TANZIA Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine J Mushi, afariki dunia kwa ajali ya Gari

Ajali hii ina maswali mengi kuliko majibu.
Mke , watoto walikuwa wapi? Balozi anaendesha gari mwenyewe kutoka Dar kwenda Kilimanjaro tena USIKU?
 
Asee bwashee kaamua kukomaa mwenyewe kwenye usukani?kaona shida kutafuta dereva ampe hata laki 2?amfikishw nyumbani arudi zake ?ubahili huu!
Nipo tayari kuzodolewa pote la mbali!
Rip balozi
Walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini wafu hawajui lolote, na hakuna malipo kwao tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Yote ambayo yanaweza
mkono wako kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa maana kuzimu, mahali utakapokwenda, hakuna kazi, hakuna mipango, hakuna maarifa, hakuna hekima (Mhubiri 9:5, 10).
 
Najiuliza maswali mengi sana Mara kunapotokea msiba!

Watu wazuri hawafi.?? Mbona Jk yupo, Kinana yupo?. Dooh!

RIP balozi wetu
Walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini wafu hawajui lolote, na hakuna malipo kwao tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Yote ambayo yanaweza
mkono wako kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa maana kuzimu, mahali utakapokwenda, hakuna kazi, hakuna mipango, hakuna maarifa, hakuna hekima (Mhubiri 9:5, 10).
 
How long does it take ku confirm kuwa ni yeye aliyefariki? Siamini kama ndani ya 6 hours KM anakosa access ya ku confirm a such socking taarifa kwa mtu wa wizara yake!!
Si ndio maana JPM alim faya huyo Sokoine. He is such a douchebag... yupo yupo tu, aloof on stilts

Siku ya tatu hujui kama balozi wako kafa ???? Katibu Mkuu Foreign Affairs ??

Atrociously incompetent. Upo hapo kwa sababu tu babaako Sokoine....

Hebu nenda Mbezi msibani katafute taarifa acha kuzubaa zubaa kama kawaida yako.
 
View attachment 2447629
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati akiendesha gari aina ya crown lenye namba za usajili T175 DMF kuelekea Moshi, Kilimanjaro.

===

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki ajalini​

Alhamisi, Desemba 15, 2022
balozi-pic.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy

Muktasari:​

Balozi huyo amefariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Tanga. Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa hapa.

Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Desemba 15, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

"Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia," amesema Balozi Sokoine.

Chanzo: Mwananchi
Majibu yako Balozi Joseph Sokoine sio katika wadhifa wako.Ina maana hakuna mawasiliano na hao mabalozi wako na hasa wawapo likizoni?
Je aliporejea alitupoti hapo wizarani kuwa yuko likizo na atasafiri?
Je hao Polisi walipopata taarifa ya ajali na kuthibitisha kuwa ni mtu wa wizara Fulani walipeleka taarifa ofisi yako?
Ndugu pia wamepewa taarifa je walizileta ofisini!
Je umeuliza watu wa ofisi yako kupata uhakika kabla ya majibu ya mkati unayotoa??

Jitafakari.
 
RIP Balozi Mushi, nimeamini wanaopendwa na wengi hufa wangali vijana!.
Huyu ni Balozi mshikaji wa 3 kuchomoka pale foreign!, alianza mshikaji Balozi Cisco, Mshikaji Balozi Akili, kufunga kufungua mshikaji Balozi Edwin Rutageruka!, sasa mshikaji Balozi Celestine Mushi!.

Wajameni kama hali ya uchumi inaruhusu, kwa gari ndogo, saloon cars, nunua chuma cha Mjerumani, na sio haya makaratasi ya Japan!.
RIP Balozi Mushi!.

P
Crown mbona zunasifika sana,au wadau husema uongo?
 
Jihoji.
Ajali ya mtu mzito kama balozi inatokea juzi ila inaanza kusikika mitandaoni leo(do you get the point?)

Akiwa peke yake anakoa gia kuelekea kaskazini anakutwa amefariki garini na gari likiwa limeteketea(kirahisi tu? Milango ilijilock? Labda magari ya umeme hatujui kilichojiri)

Vipi kama alichukuliwa na kuhojiwa vizuri halafu baada ya mahojiano jamaa wanao hoji wakaamua kumtupa hapo na ikachukuliwa gari mkweche moja ya kupitezea maboya ikapigwa kiberiti?
Huyu wamemla kichwa

Kuna neno la kiswahili linasema

"Utakuwa Mfano kwa wengine"
 
Ni kweli, chuma cha Mzungu ni salama hata unapokuwa unakiendesha tofauti na makaratasi ya Mjapani.
Hakuna kitu mkuu,siku ikifika imefika,mbona Princess Diana alifia kwenye Mercedes Benz matata sana!hata yule Ginimbi aliekuwa tajiri mmoja kule Zimbabwe alipata mzinga wa kufa mtu akiwa kwenye Rolls Royce ya kueleweka sana,tuombe tu Mungu kwani hatujui siku wala saa kifo kinapokuja...
 
Majibu yako Balozi Joseph Sokoine sio katika wadhifa wako.Ina maana hakuna mawasiliano na hao mabalozi wako na hasa wawapo likizoni?
Je aliporejea alitupoti hapo wizarani kuwa yuko likizo na atasafiri?
Je hao Polisi walipopata taarifa ya ajali na kuthibitisha kuwa ni mtu wa wizara Fulani walipeleka taarifa ofisi yako?
Ndugu pia wamepewa taarifa je walizileta ofisini!
Je umeuliza watu wa ofisi yako kupata uhakika kabla ya majibu ya mkati unayotoa??

Jitafakari.
Wewe unataka kusikia unachotaka kusikia-sasa kakosea wapi. Hajapata taarifa, akipata atatoa-shida nini sasa?
 
View attachment 2447629
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati akiendesha gari aina ya crown lenye namba za usajili T175 DMF kuelekea Moshi, Kilimanjaro.

===

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki ajalini​

Alhamisi, Desemba 15, 2022
balozi-pic.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy

Muktasari:​

Balozi huyo amefariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Tanga. Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa hapa.

Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Desemba 15, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

"Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia," amesema Balozi Sokoine.

Chanzo: Mwananchi
Hiyo njia ya Dar Segera Korogwe Moshi Arusha siyo ya kuendesha usiku, halafu ukiwa na gari aina ya Toyota Crown Athletee! Tena ukiwa peke yako. Labda kama alipatwa na dharura.

Apumzike kwa amani. Hiyo barabara ni nyembamba! Ina mashimo/viraka vingi! Hivyo ni hqtari sana kuendesha gari usiku, kama siyo mzoefu.
 
Back
Top Bottom