Naona una akili kiasi, una argue logically, ingawa una maamuzi ya haraka na unapaniki haraka ndo maan ulikimbilia humu kutafuta msaada wa mawazo. Mimi km mkubwa wako au mzazi nikuambie tu kuwa humu kuna watu wa kila karba na akili tofauti na miluzi mingi humpoteza mbwa.
Nilikwambia toka jana kuwa ulikisea sana kufufua hiyo bajaji bila kushirikisha familia (baba, dada yako na wadogo zako, ingawa sijui umri wao). Kwa hiyo km msomi na kwa kutumia busara kaa na hiyo familia yako waombe radhi na muyajenge upya. Waeleze nia na kusudio lako kuwa halikuwa kwa nia mbaya, hivyo waombe uendelee pale ulipoishia. Hakika watakuelewa km unawaza mikakati mizuri yenye faida kwako na kwako. Hapo usioneshe ubinafsi.
Wengine wanakuambia achana na mali za familia, ondoka katafute zako. Kiasi flani wako sahihi lakini kiasi kikibwa wanakudanganya. Kwenu ni kwenu tu na jana nilikwambia "running away from a problem is not a of solving it". Labda kwa vile haujasema wewe ni wa kiume wa kwanza au wapo wakubwa zako. Maan wa Kwanza kwa baadhi ya familia ndo huwa "think tank" ktk familia na ndo hubeba msalaba wa familia. Nina mengi ya kukuambia ila km hunielewi kwa haya machache basi hata hayo mengi ndo huwezi kunielwa kabisa.
Weka elimu yako pembeni, acha dharau kwa baba yako na dada yako utafanikiwa. Hata ukiondoka, mafanikio yasiyokuwa na baraka za wazazi ni sawa na utajiri wa FREEMASONI au WAGANGA WA KIENYEJI tu muda wowote utakumbwa na matatizo utafilisika na utaanza kukumbuka kwenu.
NANDOKITITA, nimemaliza