BAKWATA: Wasichana wa umri wa miaka 14 waendelee kuolewa

Uwezo wenu wa kusoma/sikiliza ni finyu/duni,kasome Tena hiyo ripoti ya bakwata
wewe umesoma hapo????? Embu nieleweshe
 
it’s too sad kwakweli, hajafikiria hata huyo mtoto wa miaka 14 atazaa vipi mtoto
Sure. Kuna wapuuzi atakwambia anaolewa ila kuingiliwa baadaye. Hivi kimantiki kweli kabisa wanaume tulivyoumbwa na matamanio uoe binti umuache eti utakuja kumuingilia baadaye? Danganya toto ya wapi hii. Ni upuuzi wa hali ya juu. Risk factors ni nyingi. Na hata ukitazama mtoto wa miaka 14 anatoa wapi free-will ya kutaka kuoelewa na ampendaye zaidi ya kulazimishwa na wazazi au kurubuniwa na muoaji.

Jamii za zamani ni kweli mabinti waliolewa wadogo kutokana na mfumo wa maisha ya zama za zamani kutomjumuisha mwanamke katika elimu na mambo mengine zaidi ya kubaki na jukumu la ulezi na ndoa.

Zama zimebadilika na wapumbavu wanataka tuendelee kuishi kama tuko mwaka 1120. Halafu baadaye yaanze malalamiko.
 
Mm nadhani wameongelea kwa binti ambaye hasomi mfano binti umempeleka shule akafika la 7 akafeli.
 
Niliku namjibu bibi Faiza amesema ikiwezekana hata miaka 12 waolewe, hata huvyo 14 bado ni watoto na hawajamaliza hata masomo ya sekondari
Kwani watoto wote huwa wanasoma sekondari?
 
na hiyo zamani vifo vilivotokana na uzazi vilikua vingi…sasa ndo wanataka waturudishe huko. Sijui wa nafikiria kwa kutumia nini
 
Waafrika wachache wajinga wanazidi kuionesha dunia na kuuaminisha ujinga wao na upumbavu kwa kujificha nyuma ya dini kwamba MWANAMKE NI CHOMBO CHA STAREHE NA KWENYE MAWAZO MATATU MOJAWAPO NI NGONO TU NDO TUNAWAZAGA.


Hatukuona la maana mpaka kuhalalisha mtoto wa miaka kumi na minne ("14") aolewe?! 😳

Duhh! 😔🙌🏾
 
KWA KWELI.
 
Kila kitu kiangaliwe mazingira wengine wana miaka13 umbo kubwa ataki kusoma na ameanza balaa kitaani, katokea MTU wa kumuoa na mwenyewe kakubali je? Apo vipi. Wengine umri uo bado watoto kabisa ata kuvunja bado .
Kila kitu kifanyike kikiwa tayari.
Afanyiwe counselling na atafutiwe mafunzo mengine ya stadi za kazi na maisha. Sijui kwanini tunayatazama mambo kirejareja bila upana wake.
Wewe hapo ulipo utaafiki mtoto wako au mdogo wako aolewe katika umri huo?
 
na hizo sheria zote zimewekwa kumfaidisha mwanaume…zoooote yani zooooote. Mara wake wanne, mara mbinguni watapewa mabikra 1000 yani zote zina favor mwanaume
 
Sikubalian nao kabisa binti wa 14 ni ubakaji wa watoto tena wafungwe maisha.

Watoto wahimizwe kusoma ili kuondoa ujinga kichwan na sio kuwaza waolewe tu ndoa zenyewe
Wavaa kobazi muzeye hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…