Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

mim nashinda hasa vijiweni kwaiyo siku nzima uwa nakula kwa kudanda danda kijiwen, Asubuhi kabisa ya saamoja uji kombe la 500, ifikapo njaa mida ya saatatu ndizi jero, mshkaki jero na Coca-Cola bariid ya 600, apo inakatika 1600, mchana wali 1500 na Coca-Cola bariid 600 inakuwa 2100, next Azam energy bariid 600, jion ya saamoja kikombe kimoja cha Alkasusu 500 kwaiyo apo inakatika kama 5,800 lakin sometimes uwa nabadirisha inafika ad 10k
Kwa ulaji huu ukifika 45 yrs huna sukari ama pressure basi ukatoe sadaka kubwa sana.
 
Tushirikishane bajeti yako hasa nyakati hizi ambazo bidhaa muhimu kama nafaka zilivyopanda bei. Je, wewe kwenye familia yako bajeti kwa siku ni shilingi ngapi?
Inategemea kuna nani nyumbani kwa wakati huo..!! Maana walioko shule huwa wana bajeti zao separate lakini wakiwepo home, ya shule inajumlishwa home. SO kwa siku inarange kuanzia 6,000/- hadi 10,000/- Lakini wakati huo, vufuatavyo vipo home na ni vya siku 30 kila kimoja; mchele, sukari, sabuni ya kuogea na kufulia, mafuta ya kula, DSTV, LUKU, perfume, lotions, wa kusuka, mafuta ya gari, unga, maharagwe, maziwa, majani ya chai, chumvi, gesi mtungi saizi ya kati (15kg), mitoko ya hapa na pale etc
 
Asubuhi chapati mbili na chai moja=1500
Mchana chakula 3000.
Jion chapati na chai 1500.
Usafiri 1000.

Jumla 7000.kwa siku
Broo maisha yako tofauti sana lakin MUNGU mkubwa nataman niķwambie y nimeandika iv lakin tuishie tu hapa hapa
 
Bajeti inategemeana na maeneo au kipato cha mtu kwa siku au kwa mwezi,mfano kwa wanaoishi kijijini bajeti yao huwa si kubwa sana,anaweza kuishi hata wiki bila hela kwani vitu vyote vipo shambani nk,ila kwangu mimi ninaeishi mjini kwa kipato kidogo bajeti ya siku ni elf 10
 
  • Thanks
Reactions: p27
Wife nimemwekea maximum ya tsh 800,000 kwa kila kitu (chakula, usafiri na mambo yote ya nyumbani) na hapo atunze laki moja kila mwezi ambayo ninamdai 1.2m mwisho wa mwaka. Namfundisha nidhamu ya kukaa na cash bila kuitumia.
Mkuu uko vizuri, ni familia ya watu wangapi kama hutojali?!
 
Mwamba huyu hapa
Screenshot_20220717-093748.jpg
 
mim nashinda hasa vijiweni kwaiyo siku nzima uwa nakula kwa kudanda danda kijiwen, Asubuhi kabisa ya saamoja uji kombe la 500, ifikapo njaa mida ya saatatu ndizi jero, mshkaki jero na Coca-Cola bariid ya 600, apo inakatika 1600, mchana wali 1500 na Coca-Cola bariid 600 inakuwa 2100, next Azam energy bariid 600, jion ya saamoja kikombe kimoja cha Alkasusu 500 kwaiyo apo inakatika kama 5,800 lakin sometimes uwa nabadirisha inafika ad 10k
Hii kwa msela ni anasa.
 
Back
Top Bottom