Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

Kuhesabu pesa ni kazi kwelikweli mkuu..njaa unaipata chapu
 
Madirisha yapo ya aina 2.

Kuna ya light cash na bulk cash.

Kule bulk cash kuna kiti kabisa unakaa unaangaliana na teller kwa sababu kuna msoto mkubwa.

Huku kwenye light cash hakuna kiti bali watu husimama au husubiria kwenye viti waitwe ila wakati wa huduma husimama.

Kwenye light cash kusimama siyo shida. Ila tatizo linaanza pale ambapo mtu wa bulk cash aidha anatoa au ana deposit kwenye dirisha la lght cash. Unaweza ukasubiri 40 minutes.
 
Kuhesabu pesa ni kazi kwelikweli mkuu..njaa unaipata chapu
wazungu kuweka mashine za kuhesabia unafkiiri wao wajinga,...

Bora uhesabu noti mpya sasa uhesabu noti za wamama wauza.mkaaa au zilizotolewa.kwenye.KIBUBU.

noti za kwenye KIBUBU ukizishika kwanza kama zina unga unga sasa mtu anakuletea alivyozipanga hata huelewi.

Unazitupia tu kwenye Drooo badae kwenye kuzichambua uzipange then uzihesabu weeee...

acheni bana hizi mambo, ma teller wao wawe tu waaminifu muda wa kuhesabu hela kaunta tutadanganyana
 
Unatakiwa kuwa bandidu unamwambia aroo geuzia huku mashine ya kuhesabia hela uangarie kwa makini. mm niliwah tumwa na bosi nikamuambia geuzi huku nitazame inavyohesabu
hahah akageuza? mkuu hawa ma teller hatuwakaziii kwasababu sisi ni wateja wa kila siku,kuna namna ukikuta ma teller wote umewakera zamu yako ikifika tu ndio nae tumbo la kuigiza linamshika anaenda chooni anakuacha umesimama hapo.

so tunaenda nao softly tu
 
Umepata bank teller sio mwaminifu mkuu...
Utaratibu wa bank ukitoa hela kwa bank teller hakikisha wakati wa kuhesabiwa unakodoa macho kama bundi... usisinzie.
Na ikitokea ukiwa na doubt hata kdg mwambie arudie kuhesabu na kama anajifanya jeuri omba kuonana na mkuu wake (head teller)....
Utaratibu wa makabidhiano ya hela ni kuhakikisha anaetoa na anaepokea wote wamehakiki usahihi wa pesa. Hio ni haki yako
Jengine mbona kuna wateja wengine nao pia sio waaminifu, wanapoenda bank kwa makusudi wanaweka pesa pungufu teller akijichanganya kdg tu keshafunga pesa less. Baadae hizo hizo ndio anakuja kupewa mteja mwengine
 
na ndio bank saivi walivyo wanatumix wateja wa bulk na wa light sababu za msingi hamna wanajua wenyewe, matawi machache sana wanaojitambua
 
hili nalo tatizo
 
na ndio bank saivi walivyo wanatumix wateja wa bulk na wa light sababu za msingi hamna wanajua wenyewe, matawi machache sana wanaojitambua
Mimi huwa ninawaauliza ni kwanini madirisha yapo mengi ila teller ni mmoja?

Majibu hawana!
 
Kuna mchezo wa noti bandia, utashangaa unapeleka milioni sita unaambiwa una noti bandia 30,000/= za 10,000/= jumla
inafika wakat mtu unataka wakataa bank kabisa ila ndio ivyo bank wana umuhimu huwezi wakataa..

hamna wakala anaweza kukupa chenchi za 2m ila bank unapewa.

Hawa watu ni kuwakazia tu kwenye utendaji kazi wao.
 
Unakuta mtu ana begi mgongoni akifika analitua pale counter anaanza kuchomoa burungutu moja baada ya lingine unabaki tu hiiiiiiii
 
Nilitoa milioni, nikakuta kuna noti mpya ya elfu mbili badala ya efu kumi, ikawa tsh. 998,000/=.
 
Kweli kabisa kuna siku nimetoka kadoo bureau de change, hela imehesibiwa vizuri nakuwa makini kabisa, nimefika holland hse yule bitch ananimbia imepungua 60k aisee nilimuwashia moto, nikaomba tuangalie camera manager akamuita yule malaya pembeni, nikaambiwa hili litashughulikiwa internally waka deposit mchongo wangu
 
inafika wakat mtu unataka wakataa bank kabisa ila ndio ivyo bank wana umuhimu huwezi wakataa..

hamna wakala anaweza kukupa chenzi za 2m ila bank unapewa.

Hawa watu ni kuwakazia tu kwenye utendaji kazi wao.
Wahuni sana hao jamaa! Wanatunza noti bandia za kubambikia wateja wao
 
Unakuta mtu ana begi mgongoni akifika analitua pale counter anaanza kuchomoa burungutu moja baada ya lingine unabaki tu hiiiiiiii
kuna watu nikiwakuta mbele yangu naondoka hilo tawi natafuta tawi lingine.

maana wana hela kwenye mabegi,ndani ya suruali,ndani ya makoti,nikimuona tu najua hapa sitoboi nageuka naenda tawi jingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…