Bangi ni kama pombe tuu, ukiona huiwezi acha. Tukiwa shule form three ujana ujana wa kujaribubkila kitu, kuberi, pombe, fegi, ugoro, kuna siku mpuuzi mmoja si akatupeleka shamba la miwa, kumbe katikati wanalima bange.
Tukakuta wajuba wanakoka, ebana si tukajaribu pafu moja moja. 😁
Mimi nilihisi kama kichwa kinapasuka na nina paa mawinguni.
Jamaa yangu mmoja yeye aliqnza kucheka mpaka anagalagala chini, anasema eti tupo uchi. 😁
Mkali mmoja na hesabu ni marehemu wa kuitwa Carlos, yeye alianza kutembea anaruka ka.a anaruka mitaro hivi. Tukamuuloza vipi, akasema kuna mitaro mingi kinoma wazee. Jamaa yangu Henry yeye alitabasamu sana siku hiyo, akawa anasema twendeni tukalime shamba la shule wazee. 😁
Ilibidi wale mabigi, watushike kwanza na kutulazimisha kuingia kwenye maji baridi mtoni na kutupa miwa mingi sana tule. 😁
Baada kama ya lisaa ndio tukawa sawa tena, tukarudi bwenini kimya kimya.
Mi nakumbuka nililala usingizi nilikuja amka mchana kesho yake. Naamka sio njaa ile, sijawahi sikia njaa kama ile tena.
Sijagusa kaya tena maisha yangu yote. 😁
Bangi na Maji ni marafiki wakubwa sana, Bangi stimu yake ni Miwa. Ukiona stimu imepanda sana wee chukua muwa mkubwa anza kula, kadiri unavyoula ndio bangi inakata.
Au kama ni mtoni, we jitupie, ukikaa dakika 15 utaona stimu inakata na unatoka ukiwa poa tuu.
Mvuta bangi yeyote akivuta bangi, lazima akaoge au utafune muwa.