Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

...Realstick. Pongezi....
 
Shilingi ya kitanzania 5,000.
Tuko watano, watoto wawili, watu wazima watatu.
Umeme, king'amuzi, unga, mchele, maharage, sabuni, n.k pembeni
...Realstick. Pongezi Mkuu Nunio...
 
...Pongezi...
 

Punguza soda hizo mkuu bora unywe maji nimempoteza mtu wangu wa karibu kisa sukari,,,
 
Naona unatafuta kisukari kwa nguvu zote.
 
Nyumbani(Wife & Junior) 10,000/=

Mimi 3500/= kwa ajili ya nauli(kwenda kijiweni na kurudi nyumbani) na maji.

Mengineyo inategemeana na hitaji litakalojitokeza.

Bando ni 2000/= kwa wiki ila huwa linaisha kwa siku 5 au chini ya hapo.
 
kuna sku,nmechukua 10k,nmeenda sokoni imeishia kwenye mboga tu na viungo,mpka leo najiulizaga inakuwaje wife ukimpa hata 10k anapika mpka usku

Wanawake wanajitahidi mno vitu vimepanda mno bei sasa hivi mchele mzuri kilo moja 3000,nyama 8000 ,samaki mzurii sangara 15,000 ,kuku mzuri 25000 wa kienyeji
Siku zingine mtakula maharage
 
Niseme tu ukweli.
Bajeti yangu kwa kila siku haivuki elfu 3000 maxumum, minimum 1,500.

nikishasaga unga kitini cha elfu 5 kinakaa siku 4, mimi n.mke wangu tunakula tu hamna shida.

Maisha bado hayaeleweki mwaka wa saba huu sina ajira yoyote, nimesaka ajira hadi najishangaa nina nuksi gani mimi

Hapa napambana kulipa kodi miezi mitatu mambo ni moto.

Nashukuru tu naishi Mwanza karibu na kijijini kwetu, mambo yakinikaba sana narudi kijijini kulima hakuna namna
 
Kwa hali ilivyo sasa hivi bajeti haieleweki kabisa inabadilika badilika sana kwa sababu hata kipato nacho kinabadilika badilika labda nyie wenzetu mnaolipwa mishahara ila kina sisi waganga njaa ni hatari zaidi siku unapokuwa huna kakibarua aisee
 
Wanawake wanajitahidi mno vitu vimepanda mno bei sasa hivi mchele mzuri kilo moja 3000,nyama 8000 ,samaki mzurii sangara 15,000 ,kuku mzuri 25000 wa kienyeji
Siku zingine mtakula maharage
Mchele 1kg @ 3,000 sawa
Nyama 1kg @ 8,000 sawa
Samaki 1pc @ 15,000 sawa
Kuku 1 @ 25,000 Hapa itakuwa wa kienyeji mmoja na wa kisasa mmoja.

Siku kukiliwa ndondo, mboga za majanj, ubwabwa, ugali; gesi, mkaa, maji, chumvi, n.k viko ndani, 5,000 haitoshi vipi?

Na kama wote tunatoka asubuhi kwenda kutafuta, weka 5k ubaoni, naweka 5k ubaoni, ishakywa 10k hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…