Balozi wa Tanzania aliyechanjwa Corona Israel arejeshwe nyumbani mara moja

Swali

La kujiuliza: Je alitakiwa kuchanjwa au yeye mwenyewe alijipeleka kwenda kuchanjwa? Hata ulaya hawachanjwi kwa lazima!
Unajuwa lazima lina njia nyingi kulielewa, nchi nyingi sehemu za kazi imeanza kuwa lazima wakiwapa chanjo watu wengi itakuwa ili uende kazini lazima umechanjwa. UAE wameanza hujaenda kuchanjwa itakubidi kila wiki upime corona kwa gharama zako mpaka uchanjwe ukiwa umechanjwa unaingia kazini no issues. kwa maana nyingine utaenda mwenyewe kuchanjwa.
 
 
Hawezi kufanyiwa chochote huyo balozi kati ya hivyo ulivyosema, misimamo ya nchi katika jambo la Kimataifa kama hilo haliongelewi holela holela kwenye msafara wa kutoka Chato kuja Dar, njiani, misimamo kama hiyo kama nchi inawekwa kimaandishi. Watachanjwa wengi, hata wewe na watoto wako mtachanjwa maana hata kiwanda cha bandeji hamna nchini kwenu, mnawategemea kila kitu, mtalainika tu.
 
Mnaanza UJINGA wa kiwango cha ujima.
Akichanjwa wewe unadhurika nini kama Taifa?
Hukisikia rais aliposema kuna watu walioenda kuchanja waliporudi wakaleta na Corona ya ajabu. Kasikilize hotuba aliyotoa akiwa Tabora.
 
Hivi ukichanjwa huwezi ambukiza mwingine?
 
Hivi ukichanjwa huwezi ambukiza mwingine?
Chanjo haikufanyi kutopata corona ila hutaumwa kwa hiyo corona itakuwepo kasoro kuumwa kutapungua. Swali lako ni zuri tuchukulie asilimia kubwa wamepata chanjo ina maana hatutajali tena sababu nitapata kama mafua ya kawaida tu tatizo ukiwa wewe umechanja halafu family yako hawajachanja unaweza kuambukiza kama una corona. Kuna issue pia watu wanasema wakichanja wao sisi ya nini tena wao hawawezi kuumwa. Tatizo lipo corona wakiachwa wasambae kwa watu wengi maambikizi mengi basi wanajigeuza kivingine janga linaanza upya ndio maana WHO watalazimisha wote kupata chanjo. Haya mengine chanjo nzuri au mbaya hilo la mtu binafsi ila itabidi huu ugonjwa wa dunia.
 
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi ...
 
Na wewe mwenyewe pia.
Mlinzi no 1 wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
Ukiona moto unakuja kwa kasi usisubiri tamko la serikali.
Chanjo inaleta korona ya ajabu ajabu.....mlevi mmoja alisikika huku akipigiwa makofi
 
Mijitu isiyokuwa na exposure kakaa England mwaka mmoja tena miaka ile PM Margaret Hilda Thatcher(Iron Lady)mwambieni kuna madiliko mengi Arsenal wako Emirates na kuna Gatwick airport bwa bwa bwa
 
Chanjo inaleta korona ya ajabu ajabu.....mlevi mmoja alisikika huku akipigiwa makofi
Hili gonjwa halitakuja kuisha kwa sababu si watu wote watapata chanjo mapema hata kama wanahitaji. Kwa hiyo virusi navyo vinajibadilishabadilisha ili kuendelea kuishi na vitaendelea kutoa roho za watu duniani hadi tuwe kitu kimoja.
 
Kama chanjo haizuii kutopata corona basi kuchanja ni upuuzi mtupu.

Kwanza kuna video inazunguka mitandaoni kwamba wao wana fake sindano ya chanjo,,

Wakati wengine wakiwachoma kweli..

Bado inaleta mashaka matupu..
 
Sasa Bavicha wataishije bila majungu? Kwanza hata JF patapoa sana. So unakumbuka pale walipotwambia Mkimbizi Tundu Lissu atahutubia Bunge la Ulaya JF ilivyochangamka hadi pale Mkimbizi mwenyewe alivyokanusha?
Bavicha chapeni kazi majungu siyo mtaji!
 
Tanzania haitaki wananchi wake wachanje, inakuwaje wachache wakiuke msimamo wa nchi?

Kiazi sikiliza, msimamo wetu wa hovyo unahusu mipaka ya kijiografia. Inapokuja kwenye mambo ya kimataifa - acha mambo yako ya kijijini kijijini kwako.

Tanzania hii hii, anayetaka kusafiri kwenda nje ya nchi anapimwa korona kwa gharama ya 230,000 (wageni, wakazi na raia)! Halafu kuna wanaokutwa chanya na kutopata cheti cha kusafiria!!

Utakuwa hujui uligeugeu wetu huu na utakataa niliyosema hapo hayafanyiki!
 
Sasa Bavicha wataishije bila majungu? Kwanza hata JF patapoa sana. So unakumbuka pale walipotwambia Mkimbizi Tundu Lissu atahutubia Bunge la Ulaya JF ilivyochangamka hadi pale Mkimbizi mwenyewe alivyokanusha?
UvCCM+uvccmCCM=bavicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…