Bank tellers ni wezi wa kimya kimya, kuweni makini

Ilishawah kunitokea baadhi yao wana tabia za hovyo.
 
Hiibimenikuta juzi tu ila ni kwa wakala. Kwenye bikda la Million Moja aliweka 5000. Sasa nashangaa mashine ilihesabuje mpaka ikaweka 5000 katikati ya 10,000
 
Ilishawah kunitokea baadhi yao wana tabia za hovyo.
Mzazi/Mtu yeyote anaweza kuja kuhisi mtu wake wa karibu kamuibia kumbe kaibiwa huko huko BANK,Msala wanapata waliongia ofisini/nyumba/na wa kwanza kufungua SAFE..hao watu majumba mabovu huwaangukia bila sababu za msingi.
 
Bulk withdrawal unatakiwa kuingia ndani ili upate space ya kuhesabu kwa nafasi...
na Muda wa kuhesabu nao uwe nao,inakua na maana gani sasa hela zinatoka BANK uhesabu.

Tunakoelekea hata ATM machine nazo tutaambiwa zikitoa hela tuhesabu.
 
Bulk withdrawal unatakiwa kuingia ndani ili upate space ya kuhesabu kwa nafasi...
BANK wana mashine za kuhesabia,wanawalipa watu wana vitendea kazi vyote vya kuhakiki namba.

Halafu ananipa hela nianze tena kuhesabu nadhani huu utaratibu ni wa BANK zinazopatikana TANZANIA TU.

Huwezi mwambia mteja Wa BULK ahesabu hela,nihangaike zitafuta nakuzipokea napo nihangaike zihesabu.

USELESS BANKS, sioni hata maana yao sasa kama unaweza pewa hela pungufu kwa kisingizio makosa ya kibinadamu au sikuhesabu.
 
Laki ya buku 🤣🤣🤣


Hiyo sio nyingi mkuu ni kakutembea nacho mfukoni tu hako.

na shida sio kutembea nayo,shida ni uhesabu chenchi Milioni ya Buku.

Vibunda Kumi vyote uvihakiki,umalizane hapo uingie kwenye noti za buku mbili,uje buku 5 umalizie kuhakiki za ten ten.

Hapo ni BANK A unasafari ingine kwenda BANK B na C nk... hivi utahesabu hizo hela kila siku kwa ratiba hiyo?
 
Wewe unataka milioni ya buku kwa matumizi gani?
 
Atm inatoa mpka 10m inatokana na uwezo wa card yako...kuna card crdb inatoa 5m,kuna catd inatoa 10m kwenye atm
 
Na wafanyaniashara wakubwa sio wa viburungutu vya mil 5,10 hapo.
 
Kuna teller mmoja aliniibia alafu namjua nakumbuka nilienda kama million sita hivi,
Nikapewa maburungutu ya million milion yakiwa sita,
Nikaona kuyahesabu pale ni jau.
Nikatia kwenye begi nikasepa,
Kwenda kuhesabu huko mbele nakuta elfu thelathini hakuna,
Yule jamaa mpaka kesho huwa nammaindi kimoyo moyo,
Ni jitu la miraba minne, mnene sana, ukimuona ni kama mstaarabu hivi kumbe mwizi.
Nakubaliana na mleta mada KWA asilimia zote
 
Afu kwanini ukiwaambia issue ya tuangalie camera hawataki.....wanasolve kimyakimya,kwnini?

Kuna teller aliniambia pesa yangu imepungua 540,000....nilistuka sanaa,nkapiga hesabu zangu nikasema hapana tatizo lipo kwa teller....nkaongea na manager tuangalie kwenye camera,nikaambiwa niwape muda jioni watalishughulikia nikawa mpole,jioni nikapigiwa simu nikachukue pesa yangu.

Wapo mateller waaminifu na wengne sio waaminifu...ila kwenye pesa usimwamini mtu.
 
kibali cha kuview footprints za camera za bank ruhusa yake mpaka ifike kwa mwenye CRDB yani🤣🤣😅🤣
 
Mimi huwa sizipokei mpaka teller azipitishe kwenye mashine ya kuhesabu huko naona! Tena huwa natamka wazi naomba uzipitishe kwenye mashine nione.
nimeianza hiii kitu saivi naonekana mnoko kinoma wakiniona tu unaona kabisa body language imebadlika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…