Bajaji aliyoacha marehemu mama imeanza kunigombanisha na baba yangu mzazi pamoja na dada yangu tumbo moja nifanyeje?

Taa hukaa gizani ili iyangaze mwanga katika giza, sasa taa ikienda penye mwanga itakuwa na faida gani, baki
 
Wewe ni taahira! Unaafahamu kwamba mali zote alizoacha Mama yako ni za Baba yako, kisheria?
 
Ila hakuna bajaj inaweza kutumia battery ya N50 hiyo ni kubwa sana hata N40 bado ni kubwa. Angalia usije ukawa umepigwa
Unamaanisha Voltage? Kama ni 12V kwaniji isitumie? Kama ni kile kisehemu cha kufunga unaweza mofify. N50 ina maanisha kiwango cha storage, na sio rate of charge release..
 
Chunguza kwa umakini ukute huyo hakuwa mama yako mzazi.
 
Hiyo ni bajaji au kisukure? Yaani imekaa 10 years ikiwa imepaki na bado familia zinagongana πŸ™„πŸ™„ bora ujipange kivyako.
 
Naona una akili kiasi, una argue logically, ingawa una maamuzi ya haraka na unapaniki haraka ndo maan ulikimbilia humu kutafuta msaada wa mawazo. Mimi km mkubwa wako au mzazi nikuambie tu kuwa humu kuna watu wa kila karba na akili tofauti na miluzi mingi humpoteza mbwa.

Nilikwambia toka jana kuwa ulikisea sana kufufua hiyo bajaji bila kushirikisha familia (baba, dada yako na wadogo zako, ingawa sijui umri wao). Kwa hiyo km msomi na kwa kutumia busara kaa na hiyo familia yako waombe radhi na muyajenge upya. Waeleze nia na kusudio lako kuwa halikuwa kwa nia mbaya, hivyo waombe uendelee pale ulipoishia. Hakika watakuelewa km unawaza mikakati mizuri yenye faida kwako na kwako. Hapo usioneshe ubinafsi.

Wengine wanakuambia achana na mali za familia, ondoka katafute zako. Kiasi flani wako sahihi lakini kiasi kikibwa wanakudanganya. Kwenu ni kwenu tu na jana nilikwambia "running away from a problem is not a way of solving it". Labda kwa vile haujasema wewe ni wa kiume wa kwanza au wapo wakubwa zako. Maan wa Kwanza kwa baadhi ya familia ndo huwa "think tank" ktk familia na ndo hubeba msalaba wa familia. Nina mengi ya kukuambia ila km hunielewi kwa haya machache basi hata hayo mengi ndo huwezi kunielwa kabisa.

Weka elimu yako pembeni, acha dharau kwa baba yako na dada yako utafanikiwa. Hata ukiondoka, mafanikio yasiyokuwa na baraka za wazazi ni sawa na utajiri wa FREEMASONI au WAGANGA WA KIENYEJI tu muda wowote utakumbwa na matatizo utafilisika na utaanza kukumbuka kwenu.

NANDOKITITA, nimemaliza
 

Si ununue ya kwako uachane na hayo madhila? Unalialia kama vile umeibiwa
 
Bajaji ni mali ya Mzee, muache afaidike nayo.
La sivyo, ungeinunua kama ilivyo na kuitengeneza au mngeingia mkataba kabla ya kuitengeneza.
Mwingine ni ubinafsi tu sasa bajaji imekaa miaka kumi imepaki mzee alikua ananufaika nayo vipi
 
Hatuingilii ugomvi wa ndugu!
 
Mwingine ni ubinafsi tu sasa bajaji imekaa miaka kumi imepaki mzee alikua ananufaika nayo vipi
Tatizo hapo ni kudhani mali za wazazi ni zako. Unakarabati nyumba, kesho unamuona Mzee anamzungusha mwarabu kumuonyesha nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…