Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

kuna watu nikiwakuta mbele yangu naondoka hilo tawi natafuta tawi lingine.

maana wana hela kwenye mabegi,ndani ya suruali,ndani ya makoti,nikimuona tu najua hapa sitoboi nageuka naenda tawi jingine
ukiwa mzembe kweli unatoa hela maana yeye akiongea anaongea kwa kujiamini haswa
 
Lakini kuna notes counter pale, anaweka buku buku zikifika 100 anafunga. Unaibiwaje?
Akiamua kukuibia anakuibia tu, wizi ni taaluma.
Pamoja na kukodoa macho anavyohesabu atakuangalia position uliyokaa, ataligeuza fungu kukuchagulia eneo la wewe kuona kisha haraka sana atatumia unyongovu wa mikono kutelezesha noti moja tu hutaona kabisa.
 
Kuna baadhi ya ma Teller ni vibaka. Mimi mwaka 2020 nilipigwa Hilo tukio mkoani. Nilienda bank kutoa milioni moja (ni fixed account-kuchukua hadi ndani tu,). Yule dada alienihudumia alinipiga elfu 20,000 bila Mimi kugundua maana sikuhesabu na ni kwa sababu alinipa za elf TANO nyingi na elfu kumi kidogo kwa hiyo nikaona uvivu kuhesabu. Baada ya muda mfupi kufanya baadhi ya mahitaj yangu ndo nikagundua nimepigwa 20,000 bank.

Wewe dada mwenye mwanya, mfupi, mwili wa wastani, mweusi kwa mbali uliyenipiga elfu 20,000 ktk tawi X hapo kanda ya ziwa acha hizo tabia ipo siku utaumbuka. Km humu umeskia.
 
daah😅

Naelewa inavyokua unapotafuta hela uliyokua unaitegemea.

Nimeshawahi poteza Jero kipindi kile Jero za NOTI

Nilitafuta ile hela nilirudi njia niliyopita hadi eneo nililohisi nimeidondosha kweli nikaenda nikaikuta.

Nilijikubali sana ile siku
😂😂😂Hatar sana
 
Nimekua ni mtu wa kuchukua Pesa mara kwa mara Bank na mara nyingi ni mtu ambae sikuaga na utaratibu wa Kuhesabu Pesa ninazo pewa toka BANK.

Lakini niwahakikishie wale ma teller either ni wao au mtu anaewapa yale maburungutu anakua anapiga hela.

Mara nyingi nikitoa Salio la maburungutu huwa unachukua yakiwa kwenye rubber band unapewa unatia kwenye BAG unasepa.

Kutokana na wingi wake huwezi kuhesabu hizo pesa mara zote huo ndio ukweli.

Haya maburungutu yapo aina mbili kuna yale ya NOTI mpya zinazokua na ki karatasi kushika noti zote (hizo hazina shida)

Kuna Hizi Burungutu ambazo noti zake ni Used unakuta zipo tayari counter pale kwa ajili ya kupewa wateja
👇👇👇
View attachment 2838836

Hizi burungutu Ndugu zanguni nawambia Ukweli nimejiridhisha kwa asilimia 100 na zaidi kwamba hata maburungutu huwa hayatimiii.

Si yote ila nakuhakikishia Ambae anabisha naomba afanye utafiti wake kisha arudi kunipa mrejesho.

Nimekua na kawaida sana ya kwenda Kuomba chenchi ninapokua nimeishiwa kwenye ofisi zangu.

Kwahyo unaweza PEWA burungutu la 2000,1000 na 5000. Mara nyingi kama mjuavyo biashara si muda wote wateja wapo.

Kuna nyakati wateja hamna mnakaa mnatizamana, Nikaona nijipe kazi ya kupanga Zile Noti za bank kwenye mafungu ya laki (noti za 5000) na 10k kwa (noti za buku na buku mbili)

Nikawa nahesabu hesabu hesabu, mara nyingi nakutaga upungufu kwenye noti za 2000 na 1000 ndio zinapochomolewa pesa.

Kila nikihesabu ni lazima kuna mafungu ntayakuta yamemiss 2000 na kwenye buku inamiss Buku.

Hawachomoi nyingi yani laki ya buku wanatoa buku na Laki ya 2000 wanatoa 2000.

Huwezi shtuka haraka utahisi umejichanganya, kilichonfanya nishtuke ni baada ya kuingia na hela kwenye chumba kisicho na pesa kabisa na begi langu nikamwaga pesa mezani kuhesabu.

Sikuamini nilihisi mazingaombwe kweli hela zimemiss.

Nikiumganisha DOTS nikapata majibu kumbe hawa watu hizi ndio tabia zao.

Unaweza jiuliza Teller anapataje marupurupu ila kumbe njia yao ni hiyo.

Wewe unae waamini BANK kwa kutohesabu pesa wanazokupa ipo siku utapga watoto wako wafanyakazi wako ukisema wamekuibia ila Nakwambia Leo hiii BANK ni WEZI mtapga watu wenu wa karibu mtawahisi na kuwafikiria vibaya lakini ukweli ni kwamba BANK kuna wezi wa kimya kimya.

Kama unaaamini hela bank hawaibi endelea.

Nimemaliza.
FNB kabla haijafungwa,coco plaza kuna braza man alinipiga laki 3...bahati yake nilikuwa nishaanza safari ndio nikastuka, nigemjazia nzi, usiamini mtu kwenye pesa,hesabu pesa zako ndio uondoke,na wakikujua unatabia ya ku count hawaibi!
 
Nadhani wanaona wakifanya hivyo watakuwa hawana tofauti na fremu za wakala
Mpaka mtu anapeleka fedha bank maana yake zimemzidi na anataka aiziweke haraka ili akaendelee na uzalishaji.

Madirisha yapo mengi ili kazi ya kufanya miamala iende haraka lakini imekuwa kinyume.
 
Levo zako mkuu,ndo watakuletea mlejesho.
Kwetu cc Kwanza Kama vile unataka tukujue unamiburungutu😄😄😄😄.

Anyway mashine huwa zipo za kuhesabia maburungutu mkuu.
Pesa nyingi unapewa chumba Cha falagha.
Kingine labda wenge lako mkuu⛷️.
Ziada,uchonganishi
 
Usisahau na hili.ukishtukia umepewa pesa bandia bank usijaribu kuwaambia wamekupa pesa bandia"

Ukifanya hivyo uta pigwa chini ya ulinzi na polisi walinzi na kupewa kesi ya uhujumu uchumi

na si hayo tu pia ni wa choleshaji kwa wale wazee wa front/gun man
Aisee Kuna jamaa aliwai nambia kapewa pesa bandia benki, ujue nilibisha mno[emoji848]
 
Back
Top Bottom