Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Wachana na hisia hit the target. Hujajibu hata point yangu moja unakimbia kimbia tu. Sikushangai ndio maana hata hoja za Mama Amon kule mwanzo hujajibu hata moja.

Bado niko pale pale siondoki, kuongelea haya mambo ya dini ni kupoteza muda bila sababu, binafsi sioni maana ya kuangalia watu kwa majina yao ili nianze kujiuliza kama huyu ni mwenzangu au sio.

Nimeshakwambia kule juu serikali ikifanya uhuni wake haiulizi dini ya mtu, unatakiwa umjue adui yako vizuri ili ujue namna ya kumshambulia, nyie naona miaka yote mnaruka ruka tu.

Kule Zanzibar Mwinyi katangaza Baraza lake la Mawaziri, asilimia kubwa ni waislamu, lakini sijamsikia mkristo yeyote au pagani akilalamikia hilo, HAKUNA.

Nyie wenyewe mko kimya kwenu mnaona ni sawa kwasababu kwa mtazamo wenu mnaona mmebebwa, miaka yote mnajiona dhaifu, mnaonewa, na hali hii ndio inawajengea tabia ya ubinafsi mnayotaka ienee kila mahali, na huu pia ni uthibitisho kwako wengine hayo mambo ya dini hatuna sababu ya kuyajadili, yanafupisha upeo wa fikra; if you think small you will remain small for life.

Halafu usinijibu issue yangu ya udini kwa kuchanganya na ukanda sijui ukabila, stick to the point, mimi najibu suala la udini pekee kwasababu huu ndio kama wimbo wenu wa taifa; wacha huo ukabila na ukanda wachangie wengine.

Mna tatizo la kisaikolojia. Siku nyingine mkija na hii hoja ya ajabu ajabu muwakumbuke na wapagani sababu nao hawana wakuwasemea.
 
Watanzania ,watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Umechelewa kufuatilia hii mada, Mama Amon alijibu kwenye page ya mbele zaidi ya hii mada, nikamjibu. Mods wakalichukua jibu lake kutoka page ya mbele alilojibia wakaliweka kwenye post ya pili ya page ya kwanza ya mada hii na pia baada ya jibu lake hilo nilifanya naye kadebate karefu kidogo tafuta hako ka mjadala kwenye page za mbele za nyuma za mada hii utaona

Kuhuzu Zanzibar ningefurahi pia kuona Mwinyi anaunda serikali inayoakisi demografia ya watu wa huko, Hata hivyo mimi nina interest zaidi na Serikali ya Muungano kwa Sababu serikali ya Muungano ndiyo serikali ya wote, ile ya Zanzibar ni ya Wazanzibari, sina hata haki ya kupiga kura huko kumchsgua shehia wala mwakilishi

Kuhusu Ukanda na Ukabila ni point ile ile tu ya demografia ya wajumbe waundao serikali, Kama ni halali kukemea sura ya ukabila kwenye uteuzi basi ni halali kutokubaiana na uteuzi wenye sura ya kidini

Kuhusu Waislamu kubebwa, ninatofautiana na wewe, infact Waislamu wamekuwa ni wachache kwenye fursa za utumishi wa kisiasa serikalini hii ilikuwa toka zamani, Hali iliboreka kidoogo wakati wa Kikwete, lakini Magufuli ndo kawasideline kupita kiasi, huyu kafanya too much mpaka aibu.

Kama hii nchi ni yetu sote tunategemea kuoba serikali yenye sura ya kitaifa kwa sababu watu wenye vigezo vya kushika nafasi mbalimbali wanapatikana katika watu wa imani zote.

Kuchagua watu wa imani moja kwa percentage ya kutisha kama alivyofanya Magufuli safari hii ni dalili za udini wa kutisha
 
Magufuli anaonekana mbinafsi na wewe hapa unasema serikali ya Zanzibar haikuhusu, ni ya wazanzibari! hauna interest nayo; kwani ile Zanzibar haipo ndani ya JMT?

Ndio maana nimekwambia hoja yenu ya udini zaidi inasukumwa na tabia yenu ya ubinafsi, kwasababu hata wapagani nao wapo Tanzania lakini sijawahi kuwaona mkiwasemea nao kila mara mnapokuja na hoja zenu za udini.

Hebu wacheni kupoteza muda na haya mambo ya udini muelekeze akili na fikra zenu kwenye mambo makubwa zaidi hili taifa lisonge mbele kidemokrasia na kiuchumi.
 
Sasa ubinafsi upi kuhusu Zanzibar?

Sipigi kura kule kumchagua rais wao
Sina haki ya kugombea kule hata kuwa mjumbe wa shehia
Sina haki ya kuwa muwakilishi

Zanzibar nitaiongelea zaidi kwenye mambo ya muungano , lakini hayo mambo yao mengine sina Interest nayo kivile. Naweza kuongelea kwa sababu ya uhuru wa maoni lakini siwezi kuwashikia bango sana ishu zao kama ishu za Serikali ya JMT pindi ikizingua kupita maelezo

Kama unaona kuna jambo liliokukera namna Mwinyi alivyounda serikali yake huko Zanzibar basi nawe unaweza kuiandalia mada, lakini mimi binafsi nina Interest na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Magufuli kuliko Hussein Mwinyi, Maana Sijawahi kushiriki uchaguzi huko na sheria inanizuia kushiriki chaguzi za huko za SMZ
 
Mzee wangu umeandika vitu vingi sana embu hitimisha kwa kutueleza ulipendelea Rais ateue Mawaziri kwa kuzingatia imani zao?

Na kama ni hivyo kwani hawa Mawaziri wanakwenda kufanya kazi za Kanisa au Misikiti?

Swali la mwisho, una hakika gani kuwa hao unaowaita Wakristo na Waislamu wanafuata misingi na mafundisho ya imani zao? Wewe ni mtu wa zamani kidogo unafahamu mwanasiasa ni mtu wa aina gani.

Shirki! Shirki! Shirki!
 
Nchi ipi au ile maamuzi yake yote yanaamuliwa tanganyika
 
Sasa kuna nani mwingine kwenye maCCM yaliyopo Bungeni anayeweza kuwa na elimu sawa au ya kumkaribia Kitila na Nchemba?
 
Hilo la wanawake lilikuwa wazi sana, wangetemwa wengi tu, mtazamo wa mzee kwa wanawake uko kipuuzi mno.
Kama Unalea binti nyumbani kwako ukileta habari ya kumfanya yeye ni special.. utampotezana kumharibia maisha..

Yeye ni binadamu aliyejaaliwa kuwa mwanamke.. kama anataka chochote maishani she has to put in equal work.. usitake uwaziri kisa wewe ni mwanamke.. upate uwaziri kwasababu unaweza.. kuliko wengine.
 
Lini hili limetokea to support your claims!?
 
Full stop... wewe una ubinafsi unajificha nyuma ya Udini. Maana wenye dini kweli hawana husda wala Kijicho kama wewe.

Unachokiongea wewe ni shirki.. kujifanya kujua ya kesho wakati Mwenyezi Mungu amekupa leo uipokee na uishi.. tayari uko hapa na mwenzako Zanzibar-ASP nyie mshaona mabaya yote hata ambayo hayajatokea..

Huo ndio Uchawi na Ushirikina unaotajwa katika vitabu vya dini. Acheni kuuchafua uislamu kwa upotofu wenu.
 
Hayo uliyoandika yakitekelezwa na kuzoeleka yatakuja kuleta vurugu na kuvunja amani nchini. Watu wateuliwe kwa sifa zao za kiutendaji nidhamu na maadili kazini. Tusije muda rais kabla hajateua waziri Muft anaambiwa pendekeza waislam wanne wa kuingia baraza la mawaziri au askofu anaambiwa hivo. Ndugu tutaiharibu nchi.
 
KATIBA,SHERIA,KANUNI ZINASEMAJE KUHUSU BARAZA LA MAWAZIRI:?

Katiba yetu ibara ya 54 inasema Mawaziri watatokana na wabunge ila hakuna sifa za Udini,Ukanda, Jinsia, Hali ya Ulemavu, elimu nk


Kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania ya 1977 ibara ya 4(1) inasema kwamba " Shughuli zote za Mamlaka ya NCHI katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na Vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji,vyombo viwili vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji HAKI na pia Vyombo viwili vyenye Mamlaka ya KUTUNGA sheria na kusimamia utekelezaji wa Umma.

ibara ya 4(2) imefafanua vyombuo viwili kuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Zanzibar, Vyombo viwili vya Itaoji haki ni Mahakama ya Jmahuri ya Muungano na Mahakama ya Zanziar na Vyombo viwili vya kutunga sheria ni Bunge la Muungano na Barazala la Wawakilishi.


ibara ya 4(3) inatajja mambo ya Muungano........

ibara ya 4(4) inasema kwamba "Kila chombo kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti mengine yaliyomo katika katiba hii.

Sasa kwa kuchangia huu mjadala wenye Hoja dhaifu 3 kuhusu baraza la Mawaziri kwamba
(i) Limejaa Wakristo wengi,
(ii) Kwamba hakuna Wazanzibar
(iii) Kwamba limejaa Wanaume na watu Ukanda wa Ziwa (Demographical variables)


Nilitegemea watu wanukuuu angalau Kifungu chochote cha Katiba/ sheria ambacho Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri atakuwa amekiuka au basi tuseme tunamhukumu kwa kutumia mazoea- mila/norms au maelekezo ya Chama kinachotawala.

HOJA kubwa inayotaka kujengwa ni ya UBAGUZI-DISCRIMINATION.

Katiba inasemaje?
Katiba yetu ibara ya 13(4-5) inapinga aina zote za ubaguzi bila kujali ni aina gani,iwe Dini,kabila,ukanda au Jinsia.

13(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa Kazi au shughuli yoyote ya madaraka ya Nchi
Ni nani anayesema kwamba amebaguliwa? UBAGUZI ndio HOJA kuu hapa; Kuna Mzanzibar anasema kwamba yeye ana haki ya kuwa Waziri ila amebaguliwa?

Kuna Mwanamke anayelalamika kuwa ameachwa kwa sababu ya Jinsia yake?
Kuna Mtu wa Mkoa wowote anayelalamika kwamba ameachwa kwa sababu ya Mahali alipozaliwa?

Ili kupata Majibu ya Maswali hayo, Katiba yetu ibara ya 35 (2) inasema kwamba Ofisi yeyote ya utumishi wa Umma itatatekelezwa kwa NIABA ya RAIS, yaani mwenye Ofisi nni Rais ila Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa MIKOA au Wilaya wanamsaidia tu, Rais huweka mtu ambaye akimwamgalia anajiona yeye,anaona mategemei yake.


Funga Kazi ni ibara ya 37 ambayo walioitunga waliona mbali,inasema kwamba " Rais halazimishwi kufuata ushauri wowote katika kufanya maamuzi yake---hata Bunge linaweza kushauri ila Rais habanwi wala halazimishwi kufuata huo ushauri, You knwo why? Ili kumpatia Rais uwanja mpana wa kutekeleza Katiba kwa minajili ya Haki,

Sasa basi, Sheria inasema kwamba " Yeyote anayeteuliwa na Rais is working for the PLEASURE of the President; yaani if the President is not pleased with you, He will dismiss you on that good moment/minute/second.


Kwa ufupi kabisa, hadi Juni 2021, kutakuwa na Wazanzibar zaidi ya 2 kwenye Baraza la Mawaziri, kutakuwa na Wanawake zaidi ya 5 kwenye Cabinet, na watu wa Mikoa/Kanda zingine zinazoona haijaingizwa kwa Cabinet; utauliza nimejuaje? Kila timu inakuwa na Wachezaji 11 uwanjani ila kunakuwa na reserve List in case of majeruhi, RED CARD, or whatever Mchezo lazima uendelee; hata Simba SC Juzi mliona akina KAGERE waliingia dakika ya 85

Pili, Ukiangalia Size ya Manaibu Mawaziri 23 ni idicator kwamba ni waiting list ya kuingia kwa cabinet ndani ya muda mfupi, Wazanzibar wapo 3, wanawake manaibu are 4,Mikoa na Kanda mbali mbali wapo wengi.

Tunachoweza kufanya kwa mujibu wa Katiba hii,ni kumwombea Rais na Washauri wake HEKIMA, BUSARA NA AFYA NJEMA ili Mungu mwenyewe awafunulie SIRI zake ambazo hata sisi hatuzijui. Ingekuwa Katiba yetu inasema Mawaziri LAZIMA wathibitishwe na BUNGE-WANANCHI, hapo wanaolalamika wangekuwa na HOJA za kutaka kuwe na mabadiliko, kwamba Bunge liwakatae baadhi ya Mawaiziri ili kuziba malalamiko yao, huo mlango haupo kabisa.

Labada Katiba yetu iseme kwamba kwenye Wizara 5 za Muungano, Kila Pande ya Muungano iwe na Uwakilishi ndani ya Baraza la Mawaziri na iseme kati ya Wizara atazounda Rais, 3 lazima 1/3 iwe ni Wanawake; hapo kutakuwa na Nguvu ya Kikatiba na itakuwa ni kufuata tu.
ILANI ya chama inasemaje?
 
Kumbuka Mh. rais kaweka wachapakazi tu, sasa uweke Waislam wengi nani atafanya kazi ikiwa kila muda inabidi atoke kazini aende msikitini au ajifiche chooni kusali swala 5? Mh. anapohitajika haonekani kisa anaswali tena wakati wa kazi...kuweni serious jamani. Mimi hapa naona ni wachapakazi tu na sioni dini.
 
Kwani marais waliyopita hawajaviona hivyo vifungu vya katiba? Mbona hatujakuwa tukisikia hizi kelele? Lisemwalo lipo na kama halipo laja.
 
Nakazia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…