Baraza la Maaskofu TEC linapobariki pesa chafu za CCM

Acha pombe na mambo ya kipunga

Or else utaishi kwa shida na taabu sana
 
Kwa maneno yako haya hata post yako haina maana tena. Kwa lugha yako chafu huna moral authority kulisemea kanisa, hebu kajipange upya, wakatoliki hawako hivyo, rudi kwa aliyekutuma.
Huyo alikuja kijinga na anajibiwa kijinga!! Hii haibadili ukweli wa mada kuu ya uzi
 
Sio kila msaada, na sibwa kila anayetoa, ikitokea kwenye Taasisi yenye movement ya USHOGA?? USAGAJI,ipokelewe tu kisa ni misaada??
 
Bila kupepesa macho una hoja za msingi sana hasa zinahusu maadili ya kanisa

Mimi mwenyewe ni mkatoliki wa kuzaliwa kuishi na kufa lakini viongozi wetu aisee hizi dhambi wanazozibeba ni kubwa sana

Jimbo la Morogoro kipindi msimbe ni monsignor na anatawazwa kuwa mkuu wa Jimbo deni la Jimbo lilikaribia takribani billion 2 shs na hakuna maelezo yaliyojitosheleza kuhusu hizo hela zilipotomika. Siku hizi watumishi wa Mungu wamekuwa mawakala halisi wa shetani hatuna tena viongozi mashuhuri na weledi kama akina askofu Adrian mkoba. Na ukijaribu kuongea watakukasurikia na kukuona vitisho.
Ninafurahi watu wenye mapenzi halisi ya kanisa mpo, msiache kukemea uovu ndani ya kanisa wala kusema ukweli na katu hatutaikana Imani yetu kwa ajili makosa ya wadhambi kadhaa, kila mtu alilikuta kabisa na ataliacha lakini misingi ya kanisa itadumu dawamu

Kuishi ni KRISTU na kufa ni faida
 
Aksante sana ndugu katika imani,umeachangia Uzi kwa weledi bila mihemko kama wanavyofanya wengine.

Kuhusu Morogoro Mhashamu Askofu Lazarus Msimbe SDS, akiwa Bado msimamozi wa Jimbo mara baada ya kupewa hiyo nafasi alishauriwa afanye mabadiliko bila kuchelewa ya ofisi ya mhasibu wa jimbo.

Lakini kama ujuavyo Mhashamu Msimbe ni laizer affair, sio mtu wa caliber ya u aggressive kama alivyo Askofu Dalu, ni Mtu wa kuangalia watu usoni.

Nafasi hiyo mpaka anakuwa Askofu kuteuliwa Mwasibu wa jimbo alitumia vibaya, na huku msimbe akijiona mpita njia, maana ukipewa kuwa Administrator wa jimbo sio lazima baadae uje kuwa Askofu.

Kuhamaki Vatican ikamtangaza, najua sasa atakuwa anajilaumu kwa kosa la kutochukua hatua Toka akiwa administrator wa Jimbo.

Hiyo ni aina ya Msimbe hata alipokuwa mlezi wa wanovisi SDS Nakapanya, na Provincial Wanachama wa SDS walimfurahia kama Baba Mwema hakuwa mkali sana.

Nirudi kwenye mada kuu, kama wakristu wakatoliki lazima tuseme kweli kwa ajili ya kanisa Katoliki, kuhusu miamala hii katika kipindi hiki Cha uchaguzi.

Aksante sana.
 
Wewe ndio mweupe kabisa, unasema "mantiki logic " unachanganya lugha mbili. Sema tu huna mantiki.
 
Ninge penda kuku'engage' wewe kwa utulivu ila muda hauruhusu. Ninakuona unang'ang'ania unayo dhani/fikiri wewe na kufanya kuwa ndiyo sababu ya uwepo wa kanisa. Unashindwa au kwa maksudi unajifanya kuliona kanisa kuwa mali au kuwa hao watumishi wake binafsi, dhana ambayo ni wazi potofu.

Huwa sipendi mijadala hii ya kiimani na kuichanganya na maswala ya kisiasa, ambayo sasa wanasiasa wenyewe wanalazimisha hizi imani ziwe sehemu ya kufanyia uchafu wao, na watu kama wewe mpo tayari kuwa mawakala wa shughuli hiyo.
Nimekwisha elewa maana ya wewe kuleta mada hii haa, kwa hiyo sina sababu tena ya kuwa mshiriki nayo.
 
Mimi sijaanzisha mada hii.
 
Tatizo mama wala sio uchaguzi mkuu. Kitendo tu cha kuchukua pesa ya serikali kwa namna inavyotolewa na kupokelewa is intrinsically evil!
Waamini ndio wana wajibu wa kwanza wa kulitegemeza kanisa na sio serikali. Kwa wabobezi wa historia ya kanisa hiyo sio dhambi mpya. Mababa watakatifu tangu enzi waliweka wigo kati ya shughuli za kanisa na serikali!
Mafungamano hayo ya serikali na kanisa yana mchango mkubwa hasi wa kuliporomosha kanisa!
 
Kumbe hujui neno vipaji? Siyo akili ni michango kwa kanisa katoliki
Unategemea nijue misamiati ya huko, kwani umeambiwa mimi ni mtu wa huko?
Shetani anapotoa michango huko naye huwa anasemwa kuwa ana "vipaji"?
 
Bado hujajibu chochote kati ya mada nilizoandika.
Completely you are Out of context,out of proportional

Naandika ukweli sio chuki, kanisa langu Katoliki linaenda siko over.

Hili ni la kupigia MAKELELE npaka wasikie na waseme.

Haiwezekani wakawa wanahongwa pesa tena kwa jina la Mgombea wa Chama .... Hii ni RUSWA!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…