Wakuu Kwema??
Mimi naishi Sinza (Makazi), na Shughuli zangu (Kazi) ni Posta. Mara zote hutumia njia hii ya kuanzia Sayansi mpaka Morocco napitiliza mpaka Posta. Njia hii toka inaanza kujengwa naiona, na mpaka sasa ilipofikia pia nimeiona. Na hata kabla haijajengwa hii mpya ya sasa still nilikua niitumia ile ya awali.
Hii barabara ilikua na njia nne, lakini sherehe fulani hivi za Uhuru nadhan kuna Mkuu mmoja akaamrisha iongezwe kua njia 5 na ikaongezwa. Sasa kuna kaujenzi kanafanyika pale sijui hata kanamaanisha nini. Kuta za fence zimevunjwa, parking zimeondolewa au kupunguzwa, Lami ya awali ikakwanguliwa ikawekwa ingine pamoja na kuweka vitofali lakini matokeo yake njia zimerudi kua nne.
Yaan baada ya Magazijuto yote hayo na gharama zote zilizotumika njia zimepunguzwa, nini sababu sasa hapa? Yaan gharama zote hizi zinazofanyika pamoja na kuwatia watu hasara ya kupunguza ukubwa wa parking zao lengo ndio kupunguza lanes kutoka 5 mpaka 4? Ili iweje?? Zile 5 za awali ambazo zilikua zinaacha parking za majengo ya watu salama zilikua zina shida gani?
Mwenye uelewa please msaada