Balozi Batilda Buriani: Mtoto aliyeandika Barua ya kuacha Shule, ana akili sana

Balozi Batilda Buriani: Mtoto aliyeandika Barua ya kuacha Shule, ana akili sana

Kama umarufu huja hivi tu basi kesho naandika barua kwa Mkuu wa wilaya fulani kumuimbisha.
 
"MTOTO ALIYEANDIKA BARUA YA KUACHA SHULE ANA AKILI SANA" RC TABORA
"Niliongea na mkuu wa mkoa wa Mtwara baada ya kuona barua ya mtoto aliyetaka kuacha shule, nikamwambia huyu mtoto ana akili sana kwasababu haiwezekani mwanafunzi mtoro aandike barua kama hiyo, nikamwambia mkuu wa mkoa wa Mtwara mtafute huyu mtoto na kweli amemtafuta na kutatua changamoto zake na sasa amerudi shule mwenyewe, kwahiyo walimu wasaidieni watoto kuwajenga kisaikolojia"-Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Buriani katika kongamano la walimu na uchumi.

Taufiki Salumu mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Msimbati Mkoani Mtwara ambaye aliandika barua ya kuacha shule kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema lengo kubwa la kutaka kuacha shule ni hali ngumu ya maisha ambayo imemlazimu yeye kuchukua maamuzi hayo.

Chanzo cha habari ni CGFM Tabora

Pia, soma:

1). Mtwara: Mwanafunzi wa kidato cha 1 aandika barua kwa Mwalimu Mkuu akisema Shule imemshinda
View attachment 2132031View attachment 2132032View attachment 2132033

Kitu gani kimemwezesha RC Buriani kumtambua huyu dogo kuwa ni mtoto mwenye akili sana?
 
..sidhani kama Dr.Batilda alikuwa na nakala ya barua ya mtoto aliyeacha shule kabla hajatoa kauli kuhusu mtoto huyo.

..Form 1 lakini anaandika kwa kiwango cha chini sana.

..huyo mwanafunzi tatizo lake sio muandiko tu, bali hata kupangilia maneno, na kuandika kwa ufasaha, hawezi.
Mtwara kuna mambo. Mama Tariq haongei... Huku Taufiq anafunguka... Dah

Suala la mpangilio sii ishu. Mtoto anaonekana kuwa smart. Pia kuna ishu zilizokuwa zikiendelea kama vikadi ambapo walimu wanajua vizuri

Pia baada ya kuona hataki tena shule hakuwa na sababu ya kurembaremba mwandiko wala mada. Ni kama wakati anaandika alikuwa ndani ya boti la uvuvi.
 
KIJANA KAANZISHA MOVEMENT..

Nchi yetu huwa kuna revolutionary minds zinaibuka lakini hupotea kutokana na Watanzania tumejaa ubinafisi. Huyu kujana kawakilisha mamilioni ya watoto wanaishi mazingira magumu sana. Watoto hawa shule ni sawa na adhabu kwao.

Imagine miaka minne mwanafunzi anaishi kwa mateso..
Njaa
Viboko
Umbali
Kutoelewa darasani
Matatizo ya kifamilia etc.

Sasa kijana huyu anakosa back up. Tuko busy na kesi ya Mbowe na Safari za Hangaya.

We realy need to come out suporting these kinds of movements. Sijui wale watu wa haki za binadamu nao wako wapi.

Nina uhakika huyu mwanafunzi ana mengi ya kusema.
 
Mtwara kuna mambo. Mama Tariq haongei... Huku Taufiq anafunguka... Dah

Suala la mpangilio sii ishu. Mtoto anaonekana kuwa smart. Pia kuna ishu zilizokuwa zikiendelea kama vikadi ambapo walimu wanajua vizuri

Pia baada ya kuona hataki tena shule hakuwa na sababu ya kurembaremba mwandiko wala mada. Ni kama wakati anaandika alikuwa ndani ya boti la uvuvi.

..huyo dogo uwezo wake wa kuandika unalingana na mtoto wa darasa la 2 wakati mimi niko shuleni.

..pia dogo alitakiwa aandike barua yake kwa KIINGEREZA kwasababu hiyo ndio lugha ya mawasiliano ktk shule za SEKONDARI.

..simlaumu dogo bali nailaumu serikali kwa kushindwa kuboresha mazingira ya utoaji elimu haswa kwa maeneo ya vijijini.

Cc Nguruvi3, MALCOM LUMUMBA
 
Watoto wengi wanaacha shule sababu ya mazingira magumu. Huwezi amini hii Tanzania kuna kaya mlo mmoja kwao ni kama neema imewashukia achilia mbali kunywa soda ni anasa kabisa.
 
Kweli dogo ana akili sana,ametafuta njia ya kusikika
 
Naona Watu wanapoteza pointi ya msingi ya hili suala.

Ni bora kukaa kimya na kutafakari badala ya kila Mtu kukimbilia kutoa hitimisho kwa hisia binafsi.

Huenda kila mmoja akawa na tafsiri yake ya kumtambua Mtu 'smart' lakini vipi kama tutadhani smart ni yule anayefikiri shule/elimu ndio inaweza kumkomboa yeye na wanaomzunguka?.

Nimeiona na kuisoma hiyo barua na sioni dalili yoyote ya kuonesha kama yupo smart (kupitia hiyo barua)...labda kama kuna taarifa nyingine nyuma ya pazia ambazo bado hatujazijua ambazo labda Mh anazifahamu...kinyume cha hapo tusimpumbaze yeye na wanaomzunguka.

Labda tuone u smart wake kwa namna alivyoamua kuvunja ukimya na kutoa la moyoni ambapo sasa sisi wengine tukae chini na kutafuta kuna nini kinaendelea?..kwa Kijana wa kidato cha kwanza (kama inavyosemekana ) kuandika hivyo basi ni dalili tosha kuwa Walimu hawakufanikiwa kumfundisha..au la labda ni mtoro kupita kiasi mpaka anashindwa kujifunza.

Na je hatudhani pia kuwa Wazazi wake nao ni tatizo?. huenda wao hawajasoma na hivyo hawaoni umuhimu wa Mwana wao kusoma.

Na kwa upande mwingine kama Mtoto anaona masomo yanamchanganya na kumpotezea muda hii ndio iwe chachu ya kuona umuhimu wa kuwa na elimu mbadala badala ya kulazimishana na mifumo ya elimu tuliyorithi kwa Wakoloni.

Vipi kama huyu sasa akaanza kuandaliwa kwa kupewa elimu ya uvuvi ya nadharia na vitendo?..ni kama ni sahihi nilivyosikia kuwa anatamani akafanye uvuvi.

Kwa karne hii hili si jambo la kushadadia bali ni kurudi nyuma na kujiuliza iweje 2022 Jamii bado haioni umuhimu wa elimu?.
 
Wasije wakawa wanamlazimisha na yeye kukubali kwa shingo upande.
 
..sidhani kama Dr.Batilda alikuwa na nakala ya barua ya mtoto aliyeacha shule kabla hajatoa kauli kuhusu mtoto huyo.

..Form 1 lakini anaandika kwa kiwango cha chini sana.

..huyo mwanafunzi tatizo lake sio muandiko tu, bali hata kupangilia maneno, na kuandika kwa ufasaha, hawezi.

Kwa level ya shule za vijijini huyo dogo Kajitahidi sana.
 
Ngoja arudi shule akasome tu...vijana wengi huacha shule Kama huyo hasa huko vijijini,unashindia kipande Cha andazi moja kila siku,inahitaji uvumilivu mkubwa kustahimili hiyo Hali kwa mtoto mdogo tu Kama huyo...ila hati yake ni ya kurekebisha kidogo tu...
 
Back
Top Bottom