Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2023/24 kugharimu Tsh. Trilioni 44.39

Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2023/24 kugharimu Tsh. Trilioni 44.39

Fuatilia Mjadala wa Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2023/24, leo Juni 15, 2023 itakayosomwa Bungeni na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba.



Mwigulu: Kiwango cha ukuaji wa pato la Taifa Mwaka 2022 kilifikia 4.7%
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mwaka 2022, thamani halisi ya Pato la Taifa kwa bei za mwaka 2015 lilifikia Tsh. Trilioni 141.9 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 135.5 mwaka 2021.

Amesema pia kiwango halisi cha ukuaji wa pato la Taifa kilifikia 4.7% Mwaka 2022 ikilinganishwa na 4.9% Mwaka 2021, wakati huohuo Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji kwa mwaka 2022 ni; sanaa na burudani (19.0%), madini (10.9%), fedha na bima (9.2%), malazi na huduma ya chakula (9%), na umeme (7.6%).

Aidha, thamani ya Pato ghafi la Taifa linatarajiwa kufikia dola za Marekani Bilioni 85.42 mwaka 2023/24.

===

UWASILISHWAJI WA BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/24

View attachment 2658579

Bajeti hii imeandaliwa ka kuzingatia nyaraka mbalimbali za kimataifa, pia kwa kuzingatia ilani ya CCM, dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na ile ya Afrika Mashariki, hotuba za Rais na Makubaliano mengine ya kikanda ambayo Tanzania imeridhia na itasomwa kwa kufuata Ibara ya 137 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uchumi wa Tanzania unatarajwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.4 kwa Mwaka 2023 kutoka Dola Bilioni 69.9 kwa Mwaka 2021.

Tanzania imepanda hadi nafasi ya 6 kiuchumi kwa nchi zinazopatikana kusini mwa jangwa la Sahara. Nchi ambazo zipo chini ya Tanzania ni Ghana, Ivory Coast, DRC na uganda.

Matokeo ya tathimini ya kukopesheka, Tanzania imepewa madaraja yanayoonesha taswira chanya kimataifa, Tanzania ikiwa juu likiko nchi zote kwenye ukanda wa Afrika Mashariki. Mojawapo ya mambo yaliyofanikisha haya ni kuwepo wa maridhiano ya kifaita.

Sekta ya Kilimo
Serikali itaendelea kuongeza bajeti ili kuongeza tija kwenye sekta hii, kuongeza pato la taifa pamoja na kuinua uchumi wa wakulima.

Kwa mwaka wa fedha 2021/22 bajeti ilikuwa bilioni 294, mwaka 2022/23 ilikuwa bilioni 954 na sasa inaweza kufikia bilioni 970.

Katika kumarisha sekta ya kilimo, Serikali itaendelea kuongeza fedha kwenye sekta hiyo kadiri ufanisi utakavyoongezeka, hatua hi inaweza kuongeza fedha zaidi kwenye ya miradi ya Kilimo na kufika Tsh. Trilioni 1.27 katika Mwaka wa Fedha, tunataka kupiga vita kwa vitendo.

Sekta ya Elimu
Waziri wa fedha amependekeza kuondolewa kwa ada kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha 4 na kupangiwa shule za ufundi za DIT, MUST na ATC ili kuongeza ujuzi na wataalam kwenye kipindi hili cha mpinduzi makubwa ya Teknolojia.

Kuanzisha program za kutoa mkopo kwa wanafunzi wa kozi zenye uhitaji maalum kuanzia mwaka huu 2023/24.

Kuongezeka kwa boom kutoka Tsh. 8500 hadi 10000/=

Sekta ya Afya
Serikali italipa madeni ya NHIF ili kuboresha huduma zake na itatoa pesa kwa MSD ili ijiendeshe kiufanisi tofauti na jinsi ilivyo sasa.

Utalii
Kupitia Royal Tour aliyofanya Rais Samia, idadi ya watalii wanaokuja nchini iliongezeka sana hadi kufikia 1,154,920 kwa mwaka 2022.

Kero za Muungano
Hoja 4 zinazohusisha muungano zimepatiwa ufumbuzi kwenye mwaka wa fedha unaoisha.
Je Mauzo ya bandari yamezingatiwa humo
 
Magufuli naye yumo kwenye kundi moja na wahujumu wa taifa letu
Naona wabunge wanashangilia na kugonga meza, mbona Mimi sioni lolote la maana?

Hawa ndio Wabunge aliowataka Magufuli kazi yao kugonga meza tu pumbaaavu.
 
Mwigulu hawezi kuongea hata kidogo, jinsi anavyo wasilisha hiyo Bajeti hadi unashangaa PhD ipi aliyonayo yeye.

Mda wote anamtaja rais samia, inafika hatua anasahau hadi jinsi ya kutamka maneno sahihi, afu anaongea kwa kujistukia na kusifia tena kwa kukazia, na mda wote anababaikaa tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kazi ipoo hapa kwa kweli.
 
Mwigulu hawezi kuongea hata kidogo, jinsi anavyo wasilisha hiyo Bajeti hadi unashangaa PhD ipi aliyonayo yeye.

Mda wote anamtaja rais samia, inafika hatua anasahau hadi jinsi ya kutamka maneno sahihi, afu anaongea kwa kujistukia na kusifia tena kwa kukazia, na mda wote anababaikaa tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kazi ipoo hapa kwa kweli.
Lile jamaa ni lisenge la grade A
 
Ninaangalia Mawaziri wa fedha hata wa Nchi Wafadhili , sijawahi kuona mbwembwe za kishamba kama anazofanya Mwigulu anapoingia Bungeni kuwasilisha Bajeti ya serikali masikini ya Tanzania , hivi sababu ya mambo haya ya gharama kubwa ni nini hasa ?

Kwa mbwembwe hizi anazofanya Mwigulu Bungeni , nina hakika akiondolewa kwenye Wizara ya fedha ni lazima ajinyonge , Wallah tena ! hata Rais hajawahi kufanya kama anavyofanya huyu jamaa !

Hii ni Aibu ? Akemewe .

Mbona akina Dr Mpango na wengine hawakufanya hivi ?
 
Kuna kitabu kimoja kinaitwa"Afrika inakwenda Kombo" kinaelezea kwa upana tabia za viongozi wa nchi za bara la Afrika kama hizi.
Screenshot_20230615-175557~2.png
 
Ninaangalia Mawaziri wa fedha hata wa Nchi Wafadhili , sijawahi kuona mbwembwe za kishamba kama anazofanya Mwigulu anapoingia Bungeni kuwasilisha Bajeti ya serikali masikini ya Tanxania , hivi sababu ya mambo haya ya gharama kubwa ni nini hasa...
Umeelezea as if wote humu tunamjua huyo unaemuita mchemba
 
Anaanza kuuzoea urais ili ikifika 2030 visiwe vitu vigeni kwake
 
Back
Top Bottom