Bajeti yako kwa siku ni shilingi ngapi kwa wewe mwenye familia?

JF bhana,,raha sana,

Ukute mtu na family yake wanashindia mahindi ya kuchoma na maji,

Lakini humu anajitamba kutumia bajeti ya 40000 kwa mlo wa siku moja..
Lengo ni kuwapa wenzao sononeko la moyo.

Jf Kila mtu tajiri.
 
Hayo matumizi hapana aisee
 
Uko vizuri mkuu
Nimeona nifanye hivo pia kwa sababu na yeye aweze kupata pesa zake za pembeni.. Ningeweza kumpa elfu kumi kila siku, ila nyumba isingekuwa na amani...

Hapo najua kila mwezi atakuwa ame save sio chini ya laki moja.. Nna maana kwanini nafanya
 
Wanawake wanajitahidi mno vitu vimepanda mno bei sasa hivi mchele mzuri kilo moja 3000,nyama 8000 ,samaki mzurii sangara 15,000 ,kuku mzuri 25000 wa kienyeji
Siku zingine mtakula maharage
Acha kabisa mie mme wangu ameshindwa kabisa habar ya budget anatoa pesa anaeka kwenye pochi tumia ikikaribia kuisha unamwambia maana kila ukienda sokoni hakueleweki
 
Acha kabisa mie mme wangu ameshindwa kabisa habar ya budget anatoa pesa anaeka kwenye pochi tumia ikikaribia kuisha unamwambia maana kila ukienda sokoni hakueleweki
Fanya hivi nunua vitu kama mchele,unga,mafuta,sukari
Vikiwemo hivi unabakiza pesq ya mboga na unapija maharage mengi unapaki unaweka kwa freezer inasaidia sana ,
Mim hupika maharage,ndegu napaki kwa friji,inasaidia usiku maana watoto wanapenda maharage na wali usiku
Nyama nunua banika au unaichemsha na viungo kisha unaigawanyisha
Iwe kuku au samaki unapaki kwa friji unatoa unapika
Mboga za majan unanunua tu kila siku maana wanatembeza
Nunua dagaa nyingi paki inasaidia sana ,ukipija zako dagaa na matembele ya kutosha mbona mchana mnakula vizuri tu ,usiku wali na ndondo
Siku nyingine mnajiachia na kuku na pilau,bajet zetu maskin hizi
 
Wanawake wanajitahidi mno vitu vimepanda mno bei sasa hivi mchele mzuri kilo moja 3000,nyama 8000 ,samaki mzurii sangara 15,000 ,kuku mzuri 25000 wa kienyeji
Siku zingine mtakula maharage
Mi mchele nautoa Kyela kabisa hivyo napata kwa 2200-2300

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Naam tunafanya hivyo maharage nachemsha kg 2 kwa mwezi inatosha samaki na kuku na nyama naweka pia kwa freezer na mainj, zile pesa za siku ndo hua sijui budget yake maana kila siku mpya ina mambo yake.
Nimenote hapo kwenye kueka viungo. Shukran nadhan itakua ni rahisi zaidi maandalizi ya kupika . shukran
 
Soseji si nzuri kwa afya

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Haishauriwi unga kukaa muda mrefu, angalau ukae wiki tu maana mahindi yetu huwa yana madawa hivyo yatakiwa kuoshwa vizuri, yakaushwe afu yasagwe. Wengi hatukaushi hivyo ule unyevu nyevu husababisha unga kuharibika

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kuna familia zinatumia zaidi ya hiyo mkuu nishaenda kwa ndugu zangu hawamcheshi maji wananunua ya dukani na familia ni kubwa ,kuna chumba ukiingia matikiti yamejaa utafikiri yanauzwa,
Kuna watu wana hela wee
Maji sehemu kama Dsm ni bei ndogo sana hayo ya Uhai, Afya, Msafi ets

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Maziwa,mayai yanatakiwa yawepo kuna hata hunywi maziwa kila siku sababu yananenepesha ,ni unaweka kwa maharage,kztengeneza custard,keki, kupikua chapati
Maziwa watakiwa unywe lita 250 kwa mwaka
Mayai watakiwa kila siku ule yai 1

Hii ni kwa maelezo ya WHO

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…