru ni kukiri kwamba we once were under colonial rule. Kwanini basi tusiache kuadhimisha hiyo siku?
 
Tukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?

Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam, sehemu ambazo babu zetu walifikia wamechapwa sana mijeredi, wamelimishwa sana mashambani, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao, utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s

View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Kuna Dar es Laaam
Kuna Zanzibar

Kwa nchi iliyoendelea na kua huru na kwa watu ambao hawana inferiority Ilitakiwa harakati zianze siku nyingi.
Tatizo tunaongozwa na watumwa wa kifikra pia walioaminishwa na dini kua waarabu walikua sahihi kututumikisha
 
Tukiangalia majina karibia yote ya mikoa yana asili ya hapa kwetu iweje jiji kubwa nchini na Africa Mashariki tubaki kungangania jina la kikoloni lenye historia ya kitumwa ?

Jina la jiji kubwa zaidi Afrika Mashariki "Dar Es Salaam" lilipewa na Sultani Majid bin Said

Kabla ya hapo, eneo hilo lilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi kilichoitwa Mzizima, neno lenye maana ya "mji wenye afya."

Sultani Majid alikuwa akifanya biashara ya kikatili ya utumwa iliyomtajirisha, Bandari aliyotumia aliisifia kwa kuiita Dar Es Salaam, kwa tafsiri ya kiswahili ni bandari salama, alisafirisha babu na bibi bila bugudha ndio maana akapaita Dar Es salaam, sehemu ambazo babu zetu walifikia wamechapwa sana mijeredi, wamelimishwa sana mashambani, walioenda nchi walizotokea masultan hali ilikuwa mbaya walikatwa viungo vya uzazi ndio maana ni ngumu kukuta wajukuu zao, utaowakuta ni waafrika waliohamia kuanzia miaka ya 70s

View attachment 3250594

Itapendeza zaidi paitwe MZIZIMA
Akili za kilofa kama hizi, sishangai akina Lissu nao wana wafuasi na watu wanawaamini.
 
Hizi pia zinaweza kutumiwa kama hoja za kuwaondoa watu kwenye kudai mambo ya msingi.
Umeona eeh ... Shielding propaganda.
Angalia sa hivi wanavombrand chura kiziwi! Picha yake ipo kwenye kila material hadi pichu!
Mara goli la mama
Cheka na mama
Show ya mama
Siku ya wanawake duniani ya mama
Ambulance ya mama
Msikiti wa mama,
Uwanja wa mama,
Gesi ya mama
Mtungi wa mama

Na vituko vinginevyo sawa na hivyo!
Lengo ni kuwa shield wananchi wasijadili masuala nyeti kwa mustakabali wa nchi yao!
 
Watu wanakula mlo mmoja kwa siku halafu analeta habari za kubadili jina la Dar es salaam?
Hii ni hoja dhaifu sana,
Kubadili jina la Dar hakuwezi kutumia hata 10% ya gharama za kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma.
 
Gharama ya kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma ni kiasi gani kwanza?
 
Mkuu,

Nimekuuliza swali hujalijibu umelibrush off tu bila kulijibu. Sijui hata kama umwlielewa na umeelewa umuhimu wake kimantiki.

Kwani tukisema huyu rais kachaguliwa na Watanzania, huyo rais inakuwa lazima awe kachaguliwa na Watanzania wote?

Kwani haiwezekani Watanzania wengi wakamchagua rais, akawa kakubalika na Watanzania wengi na hivyo kiujumla akakubalika ndiye rais halali wa Tanzania, wakati hajachaguliwa na Watanzania wote?

Kukiwa na Watanzania 100 JF wanataka kubadili jina la Dar es salaam, halafu hao wengine wote zaidi ya milioni 65 hawajali hilo jambo, hapo mtu akisema Watanzania hawajali hili jambo utakataa kwa sababu kuna 100 wanajali?

Kwani kusema Watanzania hawajali ni lazima wasijali wote?

Tukisema Watanzania wamemchagua mtu kuwa rais ni lazima awe amechaguliwa na Watanzania wote?
Inasemekana mwaka 1992 asilimia 80 ya Watanzania walikuwa hawataki vyama vingi, ajabu ni katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 upinzani ulipata 40% ya kura, tena chini ya tume inayosimamiwa na chama tawala.
 
Back
Top Bottom