Sasa huo si utaahira? Angalia mwendokasi zote jinsi zinavyojengwa, ile njia ya mwendokasi inakengwa sambamba na barabara za pembeni ili kuzihuisha na miundombinu za vituo, maji ya mvua, zebra crossing nk; hivyo lazima hii itakuja kufukuliwa hata kama si yote; ona BRT ya sasa toka Magomeni hadi karume, lazima barabara ya pembeni ifumukiwe kuendana na BRT lanes.
Halafu kwanini upunguze efficiency ya barabara toka njia 5 hadi 4 kwa excuse ya BRT? Kwanini usisubiri hadi ujenzi wa BRT uanze ili ifanyike moja kwa moja? Hebu niambie, ule ujenzi umeachieve nini ambacho hakikuwepo mwanzo zaidi ya kupunguza achievement iliyofsnywa nyuma toka njia 5 hadi 4? Goal ya mradi ilikuwa kuleta foleni au?