Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

Watu wawili ,
Nanunua vitu vingi vya mwezi ,mchele,unga,sukari,mafuta,mayai,maziwa,samaki,kuku,nyama,dagaa,soseji,tambi,viungo vya kupikia,mboga za majan buku kila siku,soda nanunua chache za mtoto maana najijua ,matunda
Vingine kama maharage na ndegu,choroko napika napaki naweka kwa friji,
Bado king’amuzi ,umeme,maji ,vocha ,kufuliwa,usafi tunafanya wenyewe
bado hatujala chips vumbi na mishikaki au kutoka tu
Mim huwa nna shida mmoja nikienda mjini lazima ninunue vikorokoro tu vinanimaliziaga hela [emoji23][emoji23]
Wanawake tuna vitu vingi mno tunapenda kununua hasa vya ndani urembo,hapo bado lotion za kupaka,perfume,dawa za mbu,sabuni za vyoon
Kwa siku siwez jua natumia ngapi maana kila kitu kinakuwa ndani vile vya muhimu
 
Niseme tu ukweli.
Bajeti yangu kwa kila siku haivuki elfu 3000 maxumum, minimum 1,500.

nikishasaga unga kitini cha elfu 5 kinakaa siku 4, mimi n.mke wangu tunakula tu hamna shida.

Maisha bado hayaeleweki mwaka wa saba huu sina ajira yoyote, nimesaka ajira hadi najishangaa nina nuksi gani mimi

Hapa napambana kulipa kodi miezi mitatu mambo ni moto.

Nashukuru tu naishi Mwanza karibu na kijijini kwetu, mambo yakinikaba sana narudi kijijini kulima hakuna namna

Mim nakoboa unga 15,000 nachanganya na kisado cha muhogo nakula miezi miwili maana sipendi ugali kiukweli kila siku,wanaomaliza ni wageni [emoji23][emoji23]
Mchele 25 kg miez miwili,nikienda mirongo nyanya ,vitunguu ,viungo bei ndogo tu vingiii kweli maisha yanasonga
Pole sana ajira ni tatizo la taifa utapata tu siku moja
 
Tsh 10,000/= Ila vitu vya msingi vyote viwepo,mchele,unga,maharage makande nyanya vitunguu carrot nk .

Kama una uwezo unachukua nyama 2Kg na samaki wa 20K unaweka kwenye friji unaacha wanajipangia wenyewe kwa bajet, kama unaishi mjini kununua ndizi za kutosha familia ni anasa siku wakipika ndizi wamix na wali siku zisogee.
Maisha ya bongo movie
 
Huuu ni uongoo bana ,uongooooooooo[emoji848][emoji848][emoji848]

Kuna familia zinatumia zaidi ya hiyo mkuu nishaenda kwa ndugu zangu hawamcheshi maji wananunua ya dukani na familia ni kubwa ,kuna chumba ukiingia matikiti yamejaa utafikiri yanauzwa,
Kuna watu wana hela wee
 
Ila jamen mnaacha 5000 au mi sijaelewa atanunua nin mboga zilivyo na beii hao,5000 tu ni ya maziwa nyie watu ongezeni kuacha hela home acheni ubahili vitu vilivyopanda bei hivyo
Matajiri wa jf jamani cx Evelyn Salt
Nitakuwa nakupa 7000

Unapenda maziwa kama paka
 
Nitakuwa nakupa 7000

Unapenda maziwa kama paka
Maziwa,mayai yanatakiwa yawepo kuna hata hunywi maziwa kila siku sababu yananenepesha ,ni unaweka kwa maharage,kztengeneza custard,keki, kupikua chapati
 
mim nashinda hasa vijiweni kwaiyo siku nzima uwa nakula kwa kudanda danda kijiwen, Asubuhi kabisa ya saamoja uji kombe la 500, ifikapo njaa mida ya saatatu ndizi jero, mshkaki jero na Coca-Cola bariid ya 600, apo inakatika 1600, mchana wali 1500 na Coca-Cola bariid 600 inakuwa 2100, next Azam energy bariid 600, jion ya saamoja kikombe kimoja cha Alkasusu 500 kwaiyo apo inakatika kama 5,800 lakin sometimes uwa nabadirisha inafika ad 10k
Una ulaji mbovu mkuu,hayo masoda na Energy unayokunywa hovyo yana madhara mwilini mwako.
 
Kwa hiyo unapoagiza gari, iPhone, nguo, saa etc ulaya au asia hujiulizi hiyo kama ni mental slavery?

Ponda mali maisha ya leo siyo ya jana
 
Back
Top Bottom