Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Katika hii taarifa kuna hoja za msingi na zingine hapana.

All in all,CCM hiyo katiba pendekezwa itawatokea puani maana mmeharibu karibu kwenye kila eneo/idara.

Nakubaliana na wewe mkuu kwenye Paragraph yaw kwanza

Then hiyo paragraph ya pili Maccm ni mawatu madikteta sana, si umeona hapo kwa mujibu wa Tamko la Jumuiya na Taasisi za kiislam, ni kwamba, Yanafanyiwa mapendekezo ya namna yaw kubadirisha SHERIA YA MABADIRIO YA KATIBA. ccm wamegundua hata wafanye nini Katiba yao haipiti kwa namna yoyote ile, Hivyo wameleta mapendekezo hayo ili pamoja na mambo mengine wabadiri kile kifungu kinachosema KATIBA HAITAPITA ENDAPO THERUTHI MBILI HAZITAPATIKANA KWA PANDE ZOTE ZA MUUNGANO.

Hapo ndipo ulipo ubovu wae kamba yao, hata wafanyeje, waibeje Theruthi mbili kamwe haiwezi kupatikana kwa pande zote za Muungano sasa hapa wanakwenda kucheza tena na uhuni wao watuletee mapendekezo ya kuondoa vifungu hivyo. Binafsi nitawashangaa sana Wapinzani kuingia kwenye kura ya maoni kama. kifungu hicho kikiondolewa.

Nadhani kama ni funzo tumelipata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Ccm hawako tayari kuumbuka kwa namna yoyote ile, tusubiri

BACK TANGANYIKA
 
Hivi wale waliokwenda kuhiji si waliipigia kura katiba pendekezwa kwa njia ya email, inamaama hawakujua kama mahakama ya kadhi haikuwepo! ama kweli ccm kiboko ya waislam!

Ngoja kwanza, subiri, Waislam tushauriane, hawa kama ni BAKWATA kutakuwa kuna walakin unless kama Mufti kaona siku zake zinakaribia na kaamuwa kwa dhati kurudi kwa Waislam wenzake na kuachana na system.
 
Nakumbuka kipindi cha uchaguzi kilichopita baada ya jk kuona waislam walipotoa msimamo wa kutoipigia kura ccm jk akiwa kama mgombea wa uraisi aliahidi kama mtaipigia kura ccm basi nitahakikisha mahakama ya kadhi inapatikana. Baada ya kuingia madarakani jk huyohuyo akasema swala la mahakama ya kadhi haliwezekani. Sasa safari hii waislam tusipokuwa na msimamo wa kuipigi kura ya hapana hii katiba yao pendekezwi ndio itakuwa mwisho wa hili swala.
 
Kama mahakama ya kadhi itawaajiri Wakristu pia sitakuwa na tatizo,kinyme na hapo itakuwa ngumu kuunga mkono wazo.
 
Institutionally Bakwata ipo upande wa Ccm. Huko kwa wagala ni individual's corrupt mind ndo wanasupport.
Kwa taarifa yako,expect nothing as Kadhi court under this Bs Ccm reign. Hata sasa mtapigwa tobo na mtakubali. wameshawajulia weakness yenu,
Kuna popote nimezungumzia mahakama ya kadhi zaidi ya ku-dis tabia zenu za hovyo hovyo zinazoonesha as if wanaoichagua CCM ni Waislamu peke yao wakati kura za Wakristo nazo kila uchaguzi zinamiminikia huko huko CCM!!! Institutionally BAKWATA ipo CCM; well, sasa kuna tafsiri gani viongozi wa juu kabisa wa kanisa wanaposimama hadharani kumpigia debe mgombea wa CCM? Wakristo wa nchi hii kama kutokipenda basi hawaipendi CUF lakini CCM si ajabu nyie wengine mnaojifanya kui-dis hapa hata baba na mama zenu wanaipigia kura CCM!!! Na kama si kwa ajili ya kura za Wakristo basi CCM ingekuwa imeshatoka madarakani kwahiyo danganyaneni wenyewe kwa wenyewe wakati mnajua kabisa deep inside your heart Wakristo mna mchango mkubwa sana katika kuifanya CCM iendelee kuwa madarakani....
 
Wewe unaongea kama nani kwenye hii nchi.

Ritz hata ungekuwa wewe raisi kesho... nakuhakikishia utamaliza miaka yako 5 au 10 na hutabadili kitu juu ya hili suala...
huo ndo uhalisia
 
mahakama ya kadhi kila muislam akaanzishe nyumban kwake watanzania hatutaki unyama wa hadharani
 
Kodi za wakristi haziwezi kutumika kuanzisha na kulipa mishahara ya mahakimu na majaji wa mahakama za kiislamu,na kumbuka serikali ya tanzania haina dini.hili suala haliwezi kamwe kukubalika hata cku moja ndani ya nchi hii,mkitaka hamieni nchi zenye mfumo wa sharia.just different day same old shit
 
Ndugu zangu Waislam, nilichokipenda zaidi hapa ni hitimisho kwamba mtapiga kura ya Hapana dhidi ya katiba pendekezwa. Hapo safi sana

Ila kwenye swala la Mahakama yenu kulipiwa kuendeshwa kwa kodi zetu wote, hapo Hapana.

Nimeshangaa sana kuona viongozi hawa wakubwa wanahoji kwa nini Mahakama ya Kadhi isighalamikiwe na Serkali kama inlivyo kwa ''
Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara n.k.;
nimeshangaa sana hoja hii
 
Hapa kuna mchanganyo. Habari ina kichwa kuwa ni Tamko la Baraza kuu la Waislamu Tanzania ambayo ni Bakwata lakini tamko limesainiwa na Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu (T) sasa hapa lipi ndio sahihi.
 
Ni lazima Serikali iwaambie waislam ukweli. Lazima tukubali kwenye nchi ambazo zina serikali za ki-secular kama ya kwetu ni ngumu kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu kama za Saudi Arabia au Kuwait.. Hata huko Zanzibar mtu akiiba hawampeleki kwa kadhi ila Jamhuri ndiyo inamfungulia mashtaka....

Lazima tufahamu sheria zimegawanyika katika mafungu mawili makubwa..

(i) Public Law.. Hizi zinalinda maslahi mapana ya umma kwa maana ya Jamhuri, Mfano sheria za jinai nk. Hapa mtu akifanya kosa anashtakiwa na Jamhuri... yule uliyemdhuru anabaki kuwa shahidi tu.. hapa hakuna dini, kabila, utamaduni wala rangi ya mtu.. Kama umefanya kosa lazima utashakiwa kwa kuvunja sheria za nchi na kwa minajili ya kulinda maslahi mapana ya taifa..

(ii) Civil/private Law.. Hizi zinasimamia maslahi ya mtu mmoja mmoja.. Mfano sheria za mikataba, ndoa nk. Hapa ni mtu vs mtu.. na sheria itakayotumika ni ile ambayo kosa limeangukia.. Kama ni mgogoro wa ndoa basi mgogoro utatatuliwa ama kwa kutumia sheria za kimila kama ndoa ni ya kimila, kama ni ya kiislam itabidi utumike utaratibu wa kiislam vivyo hivyo kwa ndoa ya kikristo..

KWANINI MAHAKAMA YA KADHI NI VIGUMU KUFANYA KAZI TANZANIA.??

Mahakama ya Kadhi inaendeshwa kwa kutumia Sharia Law, kwa maana ya kitabu kitakatifu cha Quran, Hadithi za Mtume nk. na lazima utambue kuwa Uislam ni mfumo uliokamilika kwa maana ya taratibu, sharia, mira, desturi, imani/dini vyote vinakwenda kwa pamoja. Sasa ili Mfumo huu uweze kufanya kazi kwa ukamilifu wake unahitaji watu wenye tamaduni, mila, desturi imani/dini moja.. Hivyo Sheria zake zinakuwa rahisi kusimamiwa na Serikali kwa sababu watu wote ni wa Mfumo mmoja..

Lakini kwa nchi kama ya kwetu yenye mchanganyiko wa sio tu dini, bali pia tamaduni, desturi mila na kadharika ni ngumu ku-impliment Sharia Law.. Na kwa sababu tunaishi katika Jamhuri mmoja lazima kuwepo na mfumo ambao utaweza ukawajumuisha watu wenye imani, dini na tamaduni tofauti.. yaan Secular state...

Kwa mchanganyiko wa jamii yetu.. kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu ni ndoto za mchana na lazima Waislam wakubali ukweli huo.. Chukulia Mkristo kaibiwa na Muislam.. au Muislam kaibiwa na Mkristo utatumia Sheria gani hapo ili kutenda haki????

Lazima ukweli ubaki ukweli!! Tatizo limeletwa na CCM kwa kuwapa Waislam matumaini makubwa yasiyotekelezeka ili wajipatie kura..

Niwashauri tu ndugu zangu waislam lazima tujitahidi kujenga Taasisi zetu zenye nguvu, ueledi na fedha ili kuwatumikia waislam kwa yale mambo ya kiimani na kijamii tu. La sivyo hakuna kitu hapo..

 
Alafu na sisi waislamu bwana tuna shida sana, bado hatuna uelewa wa pamoja katika maswala yetu. Maana tunapoisema CCM imekataa, maana yake tunamuweka wapi mwenyekiti wa CCM, ambaye ni mwenzetu katika hili. Ni nini msimamo wake katika swala hili. Maana sijawahi hata siku moja kumsikia akionesha msimamo wake hadi sasa miaka yake 10 inakwisha, angekuwa ni mgalatia tungesema wakristo wanatukwamisha, lakini mmmmhhh!!
Rais JK alishawahi kuweka wazi msimamo wake kuhusu hili kwenye sikukuu fulani iliyofanyika kwenye Msikiti wa Gadafi pale Dodoma Mjini mbele ya viongozi wote wa waislamu na hotuba yake kurushwa moja kwa moja TBC. Katika hotuba yake aliwataka waislamu wenzake wagharamie ibada zao wenyewe, akamnukuu Mufti kwamba "Mufti anasema Mahakama ya kadhi ni ibada. Sio jukumu la serikali kuendesha ibada za dini yoyote bali ni jukumu la waumini wenyewe wa dini husika." Huo ndio msimamo wa JK, na nafikiri kuna uzi mreeeefuuuu ulianzishwa humu na wadau wakijadili msimamo wa JK.
 
Siku za mwongo ni fupi, ni hawa hawa waliokaa kimya wakati wenzao walipopigishwa kura feki kwa njia za kichawi, kura haramu za kwenye mtandao, na nyingine alizooteshwa kwenye ndoto Samweli Sitta, bila kusahau za kupigishwa marehemu, na wale waliohamishwa kimiujiza Zanzibar.

Hawajitambui wanaotoa matamko sasa. Kama walipewa peremende wakakubali katiba feki, sasa matamko ya nini? Waishi katika kweli nayo itawaweka huru...............

Labda waikatae katiba mpya kwa sababu za msingi zaidi, na madhaifu mengi yaliyojaa kwenye hiyo katiba haramu, sio kuitumia kama chambo cha cha kupitishia/kurekebishia sheria iliyotungwa.

Hawa watu hawajui kuwa hiyo sheria hata ikiruhusu pesa za watanzania kuhudumia hizo mahakama, mwisho wake ni Mwezi April, pindi katiba wanayoitumia kama chambo kutishia serikali, endapo itapita???

Kuna tatizo kubwa la uelewa wa hawa wenzetu....., Waonewe huruma tu....

Halafu walivyo wabinafsi,ubovu pekee wa Katiba pendekezwa ni kukosekana kwa Mahakama ya Kadhi.
 
Kwa nini waislam mnalazimisha serikali kusimamia dini yenu? Ikiwashinda si muachane nalo? Kwani nani anawalazimisha?
 
Astaghafilullah kafiri weye unaongea ufirauni mwanakharam mkubwa weye..Hahahahaha...:glasses-nerdy::biggrin::biggrin:
Hii kitu wangeikomalia Ccm wangeharisha maji..lakini wenyewe kwa wenyewe wanafitiniana. Hapo utamsikia yule Shekh wa mkoa wa daslama,mnafiki yule anakuja kuunga mkono hoja ya "subra" kumlinda kikwete..ptyuuuuu!!!

Acha uquma mngese ww, iyo mahakama itaendeshwa kwa pesa kutoka chanzo kipi????umekalia kuita wenzako makafiri wakati nyie ndo makafiri mnaofikiri kwackutumia makario na mtahangaika sana hakuna cha mahakama ya kaadhi wala kazi manina.
 
Mimi si muislamu na sitaki kuamini kua uanzishaji wa mahakama ya kadhi hapa Tanganyika utakua na athari kwa taifa.Mi nadhani ianzishwe tu mbona nchi nyingine wana mfumo huo na hakuna shida?.Mwaka huu msikubali ahadi.

Leo wapinga Uislam mpo na Waislam, amma kwa hakika Uislam una nguvu za ajabu.
 
Waislamu hawana nia ya dhati ya kutaka mahakama ya kazi,wamejaa unafiki na kimbelembele kwa chama tawala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom