Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Eleza kifupi
Jpm kuhusu nkataba alidanganya? Na


Kama ndio haya sasa weka mkataba hususani masharti na namna ambavyo uta operate
 
Umepiga porojo miingi huo mkataba hatujauona tuujadili vyema.....
so tunaweza kuwa nje ya mada
 
Kwa masharti hayo huyo Mary Nagu atafutwe huko halipo na kuwekwa Segerea walau mwezi mmoja, how dumb was she kukubali mambo kama hayo.

Nikumbushe Rais alikuwa ni nani kipindi nchi inaingia nkataba huu. Nachelea /nasita kutumia neno Mkataba.
 
Ili mradi mikataba iwe wazi.

UNAKUMBUKA MIKATABA YA GESI ALIYOSAINI KIKWETE KWA HARAKA HARAKA KARIBU NA MWISHO WA UTAWALA WAKE? ULIIONA IKIWEKWA PUBLIC? HAWA JAMAA WOTE NI HIVYO HIVYO KUNA VITU WANAFICHA VYA KIFISADI!!! WATAKWAMBIA KUNA CONFIDENTIALITY CLAUSE INAWABANA MIKATABA ISIWE PUBLIC!!
 
Very ambitious mkuu!

Lakini ni sawa..., 'dare to dream Big'! Kwani kuna tatizo hapo?

Hata hivyo umenikumbusha, kama nilivyokumbushwa na ile Bandari ya Mwambani Tanga.

Hapa Dar, kuna watu tayari walihamishwa pale Kurasini, na kulikuwa na harakati kama hizo ulizozielezea kwa wachina kulitumia eneo hilo kama sehemu ya kufikisha bidhaa zao na nyingine zikiundiwa hapo.

Tuliambiwa, wanunuzi toka Congo na kwingineko wangekuwa wakija kwa wingi hapo kufanya biashara.
Lakini, kama ilivyokuwa na Mwambani, hilo nalo hatulisikii tena na sijui sehemu hiyo waliyohamishwa makazi ya watu linatumika kwa kazi gani wakati huu.

Mipango ya waTanzania wakati mwingine inazingua sana!
 
Kwahiyo na sisi tz tutakua Kama Rwanda na Burundi?!

hatutakua na bandari.

Mizigo yetu tutakua tunapitishia Bandari ya China ya Bagamoyo?!

Huu mradi ni hatari kwa maslahi ya taifa.
 
Mashariki ya mbal kama wap? Hiv mzigo utoke china Europe au Dubai uje upakuliwe tanzania halafu urud Masharik ya mbal?
 
HAKUNA LEGACY YA HESHIMA,ATAKAYOIACHA MADAME PRESIDENT KWA KUFANYA/KUSIMAMIA MABADILIKO YA KATIBA MPYA....
 
Hizi kelele zenu za bandari ya bagamoyo dawa hii hapa

Biashara ya duka, mtu huwa huingii mkataba wowote na serikali .Unaenda tu kuomba leseni yaliyobaki ya kwako.

Sasa serikali kama inaona kuna uhitaji wa biashara ya bandari itangaze tu kuwa tunahotaji biashara ya bandari hata mia anayehitaji aje aombe leseni ajenge.Mengine yote yake kuanzia kununua ardhi kufidia nk yanabaki kama ambavyo investor wengine wote hufanyiwa

Hii itakomesha huu utapeli wa watu kutaka kuuza nchi kwa mikataba ya kipuuzi .Bandati ni godown tu la mizigo ya nje inayoingia au kutoka hufikia kwenye hilo godown linaloitwa bandari haihitaji mikataba ya ajabu ajabu na serikali kujenga hilo godown la bagamoyo linaloitwa bandari ya bagamoyo

Ajenge godown lake na magodown mengine yataendelea kama yalivyo .Ndio maana ya biashara huria yenye ushindani

Madalali nendeni mkawaambie wajenge kwa pesa zao tutakuwa tu tunakutana nao TRA

Wawekeze tu kama wawekezaji wengine tu .Walete mitaji yao wajenge tukutane TRA lakini kidiwrko kikaratasi chochote cha mkataba kati yao na serikali waje tu kama wafanyabiashara wawekezaji full stop.

Si sahihi kuuza nchi kwa sababu ya magodown yanayopigiwa debe kujengwa bagamoyo
 
Mkuu Kilatha kumbuka hizo $10B ni part ya FDIs inflow... Kwa Mtazamo wangu tungeangalia terms za huo Mkataba
 
Wauweke mkataba public wananchi wapime kama.uendelee au la!
 
Na kama tushasema investor anaruhusiwa kuajiri watu anaoona wanamfaa...hivi matumaini ya job creation kwa wazawa itakuwaje? Maana mchina habagui kazi hata reachstacker operator bandarini anaweza mleta mchina….

Naomba huo mkataba wanapoujadili tuweke wazi ajenda ya local content....
 
Mkuu Kilatha kumbuka hizo $10B ni part ya FDIs inflow... Kwa Mtazamo wangu tungeangalia terms za huo Mkataba
Tunahitaji hiyo inflow ya $10 billion yote hilo halina shaka. Lakini sio hela yote hiyo inaenda jenga bandari, kuna na miradi mingine pia.

Katika hizo investment zote za Bagamoyo mkataba wa ‘Build Operate Transfer’ baina ya Tanzania na China uwe based na gharama za Bandari pekee.

Hizo gharama zitakazotumika katika investment zingine kama supporting industries ya bandari serikali aina shida ya kuingia mikataba ya ubia huko. Wachina wawekeze tu wenyewe na kumiliki asilimia 100% hiyo miradi mingine subjected to Tanzania laws na walipe kodi kama biashara zingine.
 
Yaani wanasiasa ni watu wa ajabu sana. Tunaulilia mkataba - basi watauweka wazi lakini tunauhakika gani huo ndio mkataba orginal. Maana hata wakitupa feki tutajuaje na wao wasign mwingine? Wao watanufaika upfront. Na sisi tuliyo wengi? Tukija kushtuka ni wajukuu na vitukuu wetu wanaumia….

Sasa badala ya generation hizo kufurahia nchi na rasilmali waliyorithi watakuwa tena busy kujikomboa….
 
Hivi inaingia akili kwamba watanzania wanaweza kuchukulia maoni ya Kakoko seriously - kwani uchunguzi wa CAG umetoa picha gani kuhusu projects za kimangamushi za TPA alizo zi-sign Kakoko mwenyewe - kuanzia ujenzi Bandari kwenye Lakes zote Tanzania pamoja na Bandari za Bahari za kuu ie Dar, Tanga na Mtwarahusu Taifa letu,hapo tunazungumzia masuala ya ujenzi wa infrastructures,je,tukija kwenye ununuzi wa flow meters bei walizo nunulia ndio bei alisi kweli? After sales contract ya flow meters inasemaje, je, kulikuwepo ulazima wowote wa kununua flow meter mpya pale Dar Port badala ya kukarabati ya zamani, mwaka juzi nilimuona JPM akiwahoji ma data entry clerks wa container scanners, aliwakuta wapo kwenye chumba ambacho hakuna dirisha la kuangalia kinacho endelea kwenye kwenye zoezi la ku-scan makonteina hawajui maconteina magapi yanapitishwa bila ya kukaguliwa,na Taifa linapoteza revenue kiasi gani kutokanax na hujuma hizi zilizo dhahiri - si rahisi udanganyifu huu ukawa unaendelea hapo Bandarini bila ya top managment anayo ongoza na Kakoko bila kujuwa, haya tuje kwenye manunuzi na ufungaji wa survaillance and secyurity systems hapo bandari,je, Serikali ikitumia an independent consultant akakagua vifaa vyote na system nzima wanaweza kusema gharama za manunuzi na ufungaji wa security sysyem haukuwa highly inflated?

Juzi hapa nilimsikia CAG aki question some projects zinazo fanyika TPA lakini hazikamiliki miaka nenda rudi wajanja wanaendelea kupiga hela tu under Kakoko's watch,CAG alizungumzia vile vile suala la kuwapa tenda makampuni ambayo hayana sifa mwishowe wanashindwa kumaliza kazi wanazo pewa,o hii inaleta picha gani, ni wazi tenda hizo wanapewa makampuni/watu kwa kujuwana na si ufanisi wa kazi, how about TPA (IT) system going down for days on end na wahusika wana manufacture lame excuses za kutaka kuendelea kufanya kazi manually thereby bypassing computer system ili waendeleze wizi na udanganyifa mwisho wa siku kulikosesha Taifa letu mapato - mtu ungetegemea Taasisi kama TPA inge-install a robust backup system with an equally impregnable "FAILOVER" system ya kuwezesha mitambo ifanye kazi uninterrupted 24X7 , badala yake wanawachia wajanja waingilie system wakiwa na lengo la kuikosesha mapato Serikali.

Nayasema haya yote kutokana na kauli ya Kakoko aliyo itoa akiwa Mkoani Mwanza aliwakandia Wachina kuhusu mradi wa ujenzi wa Bandari ya B'moyo alionekana wazi wazi yuko overly determined kuhakikisha mradi huo unazikwa au wenda ikawa alitaka wachina waje wawekeze katika ujenzi wa Bandari ya B'moyo kwa pesa zao halafu mwisho wa siku Bandari ikabidhiwe TPA chini ya Uongozi wa Kakoko mambo ya ndio sivyo ya shirika la TPA yajirudie tena kwenye Bandari mpya ya B'moyo, wakati akijuwa wazi kwamba Serikali haitachangia hata senti tano kwenye project nzima - na ukweli wa mambo hakuna mwekezaji mwenye akili timamu anaweza kubariki masharti ya ajabu kama hayo.

One more thing, former TPA Director General si msemaji wa Serikali, si katibu mkuu wa Wizara au Waziri wa uchukuzi - yeye ana moral Authority gani ya kutaka kuzima mradi ambao ungeweza kupaaisha Taifa letu kimaendeleo in terms of ujenzi wa viwanda vingi vya kisasa kuzunguka bandari, Korea kusini ilikuwa tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa high tech factories karibu na bandari, bandari ya B'moyo ingekuwa incoporated kwenye mpango kabambe wa ku-link reli za Continental Europe, Uingereza, Urusi, Asia (Iran,Korea nk) pamoja na Uchina kwenyewe - mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli popote Duniani bila ya kutegemea usafiri wa meli ambao ni dead slow - sasa wachina kutaka kuiweka bandari ya B'moyo in the loop ya silk road project hilo waswahili hawalioni,wamekazania ujenzi wa Bandari ya B'moyo ipigwe chini.

Maoni yangu, mama Samia na wazalendo wengine wanao litakia mema Taifa letu wahakikishe mradi huu unafufuliwa kwa hari mpya na kasi mpya, msiwasikilize waswahili wanao kuwa driven na kampein chafu zinazo ratibiwa na vyombo vya habari vya magharibi na intel agencies zao kuwahujumu Wachina kiuchumi na kidiplomasia, fufueni mradi wa bandari ya B'Moyo kama kuna mapungufu ya hapa na pale kwenye mkataba basi wahusika wakae chini na ku-resolve kistaarabu mapungufu yatakayo jitokeza na sio kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kuanzisha kampein chafu za kuwasema vibaya wachina mnarudia kampein zile zile za Waingereza na Wanerikani za kuwakandia Wachina 24X7.
 
Watanzania hata masharti yote tunayoyataka kwao wakitutekelezea,bado bandari zingine zitakufa kifo cha mende,sababu ni ufanisi wa wenzetu katika bandari.Lazima zife hatuna namna.
 
Kwa kuangalia tu sioni sababu yoyote zaidi ya uhuni!
Ziendelezwa za Tanga, DSM na Mtwara.
Kuna ka mchezo kachafu kabisa kanaendelea hapa, makuwadi wapo job.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…